Luca Paguro
JF-Expert Member
- Mar 26, 2023
- 502
- 1,141
Mkuu,Watanzania wanahitaji kukombolewa kifikra kwanza. Wengi wao wamezoea na wameridhika kuishi kwenye umasikini. Hawafikirii mbali
Tanzania hakuna demokrasia bali kuna maigizoMkuu,
Demokrasia ni kila mtu achague chama anachoona yeye kinafaa. Wenzio wameamua kuchagua CCM (kwa sababu yeyote ile) waheshimu usidhani hawana akili. Kama wewe ulivyochagua Chama kingime (kwa sababu zozote zile)
Demokrasia ni kuheshimu mawazo na chaguzi za wengine. Africa tuna tatizo la kutokujua mipaka ya demokrasia. Sio kw achama tawala au upinzani...
Tanzania hakuna demokrasia bali kuna maigizo
Tanzania hakuna demokrasia wenye akili na werevu wanalifahamu hili na wala haihitaji mabishanoNa hayo maigizo ni kwa pande zote mbili - Chama tawala na Upinzani. Yaani mdani ya mioyo yetu hatuamini katika demokrasia ila tunataka demokrasia. Ndiyo maana ni rahisi kuwabeza wemgine wanaochagua tusichokiamini.
Dah.. Japo mimi ni Mngoni ila nachukulia sana Ruangwa ndio kwetu, maana nimezaliwa na kukulia huku; hadi leo hii nina miaka 19, familia yetu haijawahi kuhama Ruangwa
View attachment 3478167
Huku wanashangilia sana CCM kwa sababu kipindi cha Magufuli, Majaliwa alijitahidi kuleta maendeleo lakini wananchi hawaelewi kwamba hayo maendeleo yaliletwa kwa sababu ya Majaliwa, sio kwa sababu CCM inajali sana Ruangwa
Tangu nimezaliwa Ruangwa kuna shida ya maji na serikali haikuwa hata na mpango. Hadi leo hii 2025 huku maji ni shida, yakijitahidi yanatoka mara mbili kwa wiki. Siku nyingine yanatoka maji machafu tena mekundu kabisa. Maji yenyewe ya chumvi ila wanatubania kinoma. Huku bila kisima hutoboi
Kuna muda mnakaa wiki nzima maji hayatoki
Halafu mwaka 2023 Rais Samia alikuja Ruangwa eti wananchi wakamwambia hatuna changamoto π₯
Yani mpaka leo, Ruangwa bila Majaliwa ingekuwa mbovu zaidi ya sasa
Na sasahivi Majaliwa anaachia madaraka, hamna tena atakayeikumbuka Ruangwa. Huku maendeleo ya kawaida sana (ambayo kwenye mikoa na wilaya nyingi za Tanzania waliyapata kitambo) ila huku Ruangwa ndio imetumika kupumbaza wananchi kwamba CCM inawajali
Hii wilaya tayari imeshakuwa Pro CCM na leo Rais anakuja huku, wananchi wamefurika kwenda kusikiliza uongo wao kwenye siasa bila kujua kuwa ndio mwisho wa maendeleo, masikini ya Mungu.
Majaliwa anatoka madarakani, so no one cares about Ruangwa anymore. Natamani wananchi wangeliona hili wakatae wahuni mapema.
Kuna muda namuomba Mungu ukubwani niwe na hela nije kuinvest wilayani kwetu mwenyewe.
Huku kwetu kila kitu tupo nyuma, licha ya miaka 60 ya uhuru na wananchi hata hawajali π₯π₯
Unaelezea vipi tukio la wana Ruangwa kumwambia Samia kuwa hatuna changamoto πMkuu,
Demokrasia ni kila mtu achague chama anachoona yeye kinafaa. Wenzio wameamua kuchagua CCM (kwa sababu yeyote ile) waheshimu usidhani hawana akili. Kama wewe ulivyochagua Chama kingime (kwa sababu zozote zile)
Demokrasia ni kuheshimu mawazo na chaguzi za wengine. Africa tuna tatizo la kutokujua mipaka ya demokrasia. Sio kw achama tawala au upinzani...
ππππππNilipita ruangwa two months ago, mchana kweupe saa 7 eti hakuna usafiri tusubiri guta moja linaenda pale mbele ya njia panda ya mandawa kule mto mbwemkuru lijae jae ndo tuondoke.View attachment 3478180
Bahati jamaa mmoja akaniona nina heshima zangu akaniambia kuna dogo ana pikipiki anaenda huko kakae kule mbele abiria wenzio wasikuone, ndo nikawekwa katikati ya mtu na kiroba cha mahindi ikawa pona yangu nisinyooshe miguu kwenye guta.
Yaaan vijana wakipewa tisheti, na buku ya kununua kitoko, bas wamemaliza.Wanashangilia vitenge, vilemba na kofia, hapo wananuka umasikini hatari.