GE2025 Kila nikiona wananchi wa Ruangwa wanavyomshangilia Samia naishiwa pawa

GE2025 Kila nikiona wananchi wa Ruangwa wanavyomshangilia Samia naishiwa pawa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hatari sana kiwango cha ujinga cha wa tz ni asilimia 95 ila ccm nao wako dhohofu san maana magari yaliyotutusa watu kuwatoa liwale masasi lindi ni weng sana nami nipo hapa uwanja wa maonyesho nna hasira natamani niwe hamza
Mi leo sijatoka home, nilikuwa nasubiri wamalize kampeni ndio niende zangu kitaa. Sasa wameshaondoka, na ziara yao hapa hamna cha msingi alichoongea Samia, nilikuwa naangalia kwenye TV.
Anasema eti wamejitahidi kuboresha huduma za maji Ruangwa, yani hiki kitu kinaniuma sana. Maji huku ndio shida kuu
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Mkuu,

Demokrasia ni kila mtu achague chama anachoona yeye kinafaa. Wenzio wameamua kuchagua CCM (kwa sababu yeyote ile) waheshimu usidhani hawana akili. Kama wewe ulivyochagua Chama kingime (kwa sababu zozote zile)

Demokrasia ni kuheshimu mawazo na chaguzi za wengine. Africa tuna tatizo la kutokujua mipaka ya demokrasia. Sio kw achama tawala au upinzani...
Yes kila mtu ana uhuru wa kuchagua kitu anachoona kinafaa lakini haiondoi ukweli wa kipi kinafaa na kipi hakifai.

Yaani ati mgombea anakuja na sera ya kuhamisha bahari toka dsm kwenda Moro umpigie makofi na kuamini sera zake, mtu anakuja na sera ambazo kiuhalisia hazitekelezeki na hazijawahi walau kuwahi kuanza kutekelezwa halafu wewe umkubali na kutaka kumpigia kura tusione kua kuna mahali hauko sawa.

Matapeli huwatapeli watu wenye tamaa na wasiofikiri mara mbili.

Wana uhuru wa kuchagua na wengine wana uhuru wa kukosoa machaguzi yao, kushawishi wachague vinginevyo as long as hawavunji sheria.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
MImi binafsi nimerudi kwenye ile hali ya kubagua wana CCM kama ilivyokua 2010 - 2015, nikiona hata mtu wangu wa karibu anajihusisha na CCM ama kuiunga mkono automatically anaingia kwenye black list, tutaishia kuchekeana kwa nje tu ila siwezi kushiriki jambo lake lolote
Ukiona shekhe au Padri kaingia CCM basi hawo ni wanafiki.
Huna ushekhe wala upadri ndani ya CCM.
CCM ni fisadi mkubwa na mnyanyasaji. kwa kweli sio Chama lakini wale viongozi ndio huwa waungu watu.

Ukiingia CCM basi uwe tayari kuwa abudu waungu watu wanaojiita makada
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Mkuu njoo Kwa Akulumombo au kwaMtota hapa upate chupa ya mdafu tupoze koo
Hatari sana kiwango cha ujinga cha wa tz ni asilimia 95 ila ccm nao wako dhohofu san maana magari yaliyotutusa watu kuwatoa liwale masasi lindi ni weng sana nami nipo hapa uwanja wa maonyesho nna hasira natamani niwe hamza
 
Unaelezea vipi tukio la wana Ruangwa kumwambia Samia kuwa hatuna changamoto 😔
Yaweza kuwa wameandaliwa; lakini ndiyo siasa za demokrasia na vyama ziko hivyo dunia nzima... kama hadi Harris alipata kura nyingi tu kwenye uchaguzi wa US; unadhani utashangaa watu wakisema hawana changamoto kwenye mkutano wa kampeni za CCM Mkuu? Tujadili uhalisia
 
Yes kila mtu ana uhuru wa kuchagua kitu anachoona kinafaa lakini haiondoi ukweli wa kipi kinafaa na kipi hakifai.

Yaani ati mgombea anakuja na sera ya kuhamisha bahari toka dsm kwenda Moro umpigie makofi na kuamini sera zake, mtu anakuja na sera ambazo kiuhalisia hazitekelezeki na hazijawahi walau kuwahi kuanza kutekelezwa halafu wewe umkubali na kutaka kumpigia kura tusione kua kuna mahali hauko sawa.

Matapeli huwatapeli watu wenye tamaa na wasiofikiri mara mbili.

Wana uhuru wa kuchagua na wengine wana uhuru wa kukosoa machaguzi yao, kushawishi wachague vinginevyo as long as hawavunji sheria.
Sasa ni mtu pekee anayekubali hizo siasa hawezi kubali ukisema hizo hoja hazifai Mkuu. Demokrasia imetupa kuchagua na kwa wakati mwingine wewe unachoona ni ujanja mwingine anaona ni ujinga...

Tuvumiliane unless hakutakuwa na maana ya demokrasia. Wale wanaoamini kwenye Oktaba wanatiki wasiwatukane wanaoamini kwenye NRNE.. ukiona watu wameenda wengi kwenye mkutano wa Octoba wanatiki usiseme watu hao ni wajinga... endelea kuwashawishi. Mwisho wa siku siasa za demokrasia na vyama vingi zinaamuliwa pia na wingi....bahati mbaya sana lakini ndio ukweli
 
Ona hapo wengi ni akina Mama ambao ukiwaangalia Tu sura zao zimekauka na kuchoshwa na Hali mbaya ya uchumi, kijamii lakini Kwa kuwa ndivyo wanavyotaka na kuamini wameumbwa wawe hivyo basi hakuna jinsi.
 
Maccm hamjawahi kuwa na chembe ya aibu. Mmeifungia jamii forums kwa siku 90, halafu kila siku hamuishi kuleta pua zenu humu na kumnadi mgombea wenu anayeshindana na kivuli chake mwenyewe kwenye uchaguzi wa mwaka huu!

Na sijajua ni kwa nini mnaachwa kujivinjari humu jukwaani. CHAWA wote mlitakiwa kupigwa BAN kwa hizo siku zote 90.
 
Sasa ni mtu pekee anayekubali hizo siasa hawezi kubali ukisema hizo hoja hazifai Mkuu. Demokrasia imetupa kuchagua na kwa wakati mwingine wewe unachoona ni ujanja mwingine anaona ni ujinga...

Tuvumiliane unless hakutakuwa na maana ya demokrasia. Wale wanaoamini kwenye Oktaba wanatiki wasiwatukane wanaoamini kwenye NRNE.. ukiona watu wameenda wengi kwenye mkutano wa Octoba wanatiki usiseme watu hao ni wajinga... endelea kuwashawishi. Mwisho wa siku siasa za demokrasia na vyama vingi zinaamuliwa pia na wingi....bahati mbaya sana lakini ndio ukweli
Mkuu kumuita mtu mjinga, mpumbavu, hana akili kwa mtazamo wako sio kosa maana hayo mambo hayana hayathibitishwi kiithibati bali kwa maneno unayotoa na matendo yako.

Yaani mtu kusema wanaoshabikia ccm/act ni wajinga haimaanishi haiheshimu demokrasi, vilevile huyo mwanaccm anaweza kuona/kumuita anaemuita mjinga nae mjinga vilevile.

Ni utofauti wa mitazamo tu wala sio fujo,kejeli au tusi.
 
Back
Top Bottom