Kila nikipost picha yangu lazima nikutane na comment yake 'Cheusi Mangala mwenyewe', inaninyima amani

Kila nikipost picha yangu lazima nikutane na comment yake 'Cheusi Mangala mwenyewe', inaninyima amani

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Habari Wakuu,

Ni muda sana nimekuwa nikipitia hii hali na inaniumiza sana nimeona nishare hapa ili niweze kupata ushauri wenu.

Nina jirani yangu ambaye hatuna mazoea sana ila anafahamu kazi yangu na mimi nafahamu kazi yake pia tumefollow each other kwenye mitandao ya kijamii. Ila kuna jambo moja ambalo huwa analifanya na linanikwaza sana na kuninyima amani, yaani kila nikipost picha yangu Instagram au hata nikiweka status lazima ata-comment "Cheusi Mangala".

Siwezi kukataa rangi yangu kwamba mimi ni mweusi ila sasa ndo mtu uje kila post unacomment neno hilo hilo jamani kweli?

Nimewahi kumwambia kuhusu hiyo tabia lakini bado anaendelea sijui anahisi ni utani wakati mimi inaninyima amani kuna muda nashindwa hata kupost nikiwaza atakuja pale kukoment huo upuuzi.

Sidhani kama ni sawa, inaninyima amani
 
Back
Top Bottom