Kila nikiwaza haya majanga nakosa hamu ya kupata mtoto

Kila nikiwaza haya majanga nakosa hamu ya kupata mtoto

Uwesutanzania

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2019
Posts
1,380
Reaction score
1,686
Natamani sana kuwa na watoto, ila nina mambo yanayonikosesa furaha kila nikiwaza juu ya kuwa na watoto,.
Miongoni mwa mambo hayo nina makubwa mawili nayo ni;-

1. Umasikini, Umasikini ni janga kubwa kwa upande wangu, huwa nakosa amani pale ninapoiona kesho ya watoto wangu kwenye swala umaskini, sina njia mbadala ya kuwa kwamua watoto wangu kwenye hili janga.

2. MARADHI, Hili ni kubwa pia japo halilingani na la kwanza, mfano kwenye hili gonjwa la UKIMWI kila nikiiwaza kesho ya wanangu katika hili janga linanikatisha tamaa na kujiona mwenye hatia endapo ntawaacha watoto waje duniani na niwaingize kwenye hili janga.

3. Upofu, Maradhi ya akili kama uchizi, utahaira nk. Pia kuna maradhi ya moyo. Na hata kifafa. Huwa nakosa furaha kila nikiifikilia kesho ya kizazi changu na naona ni bora niishi mwenyewe na hata nikifa basi nife bila ya kuacha KIZAZI kisicho na furaha.

images.jpeg

Natamani sana kuwa na watoto, ila nina mambo yanayonikosesa furaha kila nikiwaza juu ya kuwa na watoto,.
Miongoni mwa mambo hayo nina makubwa mawili nayo ni;-
Acha uzembe wewe zaa acha visingizio. Hawa wanao zaliwa hawayajui unayo ya waza ww. Na wanao zaa kwenye changamoto unawaona wajinga kama wewe??!! Ila tunasahaugi kuwa hata wajinga nao wanazeeka, mjinga mmoja wapo ni wewe.

Watu wanaukimwi na bado wanazaa watoto wazima hawana ukimwi. Watu maskini wa kutupwa ila waana zaa watoto wanaokuja kuwa potential baadae.

Kumbuka. KUZALIWA MASIKINI SIO KOSA LAKO, ILA KUFA MASIKINI NI KOSA LAKO.
 
Unaingilia mambo ya Mungu ww
mtoaji rizki ni Mungu
Mponyaji ni Mungu

Ww sasa unaogopa nini kma vyote hivo haviko katika uwezo wako?
Sawa ni Mungu ila tatizo mimi ndio source ya hayo yote kutokea, UKIMWI wangu ulitokea kutokana na umalaya wangu na si mungu,. Je, na UKIMWI wa watoto wangu huoni kuwa umetokana na umalaya wangu pia?
 
Acha uzembe wewe zaa acha visingizio. Hawa wanao zaliwa hawayajui unayo ya waza ww. Na wanao zaa kwenye changamoto unawaona wajinga kama wewe??!! Ila tunasahaugi kuwa hata wajinga nao wanazeeka, mjinga mmoja wapo ni wewe. Watu wanaukimwi na bado wanazaa watoto wazima hawana ukimwi. Watu maskini wa kutupwa ila waana zaa watoto wanaokuja kuwa potential baadae.

Kumbuka. KUZALIWA MASIKINI SIO KOSA LAKO, ILA KUFA MASIKINI NI KOSA LAKO.
Sawa, ila tatizo lako wewe umeangalia upande wa mema tu, je ukizaa mtoto TAHAIRA, SHOGA, CHANGUDOA hauoni hayo yote yametokea kupitia ujinga wako wewe?
 
Haujioni mwenye hatia unapowaona watoto wako mashoga, mateja, waathirika, na hata wakifungwa kifungo cha maisha?
Fear can exist is in our thoughts of the future. It is the product of our imagination, causing us to fear things that do not at present and may not ever exist. That is near insanity. Now do not misunderstand me, danger is very real, but fear is a choice.
 
  • Thanks
Reactions: PYD
Haujioni mwenye hatia unapowaona watoto wako mashoga, mateja, waathirika, na hata wakifungwa kifungo cha maisha?
Sas utafanyaje na ndio nature ya dunia yetu inaumiza lkn huna jinsi na huwezi kuishi tu duniani na ukafa bila kuacha uzao
 
ear can exist is in our thoughts of the future. It is the product of our imagination, causing us to fear things that do not at present and may not ever exist. That is near insanity. Now do not misunderstand me, danger is very real, but fear is a choice.
sikio linaweza kuwepo ni katika mawazo yetu ya siku zijazo. Ni zao la fikira zetu, na kutufanya tuogope mambo ambayo hayapo kwa sasa na huenda yasiwepo kamwe. Huo ni karibu wazimu. Sasa usinielewe vibaya, hatari ni kweli, lakini hofu ni chaguo.
NILIVYOISOMA KUTOKA GOOGLE TRANSLATE
 
2. MARADHI, Hili ni kubwa pia japo halilingani na la kwanza, mfano kwenye hili gonjwa la UKIMWI kila nikiiwaza kesho ya wanangu katika hili janga linanikatisha tamaa na kujiona mwenye hatia endapo ntawaacha watoto waje duniani na niwaingize kwenye hili janga.
Inatisha sana hii, nimesikia kwenye uchambuzi wa magazeti leo wanasema ongezeko la kansa kwa watoto ni kubwa
 
Sawa, ila tatizo lako wewe umeangalia upande wa mema tu, je ukizaa mtoto TAHAIRA, SHOGA, CHANGUDOA hauoni hayo yote yametokea kupitia ujinga wako wewe?

Ushoga na uchangudoa wa mtoto wako yatakuwa ni makosa yako katika malezi.

Utaahira, ulemavu wakuzaliwa, au matatizo mengine ambayo ni congenital, siyo makosa yako, na mungu huwa anawapa uwezo mwingne wa kimungu ili wa survive katika changamoto zao. Sasa kinacho kuogopesha kuzaa ni nini jamaa..?
 
sikio linaweza kuwepo ni katika mawazo yetu ya siku zijazo. Ni zao la fikira zetu, na kutufanya tuogope mambo ambayo hayapo kwa sasa na huenda yasiwepo kamwe. Huo ni karibu wazimu. Sasa usinielewe vibaya, hatari ni kweli, lakini hofu ni chaguo.
NILIVYOISOMA KUTOKA GOOGLE TRANSLATE
Nimekosea ni fear not ear

Fear can exist is in our thoughts of the future. It is the product of our imagination, causing us to fear things that do not at present and may not ever exist. That is near insanity. Now do not misunderstand me, danger is very real, but fear is a choice.
 
Inatisha sana hii, nimesikia kwenye uchambuzi wa magazeti leo wanasema ongezeko la kansa kwa watoto ni kubwa

Umeona shida hizo?,. Na tatizo kubwa litatokea pale mtoto wangu atakapozaliwa na UKIMWI wangu ambao niliupata kwa umalaya wangu
 
Nimekosea ni fear not ear

Fear can exist is in our thoughts of the future. It is the product of our imagination, causing us to fear things that do not at present and may not ever exist. That is near insanity. Now do not misunderstand me, danger is very real, but fear is a choice.
Kumbe kiswahili unaweza ee
 
Back
Top Bottom