Kila nikiwaza haya majanga nakosa hamu ya kupata mtoto

Kila nikiwaza haya majanga nakosa hamu ya kupata mtoto

UPUMBAVU.

Mtoto anakuwa vile unavyotaka wewe kutokana na malezi utakayompa.
Sasa kama wewe unazaa tu mradi kuzaa kama paka alafu malezi unayaachia jamii basi tegemea upate bomu.

Ukiona mtu anaogopa mtoto wake kuwa mjinga na mpumbavu basi tambua huyo mzazi ni mjinga aisiyejitambua na mpumbavu vilevile na sio mbeba majukumu yake kama mzazi.
Na hapaswi kuwa mzazi.
Mtu kama huyu nadham aachwe tu.Hakua mnachowez kumshawishi akwaelew
 
UPUMBAVU.

Mtoto anakuwa vile unavyotaka wewe kutokana na malezi utakayompa.
Sasa kama wewe unazaa tu mradi kuzaa kama paka alafu malezi unayaachia jamii basi tegemea upate bomu.
Kipande hiko👆👆 happy juu tupo pamoja,.
Ila hiki Cha hapa chini 👇👇 sijakielewa
Ukiona mtu anaogopa mtoto wake kuwa mjinga, mpumbavu na kuharibika basi tambua huyo mzazi ni mjinga asiyejitambua na mpumbavu vilevile na sio mbeba majukumu yake kama mzazi.
Na hapaswi kuwa mzazi.
 
Unahitaji kusaidiwa sana.
Mi nahitaji kusaidiwa ila sio nishawishiwe upumbavu,.
Kwa mfano, Mimi mwenyewe nimeshindwa kujinasua kwenye swala la umasikini alafu et nije kuweza kumfanya mwanangu aje jinasua kwenye umasikini kweli?
Alafu nahisi hata wanangu watanitoa akili Kama nitawazaa na kuja kunikuta nikiwa kwenye hii Hali,.
Mwisho wa yote,.
NI BORA NI RAUMIWE NA NINYI KULIKO KUJA KUTESEKA NA MATESO YA WANANGU KATIKA HUU ULIMWENGU
 
Thubutu wewee acha uoga babako angekuwa kama ww ungekuwepo? Tumeambiwa nendeni duniani mkaujaze ulimwengu.
 
Huu ni uoga wa maisha...zaa aisee ili uendeleze familia yenu.
 
We ni muathirika?? Kama sio wasiwasi wako unatoka wapi??

Hata hivo kwasasa hata kama mama anao kuna dawa anapewa kumlinda mtoto.
na kwenye suala la umasikini je?, na vipi kwenye elimu bora? au nizae tu watoto hata wakija kuwa machangudoa safi tu
 
Huko ulipo copy hiyo story mwenzio ameandika hayo tayari ana watoto 7 anao.

Sasa wewe endelea kuyashika mawazo yake ya mitandaoni.

Story zingine ni kwa kujiburudisha na sio serious..
 
Huu ni uoga wa maisha...zaa aisee ili uendeleze familia yenu.
Kuna faida gani kuendeleza familia iliyojaa masikini wa kutupwa? Familia ambayo hakuna hata mwanafamilia mmoja mwenye ajira ya kueleweka au biashara ya kueleweka?? Si ndo kuongeza umasikini tu?

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
Poa.... kwa sababu Unaogopa umasikini (majukumu ya malezi) acha sisi tukusaidie kuijaza dunia.
Hapana mi siogopi kulea, naogopa majanga ya kizazi changu,. kama maradhi, ajali, kifo na umasikini,.
najua kuwa sitokuwa na furaha endapo ntakiona kizazi changu kikiwa kinapigwa mpaka kufa kwa sababu ya wizi. sintokuwa na furaha kukiona kizazi changu kinatokwa na udenda kwa matatizo ya akili. sintokuwa nafuraha kukiona kizazi changu ni machangudoa au mashoga au mateja au wapiga debe au wafungwa,.
 
Back
Top Bottom