Kila ninapotaka tutoke pamoja, Mpenzi wangu anakataa kuongozana nami. Nifanyaje?

Kila ninapotaka tutoke pamoja, Mpenzi wangu anakataa kuongozana nami. Nifanyaje?

Nina mpenzi wangu ambaye tumedumu kwenye uhusiano kwa takribani miaka mitatu sasa. Kila siku nimekuwa nikiamini kwamba uhusiano wetu unaenda vizuri, kwani tumepitia mambo mengi pamoja na bado tupo imara kwa namna fulani. Hata hivyo, kuna jambo moja ambalo limekuwa likinichanganya na kunifanya niwe na maswali mengi kichwani mwangu.

Kila ninapopanga au kumwambia tutoke pamoja, iwe ni matembezi ya kawaida au kwenda sehemu za burudani, mara nyingi anakataa kuongozana nami.

Wakati mwingine hutoa sababu tofauti tofauti, lakini sababu hizo hazinipi uhakika wa kutosha na huniacha nikiwa na sintofahamu. Nimekuwa nikijaribu kuelewa lakini bado sijapata jibu la moja kwa moja kuhusu tabia hii. Na sijui nifanyaje?

Natamani kupata ufafanuzi ili nijue hatua sahihi ya kuchukua.
Bila shaka wewe ni mfupi, nguo ukivaa hazikukai vizuri , mropokaji ropokaji mpenzi wako hataki kuaibika mbele za wanawake wenzake.
 
Kwa mtazamo wangu, hali hiyo inaweza kuwa imesahabishwa na mambo yafuatayo:

1. Ikiwa ni mpenzi wako tu, na wala sio mke/mume halali mliyeoana... Huenda atakuwa anaona aibu au anafikiria watu watamuonaje huko nje, yumkini anaogopa kuonekana anaishi na wewe wakati sio mume/mke halali - hata kama majirani wanajua...n.k (I'm speaking this from experience)

2. Hayuko fully committed. Kujitoa kwa kila kitu kwa ajili yako.

3. Kama mpo ndani ya Ndoa rasmi, basi labda hapendi kutembea TU na wewe....mind you, sio kwamba hakupendi, la, ila basi tuu inatokeaga.

4. Atakuwa na sababu zake maalumu. Ambazo haihitaji hasira kuzijua.

Simple tricky, siku 1 mtoe out hata nje ya mkoa ikiwezekana, kaeni mahali, fanyeni mazungumzo ya kiundani sana - muulize (Atafunguka tu).

NB: Yote kwa yote, ili kudumisha Ndoa na Uhusiano wenu ni lazima ukubali kujitoa kwa ajili yake & usipendelee kumtuhumu (suspect) mwenzio kwa kila kitu. Sina maana uwe kipofu.
 
Back
Top Bottom