Kila ninapotaka tutoke pamoja, Mpenzi wangu anakataa kuongozana nami. Nifanyaje?

Bila shaka wewe ni mfupi, nguo ukivaa hazikukai vizuri , mropokaji ropokaji mpenzi wako hataki kuaibika mbele za wanawake wenzake.
 
Kwa mtazamo wangu, hali hiyo inaweza kuwa imesahabishwa na mambo yafuatayo:

1. Ikiwa ni mpenzi wako tu, na wala sio mke/mume halali mliyeoana... Huenda atakuwa anaona aibu au anafikiria watu watamuonaje huko nje, yumkini anaogopa kuonekana anaishi na wewe wakati sio mume/mke halali - hata kama majirani wanajua...n.k (I'm speaking this from experience)

2. Hayuko fully committed. Kujitoa kwa kila kitu kwa ajili yako.

3. Kama mpo ndani ya Ndoa rasmi, basi labda hapendi kutembea TU na wewe....mind you, sio kwamba hakupendi, la, ila basi tuu inatokeaga.

4. Atakuwa na sababu zake maalumu. Ambazo haihitaji hasira kuzijua.

Simple tricky, siku 1 mtoe out hata nje ya mkoa ikiwezekana, kaeni mahali, fanyeni mazungumzo ya kiundani sana - muulize (Atafunguka tu).

NB: Yote kwa yote, ili kudumisha Ndoa na Uhusiano wenu ni lazima ukubali kujitoa kwa ajili yake & usipendelee kumtuhumu (suspect) mwenzio kwa kila kitu. Sina maana uwe kipofu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…