Kila siku tunamnunulia Pombe tumekuja kugundua kumbe anajenga

Ndo maana haya makampani ya pombe siyataki... Mi naenda bar alone nakunywa pombe kwa pesa yangu, mtu anikute bar labda nimnunulie bia mbili tatu lakini sio kwenda wote kununuliana na kuchangishana hela za kulipa bills.

Nisipojenga nijilaumu mwenyewe sio mambo kuhujumiana kwenye pombe... Halafu pombe ni usenge tu sema basi tu
 
Ukiwa positive ni kweli, ila huwezi kuharibu katika jamii inayokuzunguka kwa maslahi yako binafsi haipishani na wale mafisiemu! Mtu ataibia serikali atajenga hotel bado ka invest ila kwa njia isiyo sahihi!
 
Upo sahihi kabisa mkuu,haya mambo ya kua grp sometimes yanaweza kumfanya mtu asifikiri zaidi,anakua anaona maisha ndio haya haya tu,

Hamuwezi kua pamoja maisha yenu yote,ipo siku mtasambaana tu,na kila mmoja wenu atakua na maisha yake,hapo ndipo kila mmoja wenu atakumbuka muda alioupoteza na hela alizopoteza.
 
Kwahio unafikiri hizo ambazo angenunua round hela za bia zenu mbili tatu ndio zinamuwezesha kujenga? Ingekuwa hivyo wasio kunywa pombe wangekuwa na magorofa na wanywaji wangekuwa homeless.
 
Yaani nyinyi ni kweli Kila siku mlikuwa mkienda kumuona mama yake hospital ? 😄
 
Huyo ndio Mwamba sasa , na msipoichukulia positive hio scenario Jamaa atawaacha mbali na mtazidi kuimia.
 
hii imezidi mkuu, rafikiyo kafiwa hasemi? na bado anakusanya michango yenu kitapeli kwenda kumalizia ujenzi
Michango Gani kunua pombe za elfu 1 mia tano Kwa 2000 ni michango ya kujenga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…