Kila unalotakiwa kujua kuhusu IPTV (kuangalia TV kwa kutumia internet)

Kila unalotakiwa kujua kuhusu IPTV (kuangalia TV kwa kutumia internet)

Tumezoea katika maisha yetu tukiangalia Tv basi huduma ile tunaipata kupitia madishi, cable au antenna. siku zinavyosogea mbele na technology ndivyo inavyokuwa na ndio jinsi madish na antenna vinavyopitwa wakati. leo kwenye uzi huu tutaangalia IPTV.

Ni nini hii IPTV?
IPTV ni kifupi cha Internet Protocal TeleVision. Hii ni aina ya uangaliaji TV kupitia mtandao wa internet ambapo kituo cha TV badala ya kutumia satelite dish au cable wenyewe wanarusha matangazo kwa internet.

Unawezaje kuangalia IPTV?
Utahitaji kifaa chenye internet na uwezo wa kustream ili kuweza kuangalia kama vile smartphone, tablet, laptop, desktop hadi TV zenye internet zinaweza kustream.

Internet yenye speed gani inahitajika?
Internet yoyote hata ya edge inaweza kustream ila iwe na latency nzuri, zipo stream zinahitaji speed ya 200kbps tu (25KBps). Kama una latency ndogo hata internet iwe na speed vipi huwezi kustream live utastream tu vitu ambavyo si live. Kujua zaidi kuhusu latency nenda thread hii
https://www.jamiiforums.com/tech-ga...iwa-na-download-speed-kubwa-ndio-mzuri-2.html

Je software gani inatumika kustream hizo TV?
Kikawaida browser yenye flash au html5 inaweza kustream tv lakini ukitaka kustream vizuri zaidi software kama VLC au KODI ni muhimu. Kutokana na uhaba wa links za VLC nitazungumzia zaidi jinsi ya kutumuia KODI kuangalizia IPTV.

KODI ni nini?
KODI ni software (media centre) ambayo hutumika kuubadili muonekano wako wa simu uwe kama TV na kuweza kuenjoy TV unazotumia na inapatikana kwenye simu, tablet, computer hadi TV.
Kodi-devices-smudged.jpg

Kuidownload nenda website yao hii hapa chini, ni bure haiuzwi
Downloads | Kodi

Nikishadownload kodi nini kinafuatia?
Utahitaji ku install plugin ili uweze kuangalia TV online. Click video add on halafu chagua watchmojo, install halafu ifungue tuone kama itafanya kazi.
9vW4MHp.jpg

KODI imefanya kazi, je siwezi angalia mpira na vipindi vyengine?
Unaweza angalia mpira chanel unayotaka kuanzia za ki-Africa kama Super sport, za Ulaya kama Sky sport, za Asia kama Bein sport hadi za kimarekani kama NBC cha muhimu uwe na plugin (add ons) husika, hizi plugin za mpira na michezo mengine zinapatikana tu internet mfano mimi plugin yangu ninayotumia inaitwa Vdtube25 ina channel nyingi sana kuanzia mpira hadi movie.
zNbDtYR.jpg

PppArCw.jpg

Hio hapo juu sky sport 3

Uzuri wa hizi plugin za kodi zipo TV ni HD na nyengine ni full HD kabisa hivyo internet yako tu.

Malipo?
Kila kitu kuanzia juu hadi hapa ulipofikia ni bure hutoi pesa, ila hizi plugin za bure haziaminiki zipo za kulipia ambazo hazikati ovyo. Mimi sijawahi kulipa natumia tu bure ila kama unahitaji service nzuri zaidi unaweza kulipa ila pia kuwa makini na matapeli

Tutorial ya kuweka na mahala pa kupatia plugins
Plugin yangu ninayotumia ya vdtube25
https://seo-michael.co.uk/how-to-install-vdubt25-add-on-kodi-xbmc

Website hio hio pia utapata plugins nyingi.

Kama una swali lolote usisite kuuliza chini
mkuu CHIEF MKWAWA hizo extensions zinakubali kwenye Chrome Os? maana yake mie pc yangu inarun hiyo OS na vitu vingi sana vya Windows huku havikubali.
 
Last edited by a moderator:
Chief-Mkwawa hiyo Kodi iko available as an app on appstore for apple users?
Najaribu kuichungulia kwa iphone siioni
 
Last edited by a moderator:
mkuu CHIEF MKWAWA hizo extensions zinakubali kwenye Chrome Os? maana yake mie pc yangu inarun hiyo OS na vitu vingi sana vya Windows huku havikubali.

kuna project inaitwa arc welder ipo kwenye beta stage ila nakushauri icheki mi naitumia kwenye chrome (pc) ila imetengenezwa kwa ajili ya chrome os. project hii inaconvert app za android kuwa extension za google chrome.
download arc welder hapa
https://chrome.google.com/webstore/detail/arc-welder/emfinbmielocnlhgmfkkmkngdoccbadn

ukishadownload itataka uipe folder la kusave vitu. download application yoyote ya android halafu fungua arc welder ieke hio app then convert itaenda kama zip file.

extract hilo zip halafu rudi chrome then tick developer mode iwe on halafu load unpacked extension then chagua ile app ya android ulioconvert. hapo utaweza kurun app ya android kwenye chrome (pengine hata hii kodi ikakubali)

ila bado hii project ni beta usitegemee vikubwa sana.
google-chrome-run-android-apps-with-arc-welder.png
 
Last edited by a moderator:
Chief Mkwawa, je IPTv kwenye kisimbusi cha QSAT 15G naweza pata hii huduma? Na inapatikanaje kwa qsat 15 g
 
Chief Mkwawa, je IPTv kwenye kisimbusi cha QSAT 15G naweza pata hii huduma? Na inapatikanaje kwa qsat 15 g

kuna sehemu ya kueka url? inakubali playlist za m3u? angalia mwenyewe then tumia link aliyonipa Watu8 hapo juu nilitest tv moja ilikubali.
 
Last edited by a moderator:
Bila shaka wewe umedownload remote app za kodi/xbmc ndio maana umeandika haya...

Kama sijakosea Google playstore hawana app ya kodi so far, ukitaka kudownload app yao inakupasa uende mtandao wa kodi, Chief-Mkwawa kauweka pale juu

Hyo kodi ndo remote mkuu... Maana nimedownload halafu sijui cha kufanya
 
Last edited by a moderator:
Kuna baadhi ya satelite receiver ni xbmc compatible...

Kama hiyo receiver uko nayo inaweza kuwa loaded na kodi/xbmc then unaweza kustream tokea links za IPTV na hata kuweka addons...

Chief Mkwawa, je IPTv kwenye kisimbusi cha QSAT 15G naweza pata hii huduma? Na inapatikanaje kwa qsat 15 g
 
Bila shaka wewe umedownload remote app za kodi/xbmc ndio maana umeandika haya...

Kama sijakosea Google playstore hawana app ya kodi so far, ukitaka kudownload app yao inakupasa uende mtandao wa kodi, Chief-Mkwawa kauweka pale juu

natumia ios
 
Kuna baadhi ya satelite receiver ni xbmc compatible...

Kama hiyo receiver uko nayo inaweza kuwa loaded na kodi/xbmc then unaweza kustream tokea links za IPTV na hata kuweka addons...

Mkuu hii kitu unakuwa na decorder u naweka kadi ya simu kupata hiyo iptv?
 
Mkuu hii kitu unakuwa na decorder u naweka kadi ya simu kupata hiyo iptv?

Mkuu IPTV ni upitishaji tu wa video, voice na multimedia contents nyinginezo via an internet...

Kuna decoders/visimbusi ambavyo huwa na uwezo wa kupokea internet, yaani sina interface ambayo hupokea internet mathalani RJ45, wireless card(wifi built in), SIM card slot (unapachika line ya 2G, 3G etc), Optical interface etc...

Visimbusi hivi vyenye uwezo huo wa kupokea internet huwekwa ndani yake software platform yenye kuweza kupokea mawimbi wa TV, Radio etc kwa mtindo wa kustream...

Hivyo mkuu huna haja ya kadi bali huwa kuna subscription ambayo mtu hufanya na hulipia kwa hao providers wa IPTV contents...

Ila sasa hii KODI aliyoelezea Chief Mkwawa yenyewe ni bure kabisa wala huna haja ya kununua maadamu uwe na kompyuta yenye Windows, Linux au iOS..Pia ukiwa na android box yoyote pia inafaa...

Utainstall kwa kompyuta yako kama software nyingine tu na utaifanyia baadhi ya configurations ili uweze kupata matangazo ya TV, radio, weather etc...
 
Asante mkuu, Kuna mtaalamu anayeweza kuniunganishia nikasema kuona kupitia tv? Ghar am a zipoje?

Swali tofauti,

Je bein sport dekoda zinashika dar?

Je dstv dekoda ukinunua S. AFRICA inafanya kazi dar? Unalipiaje kifurushi?

Thanks bro.
 
Asante mkuu, Kuna mtaalamu anayeweza kuniunganishia nikasema kuona kupitia tv? Ghar am a zipoje?

Mkuu kinachojadiliwa hapa ni namna ya kutazama TV za nje bure maadamu tu uwe na internet pamoja na kompyuta...

Swali tofauti,

Je bein sport dekoda zinashika dar?

Mkuu kuna watu huwa naona wanajadili hapa kuwa unaweza kuwa na decoder ya Bein kwa hapo Dar...

Sina uhakika sana wanazipata wapi...

Binafsi kwa kupitia hii Kodi huwa natazama channels zote za Bein, gharama pekee niingiayo ni kununua internet tu...

Je dstv dekoda ukinunua S. AFRICA inafanya kazi dar? Unalipiaje kifurushi?

Thanks bro.

Hata hili nimelisikia hapa JF kuwa unaweza nunua decoder ya DSTV huko SA na ukaisajili huko huko...

Then ukienda nayo Dar unakuwa unailipia online na unapata channels zote kama upo SA vile...

Na malipo huwa kwa gharama ile inayoonekana kwa watu wa SA.
 
Mkuu kinachojadiliwa hapa ni namna ya kutazama TV za nje bure maadamu tu uwe na internet pamoja na kompyuta...

Mkuu kuna watu huwa naona wanajadili hapa kuwa unaweza kuwa na decoder ya Bein kwa hapo Dar...

Sina uhakika sana wanazipata wapi...

Binafsi kwa kupitia hii Kodi huwa natazama channels zote za Bein, gharama pekee niingiayo ni kununua internet tu...

Hata hili nimelisikia hapa JF kuwa unaweza nunua decoder ya DSTV huko SA na ukaisajili huko huko...

Then ukienda nayo Dar unakuwa unailipia online na unapata channels zote kama upo SA vile...

Na malipo huwa kwa gharama ile inayoonekana kwa watu wa SA.

Asante mdau,

Je, Iptv receiver zinapatikana wapi dar?
 
Asante mdau,

Je, Iptv receiver zinapatikana wapi dar?

Sidhani kama kuna muuzaji yoyote mwenye kuuza hii mambo kwa sasa mkuu...

Isipokuwa hapa ndani kuna watu wauzao satellite receiver (DVB-S) zilizo na feature ya IPTV ndani yake...
Mwl.RCT au Njunwa Wamavoko hawa huwa naona wanadeal na satellite receivers humu ndani...

Otherwise ukitaka kisimbusi ambacho ni pure internet based, itakubidi uagize online kupitia Amazon or eBay...

Huko utapata kila aina ya android box zenye kubeba hii KODI kwa bei chini ya 100$...
 
Last edited by a moderator:
Asante mdau,

Je, Iptv receiver zinapatikana wapi dar?

IPTV receiver zipo ila haziwezi meet demands zako labda ununue receiver kama Qsat uziwekee premium account ya DQIPTV
Naweza sema uchukue ushauri wa mdau hapo juu uchukue android tv box online maana unaweza customize utakavyo wewe kwa kutumia Kodi/XBMC
 
Back
Top Bottom