Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Wajanja wa nchi hii wametuletea kilevi hatari kwa taifa letu, kiasi kimekolezwa na kesi za akina Magoma zinazoipotezea muda mahakama zetu.
Wakati bodi ya vilevi hairuhusu baa kuuza pombe saa za kazi lakini bodi hii TCRA inaruhusu walevi wake wanshinde kutwa nzima eti wasikilize uchambuzi na kesi za mpira wa Simba na Yanga ambako kuna wapiga kura pendwa wengi, kunogesha kilevi hiki kimeongezewa na mamilioni ya ya shilingi za goli! Leo hii uswahilini watu wamekuwa mateja wa Simba na Yanga, panapouzwa magazeti ni ubishi wa kilevi hiki kipya.
Tanzania viongozi wetu hufurahia umasikini na ujinga wetu kwani ndio unaowapa kura ili washike madaraka kupitia kutudanganya na visima vya maji yasiyo salama karne hii! Kwa pombe hii Tanzania itabaki kuwa mtazamaji huku wenzetu wanachanja mbuga, lete pombe nyingine.