Kilevi hiki ni hatari kwa taifa japo kina faida kwa wanasiasa

Kilevi hiki ni hatari kwa taifa japo kina faida kwa wanasiasa

Wajanja wa nchi hii wametuletea kilevi hatari kwa taifa letu, kiasi kimekolezwa na kesi za akina Magoma zinazoipotezea muda mahakama zetu.

Wakati bodi ya vilevi hairuhusu baa kuuza pombe saa za kazi lakini bodi hii TCRA inaruhusu walevi wake wanshinde kutwa nzima eti wasikilize uchambuzi na kesi za mpira wa Simba na Yanga ambako kuna wapiga kura pendwa wengi, kunogesha kilevi hiki kimeongezewa na mamilioni ya ya shilingi za goli! Leo hii uswahilini watu wamekuwa mateja wa Simba na Yanga, panapouzwa magazeti ni ubishi wa kilevi hiki kipya.

Tanzania viongozi wetu hufurahia umasikini na ujinga wetu kwani ndio unaowapa kura ili washike madaraka kupitia kutudanganya na visima vya maji yasiyo salama karne hii! Kwa pombe hii Tanzania itabaki kuwa mtazamaji huku wenzetu wanachanja mbuga, lete pombe nyingine.
Weee unashaur nn sasa maana maelezo meng haina hata maana kumbuka wanasiasa pia wao wapo kaz kama ww unafofanya kaz yako kila sku wanakuwa wabunfu ili waendele kula na kuish
 
Weee unashaur nn sasa maana maelezo meng haina hata maana kumbuka wanasiasa pia wao wapo kaz kama ww unafofanya kaz yako kila sku wanakuwa wabunfu ili waendele kula na kuish
Andika vizuri, kiswahili chako cha mateja mimi kimenishinda kukielewa.
 
Sawa haina shida na ndiyo maana ya demokrasia na uhuru wa maoni. Ila kumbuka pengine ungekuwa Gen Z wa Kenya ungekuwa ndiyo mmoja wa wale zaidi ya 70 waliokufa
Nikufahamishe tu, nyuma ya kila Uhuru wa nchi kuna watu waliuawa, vimbwakoko vinavyofyata mkia ni vya kuviua kwani vinakula tu havina faida kwa jamii.
 
Zama zimebadilika.
Miaka ya nyuma asubuhi ilikuwa uchambuzi wa siasa, usiku saa mbili kasoro michezo, dakika 15-30, sasa hivi asubuhi, mchana,jioni, usiku ni michezo.

Generation ya wachambuzi wa siasa ime-phase out, imeondoka na akina Jenerali Twaha.

I bet kwa sasa wachambuzi bora wa michezo ndio wanaolipwa vizuri kuliko wa siasa
 
huu mjadala wa simba na utopolo hauwezi kuisha.
Mpaka uishe mjadala wa makafiri na wapalestina.
 
Wajanja wa nchi hii wametuletea kilevi hatari kwa taifa letu, kiasi kimekolezwa na kesi za akina Magoma zinazoipotezea muda mahakama zetu.

Wakati bodi ya vilevi hairuhusu baa kuuza pombe saa za kazi lakini bodi hii TCRA inaruhusu walevi wake wanshinde kutwa nzima eti wasikilize uchambuzi na kesi za mpira wa Simba na Yanga ambako kuna wapiga kura pendwa wengi, kunogesha kilevi hiki kimeongezewa na mamilioni ya ya shilingi za goli! Leo hii uswahilini watu wamekuwa mateja wa Simba na Yanga, panapouzwa magazeti ni ubishi wa kilevi hiki kipya.

Tanzania viongozi wetu hufurahia umasikini na ujinga wetu kwani ndio unaowapa kura ili washike madaraka kupitia kutudanganya na visima vya maji yasiyo salama karne hii! Kwa pombe hii Tanzania itabaki kuwa mtazamaji huku wenzetu wanachanja mbuga, lete pombe nyingine.
wakati mataifa yaliyoendelea wanafikiri namna ya kuboresha viwanda na kufanya maendeleo ya kisayansi sisi viongozi wanawaza kukopa chanjo za covid ambazo imethibitika hazikuwa na msaada wowote na pesa za uvico wakajengea madarasa na vyoo. Na mzigo wa kulipa hayo madeni ni juu ya wananchi. Hapo unaona kuna viongozi wa kutuletea madndeleo kweli? kama tunakopa kujenga madarasa na vyoo?m
 
Wao na familia zao wameendelea, wanachowazia kila baada ya uchaguzi ni kura za urais.
 
Nilikua na page ya siasa Instagram niliishia kupata like 3 ndani ya miezi minne...Saizi nimeibadilisha,naposti michezo(hasa Simba na Yanga),napata followers wa kumwaga hadi nashangaa,...kweli nchi hii Simba na Yanga ni ulevi mkubwa
 
Na hata vipindi vya redion kuanzia asubuhi ni wanachambua mpira tu
 
April 11, 2020

Siasa ndani ya mpira​

img-20200412-wa00101408724181.jpg

Football politics

SIASA, DIPLOMASIA NDANI YA MPIRA

Utata wa Ushangaliaji wa Mchezaji wa Uswisi.
img-20200412-wa0013667808872.jpg
Granit xhaka na xhedan shakir wakishangilia kwa ishara ya double head eagle

🔰Mpira wa miguu pengine ndio mchezo wenye ushabiki mkubwa zaidi kuzidi mchezo wowote ule duniani. Ushabiki huu ambao mpira wa miguu umejipatia umeufanya kuwa na ushawishi mkubwa sana katika nyanja mbalimbali za maisha kimataifa. Kwa sasa mpira si mchezo tu kwa ajili ya burudani bali mpira wa miguu umekuwa ni jukwaa la kusukuma maswala ya kisiasa, diplomasia, kujenga ushawishi wa kimataifa na hata kujikweza kwa ufanisi na umahiri.

🔰Watu wengi mtaani tunaangalia mpira kushabikia timu tuzipendazo na kujiliwaza kwa burudani, lakini ukiutazama kwa jicho la tofauti mchezo wa mpira umegubikwa na mambo ya kisiasa na diplomasia ambayo pengine watu wengi hawayaoni.
🔰Hivi karibuni nchini Russia kulifanyika tukio kubwa zaidi la kimichezo, Mashindano ya Kombe la Dunia likihusisha timu za taifa za nchi zipatazo 32 zilizo chini ya Uongozi wa Vyama vitano vya soka vya mabara (Confederations). Inakadiriwa takribani watu bilioni 3.7 ulimwenguni kote walifuatilia kwa karibu kabisa mashindano haya kupitia matangazo ya televisheni.
🔰Katika nyanja ya diplomasia na siasa hili lilikuwa ni jukwaa maridhawa kabisa kusukuma masuala hayo.
🔰Kuna siku moja kulikuwa na mtanange wa kukata na shoka kati ya timu ya taiafa ya Uswisi dhidi ya timu ya taifa ya Serbia. Mchezo huo wa kusisimua uliisha kwa timu ya taifa ya Uswisi kujipatia ushindi wa goli mbili dhidi ya goli moja la Serbia.
🔰Licha ya uhondo wa burudani ambao tuliushuhudia kwenye mchezo ule, lakini hicho hakikuwa hasa kisanga kikuu cha mtanange ule, kisanga kikubwa zaidi cha mchezo ule kilikuwa ni namna ya ushangiliaji ya wachezaji wa Uswisi walipofunga magoli.
🔰Jambo la kwanza kabisa la kusisimua kuhusu mpambano huu wa Serbia na Uswisi ni kwamba ulikuwa unahusisha nchi mbili ambazo haziivi vizuri sana kidiplomasia. Kwa muda wa karibia miongo mitatu sasa nchi ya Uswisi imepokea kiwango cha zaidi ya wahamiaji nusu milioni kutoka kwenye nchi ambazo zina asili kutoka kwa iliyokuwa Muungano wa Yugoslavia (yaani nchi kama Serbia, Montenegro, Croatia, Slovenia, Bosnia n.k). wimbi hili kubwa limetokea kati ya miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili kutokana na vita mfululizo ambavyo vilikuwa vinaendelea kwenye nchi hizo hasa hasa mwishoni mwa miaka ya tisini.
Katika idadi hiyo ambayo nimeitaja hapo juu yaani wahamiaji nusu milioni wa asili ya Yugoslav, karibia wahamiaji laki tatu kati yake ni aina ya watu ambao wanaitwa ‘Kosovars’. Kosavars ni watu wa asili ya Albania ambao wanaishi nchini Kosovo.
Sasa basi, zaidi ya nusu ya wachezaji wa timu ya taifa ya Uswisi ni Waalbania ambao wana asili ya Kosovo (Kosovars).
🔰Kosovo kwa miaka mingi lilikuwa ni jimbo lenye mamlaka (autonomous) lakini ikiwa kama sehemu ya nchi ya Serbia. Kwa miongo mingi sana kulikuwa na mtafaruku wa Kosovo kutaka kujitawala yenyewe vuguvugu ambalo limezua vita mara kadhaa katika historia. Mwaka 2008 Kosovo ilijitangazia uhuru kutoka nchi ya Serbia kitendo ambacho kilipingwa vikali sana na serikali ya Serbia na mpaka leo hii japo Umoja wa Mataifa inatambua Kosovo kama nchi huru lakini bado Serbia imekataa kutambua uhuru huo wa Kosovo na bado wanahesabu kama ni jimbo la nchi yao. Hii ndio sababu ya watu wote wenye asili ya Kosovo hasa hasa Kosavars duniani kote kuhamasisha na kujaribu kuamsha ulimwengu uweze kuweka shinikizo kwa Serbia kuitambua Kosovo kama nchi huru.Kwa hiyo mchezo wa siku hiyo kati ya Uswisi na Serbia kwa maneno mengine tunaweza kusema ilikuwa ni mechi kati ya ‘wakoloni’ (Serbia) dhidi ya ‘watawaliwa’ (timu ya Uswisi ina wachezaji wengi ambao wazazi wao wana asili ya Kosovo, yaani Kosovars).
🔰Ndipo maana Granit Xhaka mwenye asili ya ualbania wa Kosovo alipofunga goli dakika ya 52 alishangilia kwa kuweka mikono yake mtindo wa alama inayotumika sana Kosovo ijulikanao kama ‘Double Eagle’ (Tazama picha). Vivyo hivyo dakika ya 90 Xherdan Shaqiri naye mwenye asili ya Albania wa Kosovo alipoongeza goli la pili naye alishangilia kwa mtindo huo huo.

🔰Alama hii inaakisi ndege aina ya tai mwenye vichwa viwili ambaye amechorwa kwenye bendera ya nchi ya Albania. Wananchi wa Kosovo (ambao zaidi ya 85% ni Waalbania) wanatumia bendera ya Albania na alama ya tai mwenye vichwa viwili kama ishara ya kuwakera Waserbia kumaanisha kuunga mkono uhuru wa Kosovo.
🔰Japokuwa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limepiga marufuku wachezaji kutoa ishara zozote za kisiasa wakiwa uwanjani na kuvunja agizo hilo kunaweza kupelekea mchezaji kufungiwa kucheza mpira, lakini FIFA inaonekana kama iliwasamehe Xhaka na mwenzake Xherdan na kuwatoza faini ya faranga za Uswisi elfu kumi kila mmoja. Japokuwa kiwango hiki ni kidogo mno kulinganisha na mishahara wanayolipwa wachezaji hawa wote wawili kwa kucheza mpira wa kulipwa ligi kuu ya Uingereza lakini Wakosovars duniani kote walianzisha kampeni ya kuchangishana fedha hiyo faranga elfu kumi ili kuwalipia wachezaji hao faini hiyo ili kuonesha kuwaunga mkono kwa kitendo kile walichokifanya kutetea ndugu zao wa Kosovo mbele ya macho ya mabilioni ya watu wanaoangalia kombe la dunia ulimwenguni kote. Wakosovar duniani kote kutokana na tukio hili lililofanywa na Xhaka na mwenzake Xherdan wameenda mbali zaidi na waliweka nia kwamba fedha hiyo itakayochangwa kama itakuwa nyingi mno na kuzidi faranga elfu kumi basi itagawiwa kwa asasi za kiraia ambazo zinafanya kazi kutetea kutambulika kwa uhuru wa Kosovo.
Kuna siasa nyingi sana na mambo mengi sana ya kujifunza yanayoendelea kwenye mchezo wa mpira wa miguu nyuma ya pazia.
 
huu mjadala wa simba na utopolo hauwezi kuisha.
Mpaka uishe mjadala wa makafiri na wapalestina.
Kwa taarifa yako Israeli na Palestina hakuna makafir, vinginevyo ungesikia vita vya kidini. Israeli na Palestina ndio wanaozijua vizuri dini sisi na waarabu tumedandia tu.
 
Wajanja wa nchi hii wametuletea kilevi hatari kwa taifa letu, kiasi kimekolezwa na kesi za akina Magoma zinazoipotezea muda mahakama zetu.

Wakati bodi ya vilevi hairuhusu baa kuuza pombe saa za kazi lakini bodi hii TCRA inaruhusu walevi wake wanshinde kutwa nzima eti wasikilize uchambuzi na kesi za mpira wa Simba na Yanga ambako kuna wapiga kura pendwa wengi, kunogesha kilevi hiki kimeongezewa na mamilioni ya ya shilingi za goli! Leo hii uswahilini watu wamekuwa mateja wa Simba na Yanga, panapouzwa magazeti ni ubishi wa kilevi hiki kipya.

Tanzania viongozi wetu hufurahia umasikini na ujinga wetu kwani ndio unaowapa kura ili washike madaraka kupitia kutudanganya na visima vya maji yasiyo salama karne hii! Kwa pombe hii Tanzania itabaki kuwa mtazamaji huku wenzetu wanachanja mbuga, lete pombe nyingine.
Toa mbadala ni upi???

Unataka wafanyeje??
 
Back
Top Bottom