Kwani mtoto anapolia anapata nini? Ila kilio cha mtoto humtikisa mama yake, na mtoto akinyamaza kabisa kutwa nzima mama huingiwa na wasiwasi na kuanza kumchunguza mwanae, umehoji hao GenZ wa Kenya wamepata nini wakati huohuo umeeleza Ruto alichokifanya, hicho alichokifanya kimetokana na walivyoandamana, tunawajibika kuzikubali jitihada zao kwani bajeti ijayo serikali itakuwa makini zaidi, tofauti na sisi tunaanzisha sherehe ya kitaifa Kizimkazi bila bunge kuitengea bajeti, hii inamaana bajeti yetu haina uhalisia.