Kabla Magufuli hajakabidhiwa Uenyekiti wa CCM Taifa , chama hiki kilikuwa mali ya wanachama wake , walijianzishia miradi yao kwenye matawi , walijipatia chochote kwa kulinda magari yaliyolazwa kwenye ofisi hizo , wengine walianzisha miradi ya kupangisha wafanyabiashara kwenye baadhi ya maeneo ya ofisi zao , kidogo walibugia lakini pia kiasi fulani walipeleka kwenye akaunti za chama chao kwenye ngazi za wilaya na mikoa , ulikuwa ni utaratibu wa " Pata nipate " mara kadhaa ulikuta wazee wa ccm wakicheza bao kwenye ofisi zao , huku wakisubiri posho za hapa na pale kutoka kwa watia nia mbalimbali .
Utaratibu huu ndio uliokiimarisha chama chao , hapa ndipo kulitengenezwa timu za kampeni za wagombea mbali mbali , zikiwemo pia timu za wanunua shahada za wanachi mitaani ili kutengeneza graph ya ushindi , hawa wafia chama ambao pia kwa kiasi fulani walikuwa wachumia tumbo ndio ilikuwa nguzo kuu ya ushindi ya ccm , walijitolea usiku na mchana kukipigania chama chao hata kwa njia za haramu kama uchawi na rushwa za chumvi na michele , hawa hawakustahili kutimuliwa kwenye maskani zao , hawakustahili kunyang'anywa mapato hata ya kulaza magari kwenye ofisi za chama chao , huko ni kuuwa chama .
Kuingia kwa Kamati ya kuhakiki mali za chama na kunyang'anya miradi yote ya chama ikiwemo hata miradi duni ya kulaza magari na kuipeleka ofisi ndogo Lumumba kumekifanya chama kupoteza wafia chama , kimeua morali wa kujitolea kwa wapambanaji wake , hii ndio sababu kubwa ya ccm kupoteza watu na kuogopa uchaguzi nchi nzima , baada ya utafiti wao wamelijua hili na ndio sababu ya Watendaji kukimbia kupokea fomu za wagombea wa upinzani ili kuogopa kushindwa , wameua chama chao kizembe baada ya kukosa ubunifu wa kukusanya mali za chama chao bila kuumiza wanachama wake waziwazi , sasa hivi kwenye matawi ya ccm hata mtu akitaka kununua kalamu ya mia 2 ni lazima afunge safari kwenda ofisi ya Wilaya ili kuomba hela , ni nani atahangaika na jambo hilo ?
Asante Mungu kwa kusikia kilio cha Watanzania .