Kilichomfukuzisha kazi Maulidi Kitenge Wasafi FM chajulikana

Wadau, kichwa cha habari chajieleza. Mtangazaji Maulidi Kitenge hajaondoka Wasafi FM Radio bali amefurushwa kwa sababu ya safari zake za mara kwa mara nje ya nchi, hususan nchini Marekani.

Kwa mujibu wa chanzo cha ndani kutoka Wasafi FM, Maulidi Kitenge amekuwa akienda nchini Marekani kwa mwaka mara nne jambo ambalo limekuwa likimkera CEO wa Wasafi, Nasibu Abdul 'Diamond'.

"Mfano, Novemba mwaka jana alikwenda Marekani. Januari mwaka huu, wakati Rais Joe Biden anaapishwa akaenda. Machi akaenda tena, mwezi Julai pia akaenda, mpaka unaingia Agosti yuko kule. Diamond akaona jamaa anakuwa nje ya kituo cha kazi muda mwingi, akaamua kumtimua," kilisema chanzo hicho.

"Amekuwa akitumia nguvu kubwa kutuma matangazo yake Wasafi akiwa kule, kama kusoma Magazeti (Kurasa za Magazeti, Chumvi na Ndimu) na Michezo (Sports Arena) ili aoneshe kuwa, hakuna pengo la kazi zake, lakini ukweli ni kwamba, Diamond amekuwa akikereka sana, akashindwa kumvulimia, akamtumia barua ya kumwachisha kazi," kiliongeza chanzo hicho.
Nimetoka kuliongea Hilo KABLA sijasoma uzi wako, niliwaambia anatumia muda mwingi nje, ni vizuri alivyoondoka ili apate muda wa kusafiri huyu Jana akili yake anaijua mwenyewe
 
Hilo la kusafiri lipo ndani ya mkataba
Majizo kavunja tu benki ili kuvunja mkataba
Bakhresa alipotaka kuimarisha Ufm alivunja benki na kumnunua Mussa Kawambwa toka wasafi ambae sidhani kama alishamaliza mwaka toka ajiunge na wasafi kutoka Azam Tv
Huu ni wakati wa biashara huria,vijana wanapiga pesa kwa kutumia makoo yao,wewe kama umeajiriwa Radio Tanzania,kaa hapo hapo kwa miaka 30,halafu uzawadiwe baiskeli na cheti
Muda kawambwa alitoka Ufm alipoondoka bila shaka kulikuwa na pengo, Kitenge aliondoka EFM kukawa na pengo pia Ndio maana Majizo amemrudisha.
Ila pengo la Kitenge wasafi huenda lisiwepo, mambo yatakaa sawa tu
 
Laki 6/=? Mbona waandishi wa habari wanachuliwa cheap hivyo Tanzania? Huyu ni mwandishi/mtangazaji mwenye uzoefu wa kutosha. Vipi sasa wale wanaoanza? Kama kweli alikuwa analipwa laki 6 na akawa na pesa ya kusafiri hivyo basi achunguzwe. Hizo tiketi za ndege anatoa wapi?
Mkataba wa kitenge alikuwa analipwa 600k per month hivo Kuna vipengele vikawa vinampa Uhuru wa kwenda safari zake ili arikave kwahiyo suala la kuondoka ni kwa mutual understanding baina ya wasafi na kitenge maana mkataba imeisha katika kutaka waingie mkataba mpya wasafi wakataka kumlimit safari za nje kwa madai hata boss wake hasafiri Mara kwa Mara na wakaahidi kumlipa 650k per month kutoka 600k per month
 
Wadau, kichwa cha habari chajieleza. Mtangazaji Maulidi Kitenge hajaondoka Wasafi FM Radio bali amefurushwa kwa sababu ya safari zake za mara kwa mara nje ya nchi, hususan nchini Marekani.

Kwa mujibu wa chanzo cha ndani kutoka Wasafi FM, Maulidi Kitenge amekuwa akienda nchini Marekani kwa mwaka mara nne jambo ambalo limekuwa likimkera CEO wa Wasafi, Nasibu Abdul 'Diamond'.

"Mfano, Novemba mwaka jana alikwenda Marekani. Januari mwaka huu, wakati Rais Joe Biden anaapishwa akaenda. Machi akaenda tena, mwezi Julai pia akaenda, mpaka unaingia Agosti yuko kule. Diamond akaona jamaa anakuwa nje ya kituo cha kazi muda mwingi, akaamua kumtimua," kilisema chanzo hicho.

"Amekuwa akitumia nguvu kubwa kutuma matangazo yake Wasafi akiwa kule, kama kusoma Magazeti (Kurasa za Magazeti, Chumvi na Ndimu) na Michezo (Sports Arena) ili aoneshe kuwa, hakuna pengo la kazi zake, lakini ukweli ni kwamba, Diamond amekuwa akikereka sana, akashindwa kumvulimia, akamtumia barua ya kumwachisha kazi," kiliongeza chanzo hicho.
Niliposoma Uzi wako nilipofika hapo katika CEO wa wasafi Diamond nikasheka kidogo sijui kwa nini nimecheka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkataba wa kitenge alikuwa analipwa 600k per month hivo Kuna vipengele vikawa vinampa Uhuru wa kwenda safari zake ili arikave kwahiyo suala la kuondoka ni kwa mutual understanding baina ya wasafi na kitenge maana mkataba imeisha katika kutaka waingie mkataba mpya wasafi wakataka kumlimit safari za nje kwa madai hata boss wake hasafiri Mara kwa Mara na wakaahidi kumlipa 650k per month kutoka 600k per month
600k kwa kazi yote ile? Hapana
 
Laki 6/=? Mbona waandishi wa habari wanachuliwa cheap hivyo Tanzania? Huyu ni mwandishi/mtangazaji mwenye uzoefu wa kutosha. Vipi sasa wale wanaoanza? Kama kweli alikuwa analipwa laki 6 na akawa na pesa ya kusafiri hivyo basi achunguzwe. Hizo tiketi za ndege anatoa wapi?
Bro/ninaamini wewe ni mwanaume.
Je nchi hii tungetegemea mishahara kuna wangapi wangejenga, au hata kusomesha watoto?
Mtaji wa laki 6 sio tatizo, je tunajua vyanzo vyake vingine vya mapato?
Mtangazaji huwa na kipindi kimoja kwa siku kisichozidi saa moja, umewahi kujiuliza muda uliosalia wanautumia wapi?

Bila shaka huyu ana vyanzo vingine halali vya kimapato zaidi ya utangazaji.
 
Back
Top Bottom