Kilichomharibia VUNJABEI ni hiki hapa

Vunja bei tatizo kubwa kabisa ni elimu ya biashara na uwekezaji. Hana elimu hiyo. Yaani hayo maduka yake alishindea kujitofautisha. Mi nilishawahi tembelea maduka yake yana bei ka vile unaenda kununua masaki, na ubora wa ovyo sawa na kariakoo tu. Kingine ugali cova
 
Hahaha yaani MBA ya Mzumbe ya 2014 ilikuwa ya kununua. Labda ungeniambua ya UDSM. Yaani Mzumbe hizo enzi vyeti vya Masters vilikuwa vinauzwa na unaweza msela hakuwahi hata kuingia darasani
 
Kwanza kabisa maduka mengi hasa ya mikoani sio ya kwake, anaingia ubia na watu wanatumia jina lake/brand yake kisha ye anachukua some percent.

Pili Biashara skuiz ni ushindani, inahitaji quality na creativity ya hali ya juu, wafanyabiashara wengi skuiz wanaenda extra ikifika kwenye swala la kutangaza biashara zao. Fred nguo zake ni maronya hazina quality, vijana wengine wanaleta nguo zenye quality.

So yes mbali na mdomo lakini pia ame relax sana.
 
Kweli kkoo pale kuna mmama unambeba kwenye bajaji huko mbweni huwez kuamini mjengo unaompeleka alafu yupo kawaida tu lkn unakuta ni bilionea mkubwa sasa vjana mitaji inapokuwa tunataka tukue na brand za social midia

Kina gsm tumekuja kuwajua ni matajir tz nzma wakiwa tayr wana utajiri mkubwa na misingi imara sasa kijana mtaji milioni 500 ushaanza kuweka plate number jina lako
 
Biashara ya madawa ni nzuri ila unakuwa subjected kweny sheria nyingi asikudanganye mtu , kuna vyeti kibao behind unalipia .

Nguo ni rahisi sana na faida yake ni chap , tatizo sio endelevu na ukitoa siri basi kwa sababu sasa watu wanaenda china kwa milion 5 then wanapiga faida ndefu ...Makampuni kibao wanaweka mikonon.

Vunjabei kasome upepo , threats ni nyingi hasa ujio wa wachina ..Hapo china kushakuwa kawaida sana vijana kibao wanaingia ndio maana wakina jaymodel ,wakushine na wengine kibao wanaenda na wanapiga pesa ndefu .
 
Machimbo ya siri yapo , sababu kubwa ni kupata bei nafuu .Kule china kuna viwanda wanatengeneza nguo quality ambazo ukichukua bei yake hapa bongo hutoweza kuuza ni hasara .

Wajanja wanatafuta vile viwanda vya magumashi kama tshirt 1000 ili wapate faida kubwa ...Kuna viwanda vya kuhudumia ndani na nje ...Matapeli wapo kama kawaida , kwenye kuwekewa mzigo unaweza kupigwa ....Wachina ni wajanja sana bila ya kupata mzoefu umekwisha.
 
Duh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…