Lamomy
JF-Expert Member
- Sep 4, 2023
- 25,425
- 59,309
Countrywide nahitaji mchango wako kwa hili
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vunja bei tatizo kubwa kabisa ni elimu ya biashara na uwekezaji. Hana elimu hiyo. Yaani hayo maduka yake alishindea kujitofautisha. Mi nilishawahi tembelea maduka yake yana bei ka vile unaenda kununua masaki, na ubora wa ovyo sawa na kariakoo tu. Kingine ugali covaJuzi kuna memba aliweka uzi kuwashirikisha wanajukwaa kuwa Vunjabei anahisi kama anaenda kufilisika ila hakuwa na uhakika yote ni sababu ameona maduka yake kama yanapumulia Gesi na mengine kufungwa mikoani huko wengine wanadai hadi zile plate no za majina ameondoa kuepuka Garama uchumi hauruhusu.
Ila kwakuwa mimi ni mkongwe wa kariakoo na Biashara ya mavazi naifaham vizuri basi fuatilieni huu uzi ili ambo mpo kwenye biashara hasa zile biashara ambazo zipo on Fire zinawalipa muwe makini maana biashara kupanda na kushuka ukikosea kitu tu ni Dakika moja na kupanda tena ni mtihani.
Ishu ipo hivi
Vunja ni moja ya vijana wa mwanzo kabisa hapa Tz kulijua soko la China ambalo limewaletea utajiri mkubwa vijana wengi wa Tanzania, Vijana wa mwazo kabisa hapa Tanzania kwenda China kubeba mzigo na kuja kupata pesa nyingi hapa Tanzania. Fredi alikuwa ni mmoja wapo na enzi hizo kwenda china hapo kariakoo walikuwa ni madon wachache ambao walikuwa wanayajua machimbo china wanabeba mzigo wanakuja kuwauzia n wafanyabiashara wengine.
Hata moja ya Stori za fredi na vyombo vya habari aliwahi kusema kuwa alianza biasgara na kigoli kidogo vile vifrem vya uchochoroni kariakoo hapo tena alikuwa wanashare mtaji na Rafiki yake ndio wakajichanga ikabidi mmoja wapo aende china akirudi wakiuza mzigo wagawane na kweli fredi mara ya kwanza anaenda China tu kurudi kumwaga mzigo hapo kariakoo ukaisha chap hapo ndio akasanuka kuwa china pesa ipo kipindi hicho china waliokuwa wanapajua ni wachache hapo ndio ukawa mwanzo wa fredi kupiga pesa na kufungua maduka makubwa sinza na sehem nyingine.
Sasa kilichomponza Fredi ni mdomo na kupenda kutoa siri yaani jamaa alivunja Sheria matajiri kamwe ukitaka kuwa tajiri usitoe siri za mafanikio yako kwa public ndio maana Gsm Akiuambiwa tumotivate tuwe kama ww aasema yanga bingwa yaani matajiri huwa hawatoi code ya walipopitia hadi sehem wanapobeba mzigo huwa ni siri, hata hapo kariakoo mtu hawezi kukupa code ni wapi anatoa mzigo huko China ili auze mwenyewe ukijifanya chaumbea tu utafunga Fremu.
Sasa baada ya Fredi kuwamotivate vijana kuwa China pesa ipo matokeo yake vijna wakamskiliza na wakaanza kufanya Research China wakayagundua machimbo ya nguo na viatu vya bei kitonga wakaanza kwenda wenyewe hata wale aliokuwa anawauzia wakawa wanaufuata mzigo wenyewe huko china mwisho wa siku akaengeneza upinzani mkubwa ambao ni chanzo cha kumfikisha hapo alipo.
Na kulikuwa na kesi nyingi za kushusha nguo zilizochini ya kiwango hakufanya reserch kuwa watu wanataka vitu vyenye quality mwisho wa siku vijana wakamletea upinzani wanaleta jeans zenye viwango wanashusha kkoo hapo kwa bei ile ile akaanza kupoteza soko.
Kwa sasa hapo kariakoo kuna vijana ni Madon vunjabei haingii ndani sema vijana wengi hapo kariakoo ni wasiri na hawana kelele ila wana pesa na wanauza balaa na mzigo wanaubeba china sema wamewin sababu ya kushusha jeans na tshrts kali zenye quality wakishusha utakuta watu wanagombania nusu kuuwana.
Kitu kingine ukijifanya wewe ni Tajiri ndio unawakaribisha TRA wakukamue vizuri kuwa msiri sana
Soma Pia: Ni kama vile Vunjabei anaelekea kufilisika
Ila ukiwauliza wanatoa wapi huo mzigo hawatokaa wakupe hiyo siri ila Fredi umbea kujimwambafai na kuwaeleza watu ukweli ndio kulimponza, kama unabiashara yako kamwe usitoe siri za biashara kwa watu huu uzi utakuja kuupitia tena kuwa msiri na mkimya.
Frank kafunga duka la k.koo hapo mtaa wa kongo na mwanza pia....Pale kwa frank saiv yupo Mama mashuka
Hahaha yaani MBA ya Mzumbe ya 2014 ilikuwa ya kununua. Labda ungeniambua ya UDSM. Yaani Mzumbe hizo enzi vyeti vya Masters vilikuwa vinauzwa na unaweza msela hakuwahi hata kuingia darasaniUnatokea pori gani ?
Kuna elimu gani zaidi aliyokuwa nayo sasa ?
View attachment 3090766
![]()
How ‘Fred Vunjabei’ built a Sh4bn business empire at 33
While it is everyone’s dream to succeed in life, some people are luckier than others when it comes to achieving their life goals - with some doing so earlier than others.www.thecitizen.co.tz
Fred aache kulala na wanawake ovyo ovyo wanawake wengi wana mikosi
Wengi hujua kufilisiwa na wanawake huja kwa kuwahonga nop wanawake ni sumu by nature ni kutu ilayo baraka kutoka kwa BWANA
Ulishaga mponza mbona, kipindi fulani alijitapa kuhusu mkwanja wake, TRA wakamtembelea wacha apige yowee.Kama mdomo basi utaenda kumponza na Diamond
Ugali cova? South?Vunja bei tatizo kubwa kabisa ni elimu ya biashara na uwekezaji. Hana elimu hiyo. Yaani hayo maduka yake alishindea kujitofautisha. Mi nilishawahi tembelea maduka yake yana bei ka vile unaenda kununua masaki, na ubora wa ovyo sawa na kariakoo tu. Kingine ugali cova
EehUkishawakaribisha wapambe sijui wasanii machawa kifedha lazima utayumba tu
ova
Hata mimi naona itakuwa amehifadhi mtaji wake benki anataka kubadilisha aina ya biasharaKufilisika inawezekana lakin kwa vunjabei nachelea kusema anafilisika kwasababu ana akili sana yule jamaa
Hao ndio wanafaa kufyonza jicho na kupotea
Ukitafuta wa high level wanakuganda na kukulengesha mitandaoni
Biashara ya madawa ni nzuri ila unakuwa subjected kweny sheria nyingi asikudanganye mtu , kuna vyeti kibao behind unalipia .Sidhani kama kafilisika ila kwasababu yeye alianza inawezekana anaona hailipi kama zamani,maana pia anauza dawa za binadamu,VUNJABEI PHARMACY,ni jumla na rejareja....... inawezekana nguvu amewekeza zaidi huko kwenye dawa,na asikudanganye mtu usidharau hata kiduka cha kuuza dawa mtaani kwasababu kila dawa anapata faida hata zaidi ya nusu..............kama unataka kujua faida ya dawa,uliza bei ya dawa pharmacy kkoo,then dawa hiyo hiyo pita Ubungo,Kimara au Mbezi utanielewa
Machimbo ya siri yapo , sababu kubwa ni kupata bei nafuu .Kule china kuna viwanda wanatengeneza nguo quality ambazo ukichukua bei yake hapa bongo hutoweza kuuza ni hasara .Unataka uniambie viwanda vya kuzalisha hizo nguo kule china ni siri? havijulikani? kwamba lazima ukavitafute ndani ndani huko? Kwani China wanauza products zao Tanzania pekee?
Hakuna Chimbo la siri kule China haya ni maneno ya vijiweni tu. Ukisema mwanzo watu ilikiwa ushamba na hawaendi kuchukua mzigo china hapo sawa, Ila kusema ni machimbo ya Siri hizo ni stories za vijiwe vya kahawa.
DuhMachimbo ya siri yapo , sababu kubwa ni kupata bei nafuu .Kule china kuna viwanda wanatengeneza nguo quality ambazo ukichukua bei yake hapa bongo hutoweza kuuza ni hasara .
Wajanja wanatafuta vile viwanda vya magumashi kama tshirt 1000 ili wapate faida kubwa ...Kuna viwanda vya kuhudumia ndani na nje ...Matapeli wapo kama kawaida , kwenye kuwekewa mzigo unaweza kupigwa ....Wachina ni wajanja sana bila ya kupata mzoefu umekwisha.