Kilichomharibia VUNJABEI ni hiki hapa

Kilichomharibia VUNJABEI ni hiki hapa

Believe me
Aliyeleta hii post
Ni kijana msomi anaetegemewa na wazazi wake, waliotumia muda wao kumsomesha
Huyu ndio kijana tunamtegemea wale polisi waliomteka mzee kibao angekua kwenye gari awazuie yeye na vijana wenzake
Hawa ndo vijana wetu wa Tanzania na huu ndo uhalisia wa namna wanavyofikiria
Deep deep problem in this country
 
Sasa hao ndo wakwanza kwenda china na kuleta mzigo bongo vunja bei mtoto mdogo kwenye game kuliko wamba hao ila wote chali vunja bei misifa mingi kujiona bora sana kuliko hao waliopita bora abakie kwenye siasa ccm watampa shavu la UDC
Hivi UDC kwa mtu kama Fred ni demotion au promotion?? Au UDC unalipa sana??
 
Siyajui ya Fred ila nina uhakika na ninakubaliana na wewe mdomo mdomo kitu kibaya sana...
Kikupacho utajiri kifanye siri.
Kikupacho raha na furaha kifanye siri.

Neno la Mungu tu ndio liseme seme na uwatangazie watu bure ,si zaid ya hapo

Nashangaaga sana, hata ku post post status huku watu jifungen break kupost vitu confidential, much personal
Sahihi sana mkuu
 
Dah! Huu ushirikina mtaacha lini?
Hapana sio ushirikina ni mambo ya Rohoni hayo!.
Kulala hovyo na wanawake kunaondoa baraka sana.
Tena kama huamnini hata makanisani au kwa waganga wa kienyeji kama unatafuta tiba ya matatizo yako huwa wanaangalia sana mambo kama hayo ya Zinaa huwa yanapingwa sana.
Mganga wa kienyeji kama umelala na mwanamke alafu ukaenda kwake atakuambia kaoge.
Vivyo hivyo hata makanisani wanapinga sana mambo ya Uzinifu.
Sio ushirikina huo ni Swala la kiroho kama ni muamini.
 
Hapana sio ushirikina ni mambo ya Rohoni hayo!.
Kulala hovyo na wanawake kunaondoa baraka sana.
Tena kama huamnini hata makanisani au kwa waganga wa kienyeji kama unatafuta tiba ya matatizo yako huwa wanaangalia sana mambo kama hayo ya Zinaa huwa yanapingwa sana.
Mganga wa kienyeji kama umelala na mwanamke alafu ukaenda kwake atakuambia kaoge.
Vivyo hivyo hata makanisani wanapinga sana mambo ya Uzinifu.
Sio ushirikina huo ni Swala la kiroho kama ni muamini.
Tafsiri ya kulala hovyo ni ipi?
 
Watu weusi tuna changamoto ya sustainability ya utajiri ndo maana haukai, tunajua kutumia bila ya kuwekeza kwenye miradi ambayo itakuwa inakulipa wakati umelala. Kwa level zake angeweza kumpata Guru mmoja wa investment amsaidie kuwekeza hela zake mengine yangebaki stori.
 
Yaani kutokua na mwanamke mmoja Au kuwa na wanawake tofauti tofauti kimahusiano ya kimapenzi Au kufanya mapenzi na wanawake tofauti tofauti.

Nb; Mwanamke mmoja anatosha kabisa.
Mbona diamond hafilisiki na amezaa na wanawake wanaojulikana zaidi ya 3 ninaowakumbuka? Mbona sulemani alikua na wanawake buku lakini hakufilisika? Mwisho nauliza tena kwanini mwanamke tu ndio awe na mikosi? Hivi unaamini Mungu alimuumba mwanamke na mwanaume?
 
Juzi kuna memba aliweka uzi kuwashirikisha wanajukwaa kuwa Vunjabei anahisi kama anaenda kufilisika ila hakuwa na uhakika yote ni sababu ameona maduka yake kama yanapumulia Gesi na mengine kufungwa mikoani huko wengine wanadai hadi zile plate no za majina ameondoa kuepuka Garama uchumi hauruhusu.

Ila kwakuwa mimi ni mkongwe wa kariakoo na Biashara ya mavazi naifaham vizuri basi fuatilieni huu uzi ili ambo mpo kwenye biashara hasa zile biashara ambazo zipo on Fire zinawalipa muwe makini maana biashara kupanda na kushuka ukikosea kitu tu ni Dakika moja na kupanda tena ni mtihani.

Ishu ipo hivi

Vunja ni moja ya vijana wa mwanzo kabisa hapa Tz kulijua soko la China ambalo limewaletea utajiri mkubwa vijana wengi wa Tanzania, Vijana wa mwazo kabisa hapa Tanzania kwenda China kubeba mzigo na kuja kupata pesa nyingi hapa Tanzania. Fredi alikuwa ni mmoja wapo sijasema kwamba ni wa kwanza ila kati ya watu wa mwanzo kufaidika na mizigo ya china humtoi kwenye list, na enzi hizo kwenda china hapo kariakoo walikuwa ni madon wachache ambao walikuwa wanayajua machimbo china wanabeba mzigo wanakuja kuwauzia na wafanyabiashara wengine.

Hata moja ya Stori za fredi na vyombo vya habari aliwahi kusema kuwa alianza biasgara na kigoli kidogo vile vifrem vya uchochoroni kariakoo hapo tena alikuwa wanashare mtaji na Rafiki yake ndio wakajichanga ikabidi mmoja wapo aende china akirudi wakiuza mzigo wagawane na kweli fredi mara ya kwanza anaenda China tu kurudi kumwaga mzigo hapo kariakoo ukaisha chap hapo ndio akasanuka kuwa china pesa ipo kipindi hicho china waliokuwa wanapajua ni wachache hapo ndio ukawa mwanzo wa fredi kupiga pesa na kufungua maduka makubwa sinza na sehem nyingine.

Sasa kilichomponza Fredi ni mdomo na kupenda kutoa siri yaani jamaa alivunja Sheria matajiri kamwe ukitaka kuwa tajiri usitoe siri za mafanikio yako kwa public ndio maana Gsm Akiuambiwa tumotivate tuwe kama ww aasema yanga bingwa yaani matajiri huwa hawatoi code ya walipopitia hadi sehem wanapobeba mzigo huwa ni siri, hata hapo kariakoo mtu hawezi kukupa code ni wapi anatoa mzigo huko China ili auze mwenyewe ukijifanya chaumbea tu utafunga Fremu.

Sasa baada ya Fredi kuwamotivate vijana kuwa China pesa ipo matokeo yake vijna wakamskiliza na wakaanza kufanya Research China wakayagundua machimbo ya nguo na viatu vya bei kitonga wakaanza kwenda wenyewe hata wale aliokuwa anawauzia wakawa wanaufuata mzigo wenyewe huko china mwisho wa siku akaengeneza upinzani mkubwa ambao ni chanzo cha kumfikisha hapo alipo.

Na kulikuwa na kesi nyingi za kushusha nguo zilizochini ya kiwango hakufanya reserch kuwa watu wanataka vitu vyenye quality mwisho wa siku vijana wakamletea upinzani wanaleta jeans zenye viwango wanashusha kkoo hapo kwa bei ile ile akaanza kupoteza soko.

Kwa sasa hapo kariakoo kuna vijana ni Madon vunjabei haingii ndani sema vijana wengi hapo kariakoo ni wasiri na hawana kelele ila wana pesa na wanauza balaa na mzigo wanaubeba china sema wamewin sababu ya kushusha jeans na tshrts kali zenye quality wakishusha utakuta watu wanagombania nusu kuuwana.

Kitu kingine ukijifanya wewe ni Tajiri ndio unawakaribisha TRA wakukamue vizuri kuwa msiri sana hata Diamond platnumz hapa juzi alijitamba anaingiza Mabilioni ndio Tra wakamtembelea kumjulia hali nadhani mliona alivyobanwa kidogo tu namna alivyotoa mluzi kwa kilio kuwa wanataka kumfilisi

Soma Pia: Ni kama vile Vunjabei anaelekea kufilisika

Wafanya biashara wa kariakoo wana siri sio mchezo,ukiwauliza wanatoa wapi huo mzigo hawatokaa wakupe hiyo siri ila Fredi umbea kujimwambafai na kuwaeleza watu michongo yake ndio ni sababu moja wapo inayo muharibia, kama unabiashara yako kamwe usitoe siri za biashara kwa watu huu uzi utakuja kuupitia tena kuwa msiri na mkimya.

Na kwa kumalizia kabisa kuna watu wanasema jamaa hajafulia ila kaamia kwenye uuzaji wa madawa ila hata huko kwenye pharmacy asipouchunga mdomo wake na kukaa kimya, akiendelea kutoa siri za kambi atawakaribisha wapinzani ambao watamsumbua, Utajiri unahitaji utulivu na ukimya wewe jifanye muongeaji utaonyeshwa....
Huyu mwamba fundi wake aka mganga atakuwa kagoma kula.
 
Back
Top Bottom