Kilichomharibia VUNJABEI ni hiki hapa

Kilichomharibia VUNJABEI ni hiki hapa

Acha bana, ina maana panadol ya bristapack ya Kariakoo ina tofautiana na ya Mwenge?
Unadhani bei anayonunulia kwa jumla anakuuzia kwa bei ile ile? Ukienda kununua Panadol kkoo na Mwenge inawezekana ikawa the same price kwasababu unaenda kununua vidonge kadhaa kwaajili ya kumeza na atakuuzia kwa bei sawa na tegeta
 
Uongo Whozu hawezi kumaliza Advance 2007.Hukuona hata video yake akiwa yupo Bwenini shule sijajua ni Olevel au Advance akiwa anacheza wimbo wa Diamond Platinumz "Nana"??! Sasa Nana ulitoka miaka hiyo ya 2007 au?!. Kama ni kweli kamaliza hapo Galanos fuatilia vizuri miaka aliyomaliza lakini sio 2007.Watu waliomaliza chuo miaka ya 2007 ni kama Zitto Kabww, John Mnyika Etc, sasa je Kina Zitto unataka kusema wamempita darasa moja tu Whozu
Hivi hata unemuelewa au umekimbilia kujibu, amesema kaka ake na whozu - Frank knows sio whozu
 
Sidhani kama kafilisika ila kwasababu yeye alianza inawezekana anaona hailipi kama zamani,maana pia anauza dawa za binadamu,VUNJABEI PHARMACY,ni jumla na rejareja....... inawezekana nguvu amewekeza zaidi huko kwenye dawa,na asikudanganye mtu usidharau hata kiduka cha kuuza dawa mtaani kwasababu kila dawa anapata faida hata zaidi ya nusu..............kama unataka kujua faida ya dawa,uliza bei ya dawa pharmacy kkoo,then dawa hiyo hiyo pita Ubungo,Kimara au Mbezi utanielewa
Uko sahihi. Biashara ya nguo ni kama takataka mbele ya biashara yoyote inayohusiana na afya. Wauza madawa na vifaa tiba wana hela ndefu mno. Faida ya vitu vyao huwa ni zaidi ya 200% ya bei ya kununulia.
 
Uongo Whozu hawezi kumaliza Advance 2007.Hukuona hata video yake akiwa yupo Bwenini shule sijajua ni Olevel au Advance akiwa anacheza wimbo wa Diamond Platinumz "Nana"??! Sasa Nana ulitoka miaka hiyo ya 2007 au?!. Kama ni kweli kamaliza hapo Galanos fuatilia vizuri miaka aliyomaliza lakini sio 2007.Watu waliomaliza chuo miaka ya 2007 ni kama Zitto Kabww, John Mnyika Etc, sasa je Kina Zitto unataka kusema wamempita darasa moja tu Whozhu?
Wewe ni mtu mjinga mno.
 
Nimesoma huu uzi ila kusema kuwa Fred alikuwa miongoni mwa vijana wa mwanzo kwenda China ninakataa. Watu kibao kabla ya 2010 walishaenda China. Hiyo 2010 Fred alikuwa mwanafunzi. Pia hakuna siri yoyote kubwa kuhusu machimbo ya China. Wafanyabiashara za nguo huenda na samples na kutengenezewa kulingana na samples. Pia kudumu kama kinara kwenye biashara ya nguo au nyingine yoyote sio jambo rahisi hata ukiwa low profile kiasi gani. Wafanyabiashara smart hufanya mabadiliko kuendana na uhitaji wa soko au hujiondoa kabisa kwenye hizo biashara haraka na kuhamia kwenye zingine. Kuna mama fulani Arusha alikuwa ni miongoni mwa wafanyabiashara wa mwanzo kuanza kununua na kuuza bidhaa za Dubai hasa phone and accessories.. ila kufikia mwaka 2008 aliacha hizo biashara na kununua mashine za kufyatua matofali. Ghafla tena akaanza kukimbiza huo upande na kununua malori kadhaa za kubeba matofali yake. Kimsingi jimama halichuji kabisa kifedha. Huenda Vunjabei naye ameshaanza kuhamisha mtaji kwenda kwingine. Kama ni kweli anafilisika itajulikana tu. Mimi nampongeza Fred kwa kuchakata mbususu ya Mheshimiwa Jokate.
 
Wamesoma EGM. Fred alipiga ONE na huyo Frank alipiga TWO. Kwa darasani Fred ni hatari.
Sifahamu ila najua walikuwa wanafunzi wangu na walikuwa wanatoroka sana kwenda majani mapana na wenzake akina Kipesha, Bulldog, John, yule mtoto wa shimbo Geofrey, Amani na wenzake. Walikuwa wanaishi bweni la chai Cube namba 16 na 17.

Nilikuwa nawaomba fimbo hao wakitoroka na kuwahimiza kisha kuwashika mi na mwalimu Msocha.😀😀😀

Hayo ya matokeo siyajui mkuu.
 
Sifahamu ila najua walikuwa wanafunzi wangu na walikuwa wanatoroka sana kwenda majani mapana na wenzake akina Kipesha, Bulldog, John, yule mtoto wa shimbo Geofrey, Amani na wenzake. Walikuwa wanaishi bweni la chai Cube namba 16 na 17.

Nilikuwa nawaomba fimbo hao wakitoroka na kuwahimiza kisha kuwashika mi na mwalimu Msocha.😀😀😀

Hayo ya matokeo siyajui mkuu.
Wewe ni mwalimu wa hovyo kama hujui performance za wanafunzi wako. Wewe unajua mabaya yao tu? Mzee wa hovyo kweli kweli.
 
Sifahamu ila najua walikuwa wanafunzi wangu na walikuwa wanatoroka sana kwenda majani mapana na wenzake akina Kipesha, Bulldog, John, yule mtoto wa shimbo Geofrey, Amani na wenzake. Walikuwa wanaishi bweni la chai Cube namba 16 na 17.

Nilikuwa nawaomba fimbo hao wakitoroka na kuwahimiza kisha kuwashika mi na mwalimu Msocha.😀😀😀

Hayo ya matokeo siyajui mkuu.
Na mimi nilisoma usagara wakati huo machali wenu wana upwiru wa mademu.
 
Sio kweli kwamba eti hakua msiri,tukubaliane tu kwamba dunia imekua kijiji,na biashara zimerahisishwa siku hzi...hakuna sehemu utajifanya uko peke yako..watu wanajua kutafuta fursa..zamani mtu ukimtajia china alikua anawaza atafikaje atafanyaje..lakini kila kitu kimerahisishwa na ndio maana wengi wanaenda.
 
Juzi kuna memba aliweka uzi kuwashirikisha wanajukwaa kuwa Vunjabei anahisi kama anaenda kufilisika ila hakuwa na uhakika yote ni sababu ameona maduka yake kama yanapumulia Gesi na mengine kufungwa mikoani huko wengine wanadai hadi zile plate no za majina ameondoa kuepuka Garama uchumi hauruhusu.

Ila kwakuwa mimi ni mkongwe wa kariakoo na Biashara ya mavazi naifaham vizuri basi fuatilieni huu uzi ili ambo mpo kwenye biashara hasa zile biashara ambazo zipo on Fire zinawalipa muwe makini maana biashara kupanda na kushuka ukikosea kitu tu ni Dakika moja na kupanda tena ni mtihani.

Ishu ipo hivi

Vunja ni moja ya vijana wa mwanzo kabisa hapa Tz kulijua soko la China ambalo limewaletea utajiri mkubwa vijana wengi wa Tanzania, Vijana wa mwazo kabisa hapa Tanzania kwenda China kubeba mzigo na kuja kupata pesa nyingi hapa Tanzania. Fredi alikuwa ni mmoja wapo sijasema kwamba ni wa kwanza ila kati ya watu wa mwanzo kufaidika na mizigo ya china humtoi kwenye list, na enzi hizo kwenda china hapo kariakoo walikuwa ni madon wachache ambao walikuwa wanayajua machimbo china wanabeba mzigo wanakuja kuwauzia na wafanyabiashara wengine.

Hata moja ya Stori za fredi na vyombo vya habari aliwahi kusema kuwa alianza biasgara na kigoli kidogo vile vifrem vya uchochoroni kariakoo hapo tena alikuwa wanashare mtaji na Rafiki yake ndio wakajichanga ikabidi mmoja wapo aende china akirudi wakiuza mzigo wagawane na kweli fredi mara ya kwanza anaenda China tu kurudi kumwaga mzigo hapo kariakoo ukaisha chap hapo ndio akasanuka kuwa china pesa ipo kipindi hicho china waliokuwa wanapajua ni wachache hapo ndio ukawa mwanzo wa fredi kupiga pesa na kufungua maduka makubwa sinza na sehem nyingine.

Sasa kilichomponza Fredi ni mdomo na kupenda kutoa siri yaani jamaa alivunja Sheria matajiri kamwe ukitaka kuwa tajiri usitoe siri za mafanikio yako kwa public ndio maana Gsm Akiuambiwa tumotivate tuwe kama ww aasema yanga bingwa yaani matajiri huwa hawatoi code ya walipopitia hadi sehem wanapobeba mzigo huwa ni siri, hata hapo kariakoo mtu hawezi kukupa code ni wapi anatoa mzigo huko China ili auze mwenyewe ukijifanya chaumbea tu utafunga Fremu.

Sasa baada ya Fredi kuwamotivate vijana kuwa China pesa ipo matokeo yake vijna wakamskiliza na wakaanza kufanya Research China wakayagundua machimbo ya nguo na viatu vya bei kitonga wakaanza kwenda wenyewe hata wale aliokuwa anawauzia wakawa wanaufuata mzigo wenyewe huko china mwisho wa siku akaengeneza upinzani mkubwa ambao ni chanzo cha kumfikisha hapo alipo.

Na kulikuwa na kesi nyingi za kushusha nguo zilizochini ya kiwango hakufanya reserch kuwa watu wanataka vitu vyenye quality mwisho wa siku vijana wakamletea upinzani wanaleta jeans zenye viwango wanashusha kkoo hapo kwa bei ile ile akaanza kupoteza soko.

Kwa sasa hapo kariakoo kuna vijana ni Madon vunjabei haingii ndani sema vijana wengi hapo kariakoo ni wasiri na hawana kelele ila wana pesa na wanauza balaa na mzigo wanaubeba china sema wamewin sababu ya kushusha jeans na tshrts kali zenye quality wakishusha utakuta watu wanagombania nusu kuuwana.

Kitu kingine ukijifanya wewe ni Tajiri ndio unawakaribisha TRA wakukamue vizuri kuwa msiri sana hata Diamond platnumz hapa juzi alijitamba anaingiza Mabilioni ndio Tra wakamtembelea kumjulia hali nadhani mliona alivyobanwa kidogo tu namna alivyotoa mluzi kwa kilio kuwa wanataka kumfilisi

Soma Pia: Ni kama vile Vunjabei anaelekea kufilisika

Wafanya biashara wa kariakoo wana siri sio mchezo,ukiwauliza wanatoa wapi huo mzigo hawatokaa wakupe hiyo siri ila Fredi umbea kujimwambafai na kuwaeleza watu michongo yake ndio ni sababu moja wapo inayo muharibia, kama unabiashara yako kamwe usitoe siri za biashara kwa watu huu uzi utakuja kuupitia tena kuwa msiri na mkimya.

Na kwa kumalizia kabisa kuna watu wanasema jamaa hajafulia ila kaamia kwenye uuzaji wa madawa ila hata huko kwenye pharmacy asipouchunga mdomo wake na kukaa kimya, akiendelea kutoa siri za kambi atawakaribisha wapinzani ambao watamsumbua, Utajiri unahitaji utulivu na ukimya wewe jifanye muongeaji utaonyeshwa....
Kosa kubwa la Fred ilikuwa kufungua ofisi nyingi wakati bado hajasimama vizuri na kuwa na mameneja wazuri.
 
Unataka uniambie viwanda vya kuzalisha hizo nguo kule china ni siri? havijulikani? kwamba lazima ukavitafute ndani ndani huko? Kwani China wanauza products zao Tanzania pekee?

Hakuna Chimbo la siri kule China haya ni maneno ya vijiweni tu. Ukisema mwanzo watu ilikiwa ushamba na hawaendi kuchukua mzigo china hapo sawa, Ila kusema ni machimbo ya Siri hizo ni stories za vijiwe vya kahawa.
Umewahi kufuata biashara china au unajiropokea tu?
 
Back
Top Bottom