Tetesi: Kilichomponza Diamond ni Sakata la ATCL

"INFLUENCES POWER" au sisi wabongo husema ana nguvu ya ushawishi mkubwa sana katika kuleta wateja kwenye biashara yoyote ile tokana na umaarufu wake.

Ndiyomaana mashirika mbali mbali duniani hutumia Watu kama wasanii, wanamichezo, wanariadha ili biashara zao ziwavutie wateja sababu wanaamini kuwa tayari Watu kama hawa hupendwa sana na Watu wengi duniani.
 
Mimi ningekuwa daimond ningehama nchi na ningebadili uraia,mbona wakati anauza mitumba basata hawakumsumbua?yani tuna baraza la kufungia nyimbo peke yake.
Hata akihama bado Tanzania itaendelea kuwepo na dunia itazunguka tu, nakutolea mfano thabiti hata akina Lionel Mess huwa wanawajibishwa sana kisheria ikiwa hawakufuata sheria na kanuni za nchi.

Mfano kuhusu kukwepa kulipa kodi Hispania, so haimaanishi kuwa ukiwa vizuri kiuchumi ndiyo usiitii mamlaka inayokuongoza katika nchi unayoishi au unazotembelea kwa masilahi yako binafsi.

Dola itaendela kuheshimika sababu hata huo uhuru alionao wa kuzunguka nchi yote akifanya shoo zake za mziki ni sababu nchi inawajibika kumlinda kwa amani kupitia askari wake, la sivyo asingeweza kuthubutu hata toka mkoa m1 kwenda mwingine laiti pangekuwa hapana amani.
 
Mahaba ya ushabiki kwa mtu asiyejielewa akiongozwa na kiburi cha pesa ndiyo yanatusumbua kupagawa kiasi hicho chote Chifu.
 
Ni kwer kabisa mkuu...Hata hapa kwenye huu Uzi tayari wengi wameichukia ATCL ni dhahili kwamba chanzo ni msanii diamond...yeye mambo mengine anafanyaga ujinga lakin serekali inatambua umuhimu wake inaamua kupotezea lakini yeye kafanyiwa hivo kakimbilia Instagram...Duh....kweri wamemkosea lakini inapaswa afate masharti ..huyo alierekodiwa keshadhalilishwa kwa upande flani hivi...
 
Sana " yule mzee kadhalilishwa sana binafsi sikupenda alichofanyiwa
 
Taasisi ya umma haikosolewi? Hao wanaoongoza hiyo taasisi si ni binadamu kama wewe kwamba hawafanyi makosa?
 
Kufanikiwa siyo kuwa vizuri kiuchumi, je mahusiano yako na jamii inayokuzunguka katika maisha uishiyo inaakisi au inazaa matunda mema kwa kumpendeza Mungu?

Kila mwenye pesa anaishi maisha ya furaha(ametawaliwa na amani nzuri rohoni mwake)?
Hahaa mindset za watu wengi sana wanadhani kuwa kufanikiwa nikuwa na ukwasi tu pekee " huu ni ujuha" ... kwa mantiki hiyo waliyonayo basi tunaweza kusema kuwa che Guevara" na wana harakati wengi sio watu waliowahi kufanikiwa
 
Dah...hili ni somo jingine tena...hasa kwa wale wote wasiotaka kuelewa nguvu ya aliyempiga Goliath...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hahaaa inamaana round hii bashite hana cha kuwafanya BASATA ??
.
hii inamaanisha kwamba maamuzi ya BASATA ni amri iliyotoka juu
 
Taasisi ya umma haikosolewi? Hao wanaoongoza hiyo taasisi si ni binadamu kama wewe kwamba hawafanyi makosa?
Muwage mnasoma nakuelewa basiii "" gosh mnachosha ".... wapi nimesema kwamba taasisi ya serikali haikosolewi "!?

Kukosoa ni haki ya kila raia " bali tunapaswa kukosoa kwa njia rafiki ambayo haitoleta athari za kushuka kwa bidhaa/biashara na kuwafanya watu wengine waweze kukosa Ajira katika biashara hiyo ..
 
Management yake ndio inabidi ilaumiwe,Diamond ni mwanamuziki makubwa mwenye hadhi kubwa kama waziri au balozi,yote haya yasingetokea kama angekuwa na meneja uhusiano mzuri,ambaye angekuwa amefatiria ishu ya tiketi mapema,na kumwepusha Mond na balaa hili LA kutoa maneno ya ovyo na kurekodiwa,au angewaona basata au viongozi wa ATCL mapema na kusawazisha mambo,kabla hayajaharibika.
Vijana wakisha kuwa na hela,wanakuwa na tabia za ajabu,au wakati mwingine wanateleza na kutoa kauli za hovyo,Personal relation manager angeweka mambo vzr,na maisha yangeendelea.
Basata nao wamechemuka,azabu waliyotoa ni kubwa sana,wangempiga faini ingekuwa poa sana.
Mond ndio wasafi,ukimzuia asiingize pesa,Kampuni yote ya wasafi,itatetereka,hata hisa zake zinaweza kushuka thamani,
Kampuni imeajiri vijana wengi,tamasha lingeingizs pesa nyingi na kuwapa kipato vijana wengi,na makampuni yaliyodhamini,sio sahihi kuwaumiza wote hao kisa wimbo tu.
Hii adhabu ni kubwa sana.Basata wameonyesha chuki kubwa kwa kijana aliyejitengenezea utajiri.
Ni bora apigwe faini,maisha yaendelee,na wengine wote wanaoitegemea Wasafi,wasipate shida.
 
Jana ilikuwa siku mbaya sana kwangu..!
Kwanza namkubali sana Diamond Platnum lakini pia namkubali sana Jose Morinho! Unaweza jiuliza sasa nilikuwa katika hali gani jana......................πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
 
Mimi ningekuwa daimond ningehama nchi na ningebadili uraia,mbona wakati anauza mitumba basata hawakumsumbua?yani tuna baraza la kufungia nyimbo peke yake.
We jamaa wakati anauza mitumba alikuwa na nguvu ya ushawishi kwa jamii?? Hata hizo taratibu za ndege alikuwa anazijua?? Ndege alikuwa akiziona angani tu na kusikia muungurumo wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…