Forex... forex.... forex, kuna mtu mwingine juzi humu kalialia sana kupoteza hela mpaka anamtukana demu wake aliemsaidia milioni 1 na nusu. Vijana mtapata ukichaa kwa hela za kwenye screen za simu na computer wanazowadanganya wazungu, hela ambazo sio tangible.. huishiki. Fanya kazi nyingine ongeza kipato chako bila stress za mitandao kuzima kama ilivyozimwa D9Clube.. mbona hela zipo kwingine kwingi tuuu? kwa nini mpende ukitonga wa hela nyepesi umekaa zenyewe zinakuja??? uliskia wapi hela inatafutwa hivyo? hela ifuate... hela kapigane ngumi na vijana wanakuibia... hela katoke jasho tukuone... hiyo ndo hela halali, na hela inakua tamu umeisotea... nenda kariakoo kalenge viatu, yebo za kanye, au nguo kauze mkoani huko mwanza, kigoma na mikoa mingine.. kapande Kisbo, Nyehunge.. kagombane na makonda wa mizigo... uspo pata hela njoo ututukane wote humu tumekudanganya. Usije kulia lia na mambo yenu ya forex au wale jamaa wa QNET kila muda goodmorning kama vichaa. Badilikeni ... tutawaskia wengi tuu wanakuja na hasira zao humu..