Kilichonifanya niachane na forex ni hiki hapa

Kilichonifanya niachane na forex ni hiki hapa

Nina hamu ya kupambana nakosa motivation.Kitaa waniambia ntaliwq tu
Kwenye maisha kila mtu ana namna yake ya kutoka, coz hatufanani malengo na mafanikio na wala njia ya kutoboa

Katika umri wetu tunapambana na kila fursa ila itakayokubali ndo hiyo hiyo

Ila jamii yetu kubwa ya Tanzania tumezaliwa before Technology, kwahyo vitu kama hivi lazima vionekane ni utapeli

Kina kitu kinaitwa stock market huko ndo jamii kubwa ya watu wa Ulaya wanaishi nayo hii, wanachokifanya ni kununua shares za makampuni mbalimbali na wanabaki kupata mgawo wao kila mwezi na maisha yao yanasonga hadi wajukuu wanakuja na kurithi zile shares walizonunua mababu zao.
 
So uliamua kabisa uanze na real gun ili ujue risasi ikikupiga inakupigaje. Big up Sana
ndio mkuu, nilitia dola 40, nikaizalisha mala tatu nikala faida then nikachomaa, so nachomaga sanaa na nishazoea kupoteza nachukulia ni sehemu ya maisha tu cha msingi afya njema,chakula,na sehemu ya kulala
 
sasa kwanini unasema broker mzuri hacheat sana?
unamajibu humohumo ila hautaki kujiuliza haya huyo broker anajisajili kwa nani?
rudi kwenye andiko langu kuna maswali yapo ya msingi sana pale nisaidie kujibu labda na wadau wengine wanaweza wakaelewa vzuri
learn all stuffs concerning speculations
 
Najua wote muwazima

wacha nisonge kwa mada moja kwa moja

nimewahi kuleta maandiko mbali mbali ya forex humu kwa siku za nyuma kipindi nikiwa naifanya nk

kwa mara ya kwanza nimeijua mwaka 2013 japo nilianza rasmi kuisoma na kuifanya mwaka 2015, kwa uhalisia siwezi sema nimewahikuliwa nikijumlisha faida na kutoa hasara.

Kwa haraka haraka nilitumia kama laki na 80 kununua materials kwaajili yakujisomea, lakini pia ilinigarimu tsh laki mbili kuweza kuwapooza baadhi ya waalimu ambao sikuwaweka rasmi kama walimu wangu bali niliwatumia kwa muda tofauti tofauti kujifunza kwa njia ya maswali ili kuongeza udhoefu hivyo niliwapoza kidogo kidogo kama kulipia muda wao wanaojitolea kukaa pamoja namimi.

hadi naingia mwaka 2019 naweza kusema nilikuwa ni miongoni mwa watu wanaoingiza faida fulani inayoonekana na kueleweka

nilizingatia sana kujikita katika kuweza kuielewa forex katika theory na application yake.
Lengo ilikuwa mimi na forex iwe ndio kazi ya maisha yangu wala nisihangaike kufungua madarasa nk, zaidi zaidi tu niwe ni mtu wa kuwekeza katika kuchambua masoko nakutumbua pesa zangu(bata) na kuzidi kuwekeza katika miradi mbalimbali huku nikiwanyanyua ndugu zangu maana kupitia forex nilitaka hadi inapofika 2030 walau ukoo wangu niwe nimeutengenezea hata ma bilionea zaidi ya kumi.
Ila tatizo lilianzia hapa na ndio ambapo niliweza kusanuka mapema nisiendelee kupoteza muda

1.HAIJARISHI UMEISOMA FOREX KWA UNDANI KIASI GANI UMEFUNDISHWA NA WATU WAKUBWA KIASI GANI HAKUNA MPANGO SAHIHI / AU MKAKATI SAHIHI WA FAIDA KATIKA BIASHARA YAKO.

Yaani hapa ndio biashara ilipo lakini pia bado hauwezi kuwa na uhakika wasoko lako sababu lazima tu utaingia chakike vilevile, yaani kwa ufupi naweza sema hivi unaweza chambua soko lako na unafikia hatua ambayo hakuna mapungufu yoyote lakini bado unaweza ukapigwa vilevile na sio hapo tu ukisoma sana forex inakusaidia KUPUNGUZA KIWANGO CHA HASARA NA KUBALANCE MTAJI WAKO ILA SIO UHAKIKA WA KUPATA FAIDA YAKO.

hebu fikiria unafanya biashara lakini hauna hesababu yoyote ya uhakika wakuweza kuingiza faida yako hivi inakuja akilini kweli?

2.HAKUNA WAFANYABIASHARA WAKUBWA WANAOIONA FOREX KAMA BIASHARA YA FAIDA WALA MABENKI HAWAFANYI UTOPOLO HUU.
Kuna mtu aliwahi kusema humu jf kuwa forex ni biashara ambayo mabenki hawataki ujue ila ukweli naweza kusema hapa alituingiza chaka wote tulioamini hii kitu sababu hakuna kitu kama hicho ILA SASA
Forex wanaoweza kupata faida ni wale wanao trade na mitaji mikubwa tena kupitia mzunguko halisi wa pesa sio hizo virtual money sijui uweke kwa broker nk
Ndio maana mtu akisoma forex akielewa vizuri anakimbilia kuwa mwalimu ili awapige wanafunzi na kubalance hasara zake akijitahidi kukuza mtaji ukawa mkubwa anaamua kuwa broker yaani hataki yeye kutrade ila anataka wewe utrade mfano mzuri hapa ndio Sir Jeff aka Ontorio sijui nadhani mnamjua.
Sasa biashara ambayo inakimbiwa na wafanya biashara wakubwa na mtu anakushawishi wewe ndio utrade kwake basi hapo hakuna kitu cha ukweli ni ubadhilifu tuuu.

Sasa mwisho wa siku nikaona FOREX ni ktu kimekuja kutufanya vijana tupoteze muda mwingi kujikita katika virtual money na tuhangaike kupoteza muda katika mambo yasiyo ya msingi,
Unaweza kulamba bingo ila haina tofauti na tatu mzuka kwakweli, zaidi ya yote zile fundamental zote huwezi kuuona mfumo wake kwa uwazi, na zaidi ya hapo hakuna mtu anayejua ile pesa inamilikiwa na nani sababu ni virtual money wala sio real money ndio maana unapitia mabroker ambao hata hawahusiani katiba na uhalisia

fungua real account katika mt4 yako fungua pair sawa na demo account ingia live market kisha jishuhudie mchezo hapo utashangaa sana

Naenda kula na kuoga nitarudi kuendelea kutiririka mambo mengine ya msingi nk

UPDATES

Naendelea tena na uzi.
Kuna jambo moja muhimu sana liko katika msemo unaosema hivi "Always a House win"
Huu msemo hutumika sana katika vitu ambavyo vinafaida kubwa zaidi ya upande mmoja, mfano mzuri nitakaouweka hapa ni yale mambo ya betting.
Jiulize swali hili kwanini sportpesa wao wanamiliki betting ikiwa wanaweza kuwa na watu wazuri wanaojua namna ya kupangilia alama za ushindi(odds) na wakabeti kwa makampuni makubwa mengine wakapata mihela mingi?
sasa ukijiuliza hilo utajua yakuwa huko hakuna uhakika wa ushindi sasa betting zote wanajiweka safe sade wanakaa upande salama wapo winning house huko wanapiga pesa kuliko wewe unayeitamani ile mil 500 ya jackpot.
hebu fikiria mtu anachukua asilimia 99 ya faida halafu ninyi mnabakiwa na asilimia 1 tu.

ndio maana katika forex pia mtu akisoma nakuielewa vyema na anahitaji kutengeneza pesa huwa siku zote anaanza nayeye kukimbilia safe side anajipeleka katika wining house ili awe salama.
Kuna maswali haya hapa nayewa yatakusaidia kujua nini kinaendelea ukiweza kuyajibu kiufasaha
1.Kwanini unauza pips ikiwa wewe ni mtu wa faida?
2.kwanini unafungua darasa kula laki laki za watu ikiwa unamake kuzidi hiyo ada?
3.kwanini unajiweka kuwa broker uanze kula hela za matrder wengine ambapo unaweza kumake pesa ndefu kuzidi hiyo ya ubroker?
4.Yule broker wetu yeye anasimama baina ya trader na nani? huyo aliye juu ya broker ni asasi ipi yenye makao yake wapi inasimamiwa na nani? tunaweza kuingia hata wikpedia tukapata habari zake?

maswali machache sana hayo hilo la mwisho linahitaji majibu yaloshiba

Neno langu sio sheria hii ni kwa mtazamo wangu ukiona inafaida unaweza komaa nayo tu ila kumbuka
"ALWAYS A HOUSE WINI"
tchao.

Updates No 2 Sep 1

NImekuja kuongeza updates nyingine hapa na ni muhimu mno sana,
kuna watu wamenipinga sana lakini ni vile tunatofautiana uelewa tu wa mambo,
mimi nilijua jambo moja hili hapa kwa upande wangu ili niweze kuifanya vyema forex nikuweza kuelewa mfumo mzima ikiwa ni jumla yakujibu maswali yote yasiyokuwa na majibu hii ingenifanya nichezeshe forex kama game tu na ningemake faida kubwa sana.
Hili jambo hapa chini linaweza kukupa mtazamo mpya kabisa katika forex kiasi kwamba ukipata majibu yakukuridhisha basi yawe mwangaza kwako kupata faida ila yasipokupa faida jua hayalingani kabisa.

Fikiria leo USD inathamani ya Tsh.2300/= na wakati huohuo pia Euro Inathamani ya Tsh.2500/= ukiingia katika soko la dunia ama katika mabank yote duniani utakutana na rate ambayo inakwenda sawa kabisa.
Lakini katika forex inakuwa nikwamba thamani ya fedha inaweza panda dakika tano zijazo na dakika 20 zijazo ikashuka na lisaa lijalo mbele ikapanda tena nk japo katika sehemu zile zinazoizungusha hiyo fedha hakuna hata mabadiriko kama hayo.
Sasa jiulize zaidi inakuwaje fedha inayorun katika biashara za ulimwengu ndani ya forex inapata nguvu kuzidi pesa nyingine ila katika uhalisia ukizunguka katika mabank hata ukichungulia soko la dunia haukutani na ushubwada kama huo.

tukutane next episode tena
Mkuu nikujibu kwaufupi tuu...,, mimi naweza sema nimoja ya traders ambao bwana ontario alianza kuutambulisha huu uzi hapa JF, nilifuatilia na kutrade real cash on forex nilichokuja kugundua ni kwamba brokers karibu wote duniani huwa wanaongeza spread katika platform zao ndio maana ukifungua trade inaanza na negative iwe position yoyote either selling au buying, nalapili soko lake huwa halieleweki anaweza akazungumza tajiri mmoja juu ya pair flan akageuza upepo wa soko nzima ukaishia kupata losses za kufa mtu mfano mzuri ni bwana trump one of the big forex trader, mfano mzuri ni bwana waren buffet alivyogeuza soko la BTC likashuka mpaka dolla 3000 toka dola 10000 iliyokuwa awali. Toka kipindi hcho nikajua tuu forex is meant for big traders sio sehemu ya kutoka kimaisha,,,,, ni mara mia ufanye treasury bills au mtu ujifunze madini uweze kuyatambua realness yake na fakeness yake ununue huko weka ndani wait for price iwe kubwa then uza. Na sivinginevyo....,,, au fanya biashara isimamie pesa vzuri, funga mkanda, utatoboa kimaisha lakini cryptocurrecy, forex not for people who are looking for succeess on it. Hayo ni mawazo yangu mkuu
 
"A forex trading is a job not a cassino,a forex trader that approach a forex market as a gambler or addict to money won't get a fortune".
-katika biashara yoyote ile Utafanikiwa mapema Kama utawekeza katika MAARIFA,katika biashara yoyote ile ni vyema TAMAA isizidi JITIHADA.
By NDORANGA
 
Umefunga thread mkuu. Wabongo sijui tutafungua lini vichwa asee yani bado tupo karne ya 19 hahhaa kuna madogo wanapiga mpunga mrefu kwa hizi mambo sasa akiambiwa mambo ya NFT si atakimbilia kijijini.
Karne ya 19 au sio😂
 
Ontario akamatwe afungwe jiwe kubwa sana shingoni atupwe baharin tena katikati ya bahari.. wakat anatupwa baharin apigwe bisibisi ya kichwa.
 
Screenshot_20210901-222619.png

The marathon continues.
 
Ontario akamatwe afungwe jiwe kubwa sana shingoni atupwe baharin tena katikati ya bahari.. wakat anatupwa baharin apigwe bisibisi ya kichwa.
propesa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] afu husemagi n kwann akamatwe
 
Back
Top Bottom