Kama sio utapeli haya niambie Tanzania umesajiliwa wapi?
Duniani kote forex imesajiliwa wapi? ujibu utoe ref za hiyo virtual money sio real money ya cash kupitia bank
Aiseh bado tuna safari ndefu kama nchi...wewe umeshawahi kuona chombo chochote kinacho regulate business dunia nzima? Kuwa tukitaka ku exchange pesa baina ya nchi na nchi lazima twende kwenye hicho chombo cha dunia nzima?
Brokers wako regulated na sheria za nchi husika walikojisajilia. Ila forex ni something global, haina mipaka, haina central authority, ni networks of banks and other players at once. Hauwezi kusema internet ni fake kwa vile haimilikiwi na any central authority.
Bila shaka umeshasikia kuna kitu kinaitwa "soko la dunia" utasikia kuwa mafuta yamepanda bei kwenye soko la dunia...hilo soko la dunia umeshawahi kuliona? Kuwa kuna mahala ukifika unaambiwa hapa ndiyo soko la dunia? Nani ana regulate hilo soko la dunia?
Inatia simanzi kuona kijana anasema forex ni utapeli kwa vile haijasajiliwa popote. Sasa ukisikia kuwa hadi central banks zinafanya Forex si utasema nazo ni matapeli?
Hii suala la virtual money sijui haulielewi kwa nini wakati ni simple concept kabisa..! Kabla hela haijaonekana kwenye account yako ya forex ni lazima udeposit...u-fund hiyo account kupitia njia zinazoruhusiwa..eg bank, Mobile money etc.
Na mtu anapoeda kudeposit maana yake ametoa physical money kampa whoever is concerned na hiyo taasisi ikamuwekea fedha hizo kwenye account yake ya Fx.
So zinapo appear kama virtual money once account ikiwa funded ni kuwa mchakato ulianza na kudeposit kwanza...trader alitoa kiasi fulani kwanza either toka bank account au mobile au njia nyingine akaziweka kwenye forex account.
So hizo unazoziita sijui virtual money...hazitokei tu out of nowhere. Zina backing ya fiat money..tangible money.
Wewe ukiwa na laki 5 kwenye Mpesa yako...hizo si fedha halisi kwa sababu tu hazishikiki? Ukimtumia mtu kutoka kwenye hiyo mpesa kunakuwa na makato ya kodi, service fees za makampuni.
Hizo pesa za makato wahusika wanazipataje kama ni virtual money tu? Maana unapokatwa kodi ya serikali na tozo pindi ufanyapo muhamala hakuna sehemu ambayo serikali inapelekewa ile pesa yake physically...sasa serikali inaipataje hiyo pesa ya tozo? Think critically.
Mtu akikutumia milioni 40 TZS toka akaunti yake kuja kwako....hizo pesa huwa unaletewa physically ndipo tuseme ni real money? Elewa kuwa money inaweza kuwa transferred electronically na bado ikabaki kuwa ni ile ile.
So hizo fedha zote unazoziona kwenye forex market zilianza na mchakato wa kuwa funded kwenye accounts za wahusika. Ni sawa na wewe uende bank kwa teller u deposit pesa...anaingia kwenye account yako ambayo ni virtual anaongeza kiasi ulichoweka na kukupa print out slip kama ushahidi wa kuhifadhi fedha. Ila pesa zenu wateja wote zinahifadhiwa sehemu moja. So ushahidi unaoonesha kuwa wewe una kiasi fulani cha fedha bank ni electronic si physical.
Hicho unachokidharau na kukibeza kama virtual money ndiyo kimewapa watu ukwasi. Hisa zinashikika? Ni tangible? Ila si zinauzwa na kununuliwa? Majuzi hapa Gamestop imewafanya traders kuwa overnight millionaires kwa ku trade hisa tu...kuna kijana alinunua hisa hizo kwa 28,000$ zilipopanda thamani akawa na $3.8 M sitting on his account. Ni virtual na ni halisi pia...anaweza kuzi withdraw akazifanyia chochote akitakacho.
[/QUOTE]
Mkuu unamoyo kumuelezea yote haya mi nishamaliza kumuita Bata tu inatosha mtu anafanya forex halafu hata hajui kuwa brokers wanaleseni..🤣
Huyu usikute hata alichagua broker wa hovyo!.