Kilichonikuta usiku wa leo, ila bado sijakoma...nitarudia tena

Kilichonikuta usiku wa leo, ila bado sijakoma...nitarudia tena

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,288
Reaction score
18,579
Usiku wa leo mida kama ya saa 10 hivi nikiwa zangu ndotoni, ufahamu wangu ulirudi hivyo nikawa najitambua kuwa naota (lucid dreaming). Basi bwana nikaanza kuipeleka ndoto vile ninavyotaka mimi. Shukrani kwa jf maana kupitia hapa ndipo nilijifunza haya mambo ya lucid dreaming japokuwa siyafanyii kazi sana ila huwa nikipata nafasi siiachi.

Basi bwana, nikaendelea kuota huku nikiwa najitambua kuwa naota na nikawa naiendesha ndoto iwe vile ninavyotaka. Ghafla nikapata wazo huko huko ndotoni kuwa, kama naota na najitambua kuwa naota, kwa nini nisitumie muda huu kufanya tahajudi (meditation) kwa kuwa ubongo na mwili wangu kwa sasa vimetulia kwa kiwango kikubwa.. Basi nikiwa hukohuko ndotoni, nikatulia na nikaanza kutamka maneno ambayo huwa napenda kuyatamka nikiwa nafanya tahajudi.

Balaa likaanzia hapo...

Ile kutamka sentensi ya kwanza tu, nilihisi kupata utulivu wa ajabu sana hadi nikashangaa. Then nikaanza kuhisi kama napigwa shoti ya umeme ndani ya kichwa kwenye ubongo humo ndani huko then hiyo shoti kaanza kusambaa kwa kushuka kwenda kifuani na kuanza kwenda sehemu nyingine za mwili. Ile hali ikaanza kunitisha, nikapata wazo kuwa huenda ni mwili unatengana na roho kwa ajili ya astral projection au ndo nakufa hivyo😀😀😀

Kwa kweli ndugu wajumbe sikutaka kusubiri kuona nini kinaendelea, ikabidi nijitikise huko huko ndotoni ile hali ikaondoka. Hata mpango wa kuendelea na lucid dreaming nikaona haufai kabisa ikabidi niamke tu.

Sasa baada ya kuamka nimejikuta nataka kujua vingi zaidi. Je, ile hali imetokea kwa bahati mbaya au ndivyo ilivyo mara zote? Kama ndivyo ilivyo mara zote, ni nini kinatokea kama ile shoti ikisambaa mwili mzima?

Majibu ya maswali haya nitayapata kwa kufanya hili jambo tena, hivyo nimepanga kurudi huu mchakato kwa mara nyingine na mara hii kama hiyo hali ikitokea tena basi nitakomaa hadi mwisho nione nini kitatolea.
 
Wee umechapwa na ule ubaridi wa alfajiri ukijumlisha mawazo ya kipato ndio kabisaa akili imehama. Ndoto ya kweli ikikujia asubuhi hata ufanyeje huikumbuki.
Mkuu, ina maana wewe hujawahi kupitia hali ya kuwa nusu umelala na nusu uko macho?

Wataalamu wanasema hii hali hutokea pale usingizi ukiwa hatua ya REM (Rapid Eye Movement). Sijasoma science ila wenye dunia ndo wanasema hivyo.

Mimi mara nyingi huwa naipata kuanzia saa 9-12.

Unakosa moja ya starehe tamu sana mkuu.
 
Either ulilala vibaya su ulikula chakula kigumu kikaupa mwili shida ya kukimeng"enya ndio maana ukaota hayo.
Au vyote kwa pamoja😉
Chakula kigumu; hapana, kulala vibaya; labda.

Ila hiyo hali ya kupata ufahamu nikiwa usingizini na kujitambua kuwa hapa naota ni hali ya kawaida sana kwangu, nimeshazoea. Sema leo nikataka kupiga hatua moja mbele.
 
Mkuu, ina maana wewe hujawahi kupitia hali ya kuwa nusu umelala na nusu uko macho?

Wataalamu wanasema hii hali hutokea pale usingizi ukiwa hatua ya REM (Rapid Eye Movement). Sijasoma science ila wenye dunia ndo wanasema hivyo.

Mimi mara nyingi huwa naipata kuanzia saa 9-12.

Unakosa moja ya starehe tamu sana mkuu.
Hiyo ndio ndoto mawazo inaitwa yaani hiyo ni ndoto arinacha sasa..
Ndoto ya ukweli ukweli ile ambayo inakupeleka mbali huko ukiiota akija kufika asubuhi hata uifikirie vipi huikumbuki hata iweje.
Hiyo yenu naotaga sana lakini sinaga time nayo maana niya uongo uliotukuka[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inataka kufanana na incidence yangu nilipovuta bangi kwa mara ya kwanza. Ni mbali basiii? mwezi jana tu.

Anyways, kuvuta bhangi kumejifanya nijitambue na kutambua vitu ambavyo vingenichukua miaka au nisingevijua
 
Nafahamu stimu za mjani zinavopelekesha ubongo, Badilisha muda wa kupiga kitu, usipige kabla hujalala. Siku nyingine utasukuma kitanda hadi sebuleni! [emoji16]
 
Inataka kufanana na incidence yangu nilipovuta bangi kwa mara ya kwanza. Ni mbali basiii? mwezi jana tu.

Anyways, kuvuta bhangi kumejifanya nijitambue na kutambua vitu ambavyo vingenichukua miaka au nisingevijua
Watu kama niny ndo huwa mnafanya nitamani kujaribu hii kitu...😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom