Kilichonipa huzuni kuu kwenye iftari ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Bwana Makonda

Basi futari hiyo imewafikia walengwa, ukitaka kufuturisha ita wenye uhitaji siyo unaandaa invitation card unaalika watu maarufu na wenye uwezo ili kutengeneza attention huku wenye uhitaji unawazuilia getini

kuna watu hata mlo mmoja hawawezi hawapati ni vyema futari hiyo ikawafikia wao kama ilivyo mafunzo na lengo sahihi la kufuturisha.
 
Bado hujahuzunika kisawasawa, nikuhuzunishe zaidi kwa kukujuza kuwa hiyo futari waliyobeba kwenye suruali ni sababu tosha ya wao kuimwagia kura sisiem october, tena kwa nderemo na vifijo kuwa hakuna kama sisiem! Na hata hapo Kuna waliokuja na t-shirts na kofia zao za sisiem zilizojichokea wakidhani ndio njia rahisi ya kufurahiwa na kupendelewa kwa kupakuliwa futari nyingi.

Kipindi cha nyuma nilikuwa na huruma na watu wenye maisha magumu (nami na ukoo wangu wote tukiwemo) hadi nilipobaini kuwa % kubwa hali hiyo wanaipenda wenyewe na hawataki kubadilika.
 
Siku hizi mtu ataandaa sherehe/hafla kwa pesa za walipakodi ili asishtukiwe analenga mrengo wa kidini kujipatia ushawishi wa kisiasa.
 
Sijaambiwa nimejifunza hivyo tangu mdogo.
Iftar ndo neno la asili , futari ni kutohoa tu kutoa kwenye kiarabu, ila akisema Iftar yuko sahihi maaana yake ni mlo wa kufungua funga baada ya jua kuzama
 
Serikali inapaswa iwe na mpango wa kudhibiti ongezeko la idadi ya watu kwa kasi.
 
Je nini kifanyike kusaidia wanaotaabika.?
Jambo la kwanza wajitambue na wajifunze kuiwajibisha serikali yao inapofanya ujinga ili ibadilike na kufanya mambo ya maana yatakayowakwamua.

Ofisi ya umma inaandaa futari kwa mamilioni ya fedha za umma kwa lengo la kupaisha jina la mtu mmoja kisiasa, wao wanachokifikiria ni kutembea kilomita 10 kwenda kubugia futari!

Fedha za umma zinanunua magoli ya Simba na Yanga wao wanachoweza kufanya ni kutambiana na kubishana vijiweni upande upi unayachuma mamilioni hayo kuliko upande mwingine. Humsikii yeyote akikosoa matumizi ya namna hiyo.
 
Serikali ingejikita zaidi kutoa huduma Bora na kutengeneza mazingira wezeshi ya watu kufaidika na rasilimali zao hii ingesaidia watu kujikwamua na kuinua vipato vyao
 
Iftar ndo neno la asili , futari ni kutohoa tu kutoa kwenye kiarabu, ila akisema Iftar yuko sahihi maaana yake ni mlo wa kufungua funga baada ya jua kuzama
Sasa mleta mada hapa katumia lugha gani kuwasilisha hoja yake kiswahili au kiarabu?!
 
Serikali inapaswa iwe na mpango wa kudhibiti ongezeko la idadi ya watu kwa kasi.
Siku hizi nafikiri watu wengi wamejiongeza wenyewe kuzaa Kwa mpango kutokana na elimu mbali mbali na hali halisi ya maisha
 
Mkuu tabia ya kubeba vyakula ni ya Nchi nzima hii ishazoeleka miaka miaka Mimi nilikuwa nashuhudia mama akirudi na maandazi Kila alienda harusini!!

Siyo kwamba home tulikuwa na njaa la hasha siyo hivyo ni tabia kabisa ....
Nenda kwenye maharusi yanafanyika kwenye ukumbi wa kawaida isipokuwa na walinzi kuwa kuingia Hadi uwe na kadi utaona haya wamama wakibeba chakula kupeleka makwao.


Nina uhakika walio chukua ni wachache sana ambao kwao hapakuwa na chochote kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…