Kilichonipa huzuni kuu kwenye iftari ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Bwana Makonda

Utafiti wako upo shihi kabisa, na hiyo ndiyo hali halisi ya wananchi wengi. Ukichunguza hali za wananchi mmoja mmoja ni ngumu sana tofauti na ukuaji wa uchumi wa nchi. Nadhani viongozi wangetumia fursa ya Iftari kupata tathmini ya uwezo wa wananchi kumudu mlo angalau mmoja katika kaya. Labda iandaliwe iftari hapo Benjamini Mkapa na waalikwa wawe wananchi wa kawaida....!
 
Hizo ndizo hali zetu mi kwa mtazamo wangu serikali kuanzia kwa balozi wa shina wangeweka utaratibu mzuri jinsi ya kusaidia makundi ya watu lakini kingine hao nao ukifika wakati wa uchaguzi badala waweke mtu anae wajali wao wameweka mbele ushabiki wa kisiasa wanasahau kabisa hali walizo nazo
 
Hii ndiyo inaitwa ''mtupie mbwa mifupa ili asiwabughudhi wakati mnakula''. Makonda anatumia umaskini wa watu ambao umetokana na uongozi mbovu wa CCM, kuwalaghai watu kwa chakula ili wasikumbuke kuhoji ufisadi na kutowajibika kwa serikali. Wataendelea kutupiwa kama mbwa mpaka lini? Wakiamka kesho, wanasema afadhali ya juzi.
 
Hamna masikini wa Tanzania kwasasa ninayemuonea huruma, hao ndio wakata mauno kwenye shughuli za watawala. Wameamua kuwa kenge ngoja wasubiri damu ziwatoke ndio watagundua umasikini wao ni wakujitakia.
 
Mtu aliyepika vyakula vya aina aina nyumbani anaanzaje kubeba maandazi kwenye tukio! Hakika ni umasikini tu
Kwanza ukiwa mstaarabu hata kama nyumbani kwako huna hivyo vyakula huwezi kubeba. Sasa mtu katoka kwake kajiandaa kabisa kabeba na bakuli๐Ÿ˜…
 
Kama ameamua kuwapa chakula wahitaji kwanini ajifiche kwenye hilo neno futari? Huyo ana malengo yake ya kisiasa.
 
Serikali ianzishe mfuko wa jamii kusaidia kaya masikini kama wanavyofanya baadhi ya mataifa hasa barani Ulaya na baadhi ya mataifa ya kiarabu.
Mfuko huo ugharamie posho inayotosheleza mahitaji ya chakula ya familia kila siku.
Ili muendelee kuzipiga majuu huko๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ