Kilichonipa huzuni kuu kwenye iftari ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Bwana Makonda

Acha uzushi na chuki. Kwahiyo kama siyo hiyo siku moja wangekufa kwa njaa? Na vipi baada ya kula si hadi mwakani tena kwahiyo kuna watu wanaenda kupoteza maisha kwaajili hawana chakula?
 
Hii hali nimeikuta juzi hapa Dar maeneo ya posta kuna jamaa walikuwa wanajadiliana kwani wanataka kwenda kwa familia inayofutulisha ila sasa kuna moja hairuhusu kubeba chakula ila ina chakula kingi. Familia nyingine inaruhusu kubeba ila inatoa zaidi mikate na vitafunwa vingine ... sikusikiliza sana mjadala jamaa wakaondoka eneo langu ni kama walihisi nawasikiliza ila iliniumiza nikatamani kuwaachia hela kidogo na roho nyingine ikawaza mambo ya chuma ulete nikasepa zangu.
 
Watu wasizae kabla hawajajipanga eti maana ccm haiwezi saidia watu wote jua kuwa tanzania inawatu wengi
 
Acha uzushi na chuki. Kwahiyo kama siyo hiyo siku moja wangekufa kwa njaa? Na vipi baada ya kula si hadi mwakani tena kwahiyo kuna watu wanaenda kupoteza maisha kwaajili hawana chakula?
Daah ndugu umesoma jamaa ameandika nini mbona hakuna mahali ameonyesha chuki kwa mtu wala taasisi yeyote ile.
 
Wengi wanafikiria ni utani eti
 
Ukweli ni kwamba nchi yetu ni masikini sanaa yaan sanaaa, ila hatuna la kufanya maana ndo nchi wameshajikabidhi na kuidhibiti watu wasio na uwezo wa kusogeza popoye zaidi, zaidi ya asilimia 90 ya watanzania ni masikini zaidi asilimia 70 ni ombaomba, prove me wrong. Ndio maana CCM haitakaa ikubali nchi hii iwe na uchaguzi huru na kuitoa madarakani ni lazima patachafuka kwanza humu.
 
Serikali ianzishe mfuko wa jamii kusaidia kaya masikini kama wanavyofanya baadhi ya mataifa hasa barani Ulaya na baadhi ya mataifa ya kiarabu.
Mfuko huo ugharamie posho inayotosheleza mahitaji ya chakula ya familia kila siku.
Huo mfuko Hadi uwepo Hadi itokee misaada Toka nje Kwa ajili hiyo vinginevo tusahau
 
MashaAllah=Maisharaha.
 
Umeongea ukweli mtupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…