Kilichonitokea kituo cha Daraja la Salenda baada ya kushuka kwenye daladala saa nne usiku

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Nakumbuka nikitokea maeneo ya Slipway baada ya boss wangu kunipa laki moja nikatafute samaki,

Nikaenda msasani nikakosa hivo nikaona niende feri, nikapanda gari la kwenda Kariakoo tulipokaribia Salender nikamwomba konda anishushe hapo, konda kwa mshtuko, unasema?

Nikamwambia tena nishushe Sarenda muda huo ni saa 4 usiku basi bhana kama unavojua kuna watu hawapendi fuatilia mambo ya watu gari ikasimama nikashuka

Mbele yangu kulikuwa na gari moja ndogo imesimama halafu but I la mbele limenyanyuliwa nahisi ilipata hitilafu, nyuma kulikuwa na trafiki anaelekeza magari ile njia ya kwenda Coco beach, njia ya kutokea Coco nikaona vijana kama sita hivi muda huo wote yaani ni kama dk 10 zimepita toka nishuke ila kila gari ninalolisimamisha la kwenda Posta kutoka Makumbusho hayasimami yaana yanapita na mia

Sasa wale jamaa walikuwa na vifaa vikubwa balaa nikafikiri ni wanamazoezi, nikafikiri kujiunga nao ili nivuke pale darajani

Bado nawaza haijaisha sekunde kumi naona wameanzisha timbwili kwenye gari lile lililokuwa limepaki hapo mbele, kulikuwa na vijana wawili, kama sio waarabu basi ni wahindi, mara jamaa wakafungua milango muda huo hawa jamaa wenye gari wamekimbia mmoja anaelekea kwa askari anayeongoza magari hapo njia ya Coco beach mwingine anakimbia huko upande wa Pili wa barabara

Sikumbuki nini kilitokea ila nilijikuta ile njia ya Muhimbili nipo kwenye kituo karibu na chuo sijui ndo Mzumbe nasubiri gari ya kutoka Kariakoo nirudi Masaki
 
Uandishi wa hovyo ambao mtu mzima hapaswi kuandika.

"sikumbuki nini kilitokea ila nilijikuta ile njia ya muhimbili nipo kwenye kituo karibu na chuo sijui ndo mzumbe nasubiri gari ya kutoka kariakoo nirudi masaki"

Kichwa cha Habari:

"kilichonitokea jituo cha daraja la salenda baada ya kushuka kwenye dala dala saa nne usiku"​


Swali:

Ni nini kilikutokea?
 
Ilikua lini mkuu? Maana last week nilikodi bajaji usiku ilizimika pale darajani kwa nyuma kidogo,ilikua usiku saa nane panatisha sana na magari hayasimami yanapita nduki balaa.

Tukaamua kuisukuma mpaka pale kituo cha polisi, tukapaki na dereva kuanza kuitengeneza. Nadhani vibaka wa pale wanaangalia na mtu wa kumvamia, hasa wanavamia wenye magari na wanaopita mtu moja mmoja mkuu
 
Saa nne usiku trafiki huyo anaongoza magari ya vibwengo.
Wanakuepo pale nje ya kituo na wanafanya doria mpaka kule darajani.Sio trafic ni asikari maalumu wa kikosi kazi cha doria sometimes waga wanajificha kwenye vile vichaka vya mianzi upande ule usio wa baharini kuvizia wahalifu na magari wanayoyatilia mashaka usiku.
 
ndo maana nikasema sijui ila ni chuo pale kuna kipindi konda wa daladala aliwahi dungwa kisu na mwanafunzi hapo ndo maana nakikumbuka ila jina ndo silikumbuki la chuo
Kipo mkuu hapo upanga.Hv ndio hapo yule mbabe wa tambaza alipomuua konda???
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…