Kilichonitokea kituo cha Daraja la Salenda baada ya kushuka kwenye daladala saa nne usiku

Kilichonitokea kituo cha Daraja la Salenda baada ya kushuka kwenye daladala saa nne usiku

Okay napitaga sana hapo makaburini... Zaman wakati bwana mkubwa yupo pale sarenda hata saivi kuna manjagu....
Mkuu wapo manjagu ila mda mwingi wamevaa kiraia wanapiga round.Na mle ndani vichakani kwenye njia ya mto msimbazi mpaka kule nyuma kwa marehemu mzee mengi na ubalozi wa kenya,kwenye njia yote ya mto msimbazi na lile tawi la kutokea muhimbili kumejaa matope kama sio kibaka mzoefu huwezi kukimbilia kule,utazama na kufa.Vibaka wastaafu ukikaa nao wanakupa details zote pale kwenye kituo cha daladala cha kinondoni makaburini.
 
Ndiyo maana konda alikushangaa hicho si kituo cha kushuka giza likiingiaa tu wachilia mbali saa nne usiku
 
Nakumbuka nikitokea maeneo ya Slipway baada ya boss wangu kunipa laki moja nikatafute samaki,

Nikaenda msasani nikakosa hivo nikaona niende feri, nikapanda gari la kwenda Kariakoo tulipokaribia Salender nikamwomba konda anishushe hapo, konda kwa mshtuko, unasema?

Nikamwambia tena nishushe Sarenda muda huo ni saa 4 usiku basi bhana kama unavojua kuna watu hawapendi fuatilia mambo ya watu gari ikasimama nikashuka

Mbele yangu kulikuwa na gari moja ndogo imesimama halafu but I la mbele limenyanyuliwa nahisi ilipata hitilafu, nyuma kulikuwa na trafiki anaelekeza magari ile njia ya kwenda Coco beach, njia ya kutokea Coco nikaona vijana kama sita hivi muda huo wote yaani ni kama dk 10 zimepita toka nishuke ila kila gari ninalolisimamisha la kwenda Posta kutoka Makumbusho hayasimami yaana yanapita na mia

Sasa wale jamaa walikuwa na vifaa vikubwa balaa nikafikiri ni wanamazoezi, nikafikiri kujiunga nao ili nivuke pale darajani

Bado nawaza haijaisha sekunde kumi naona wameanzisha timbwili kwenye gari lile lililokuwa limepaki hapo mbele, kulikuwa na vijana wawili, kama sio waarabu basi ni wahindi, mara jamaa wakafungua milango muda huo hawa jamaa wenye gari wamekimbia mmoja anaelekea kwa askari anayeongoza magari hapo njia ya Coco beach mwingine anakimbia huko upande wa Pili wa barabara

Sikumbuki nini kilitokea ila nilijikuta ile njia ya Muhimbili nipo kwenye kituo karibu na chuo sijui ndo Mzumbe nasubiri gari ya kutoka Kariakoo nirudi Masaki
Mkuu ni tukio la siku nyingi au la hivi karibuni.
 
Back
Top Bottom