Kilichopo nyuma ya mzozo wa Niger vs ECOWAS, EU na Nigeria

Hivi nikwanini
Sababu kubwa mbili
-Uranium (Marekani na EU ndio wanufaika wakuu wa uranium ya Niger ,sasa Serikali mpya imefunga uuzwaji wa uranium kwa Marekani na ulaya)

-Trans Saharan Gas Pipeline, ni mradi wa kutoa gasi Nigeria to Europe kama sehemu ya kutafuta mbadala wa gesi ya Russia, Niger ni sehemu ya mradi huo (kupitisha bomba).

Hivi vitu viwili vimewaumiza sana na ubaya zaidi Urusi imeonekana kuinga mkono na Nina wasi wasi hata haya mapinduzi yameratibiwa na Putin

Nigeria yeye amekasirika kwasababu amepotezewa ugali wake wa kuwauzia gesi ulaya, EU nao kama mradi usipo fanyika utawafanya kuwa tegemezi na gesi ya mrusi (Hawana mbadala) , Marekani anataka kumualibia Urusi na kuwasaidia rafiki zake EU
 

Russia alishatibua Syria kupita kwa Bomba kutoka Qatar acha tuone hapa Niger EU nyuma ya mgongo wa ECOWAS watafanya nini.
 
Umeliweka vizuri sana, kazi ipo
 
Hapo bado hujagusia umuhimu wa Niger katika kuzalisha madini ya Uranium duniani, na umuhimu wa Uranium katika kutengeneza nishati na mabomu ya nyuklia.
 
hakuna Vita itakayopiganwa , Mali, Niger na bukinafaso wamekubaliana kuungana kijeshi endapo ECOWAS watafanya uvamizi , piga hesabu nchi 3 zikiungana kijeshi hiyo Vita yake itasambaa na kuwa Vita kubwa , halafu hapo hapo Russia na marafiki zake lazima watawasaidia niger ,nigeria anaweza kujikuta anapigwa nje ndani , bokoharam nao watapata mwanya wa kuanzisha Vita Nigeria .
 
Hata kule Misri alipopinduliwa Morsi hawakupeleka vikosi, je na Misri naye hakuwa na cha kutoa ?
Misri ana kitu gani cha maana zaidi ya kuwa strategic area?
Lakini pia, kwanini mapinduzi ya Misri yameefadhiliwa na kuratibiwa na West. Kwahiyo, USA & Co hakuwa na sababu ya kufanya hiki anachokifanya pale Niger. Tatu na mwisho, Russia hakua na interest pale Misri, so hakuona umuhimu wa kupeleka kuingilia mzozo huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…