Uchaguzi 2020 Kilimanjaro, Mwanga: Henry Kilewo amuwekea pingamizi Mgombea Ubunge wa CCM Joseph Tadayo kwa vile hakusaini sehemu "E"

Uchaguzi 2020 Kilimanjaro, Mwanga: Henry Kilewo amuwekea pingamizi Mgombea Ubunge wa CCM Joseph Tadayo kwa vile hakusaini sehemu "E"

Lawama zielekezwe kwa Mhe. Hakimu aliyemgongea muhuri na yeye kuweka saini yake. Kwanza angemuomba mgombea kwanza kuweka sahihi yake. sijui hapo atajitetea vipi.

Iko hivi mkuu, hawa jamaa wanapita kwa hakimu anasaini na kugonga mihuri kwanza!![emoji23][emoji23]
 
Mambo yanachekesha haya yaani naona utoto mwingi balaa
 
Yote hii ni matokeo ya kuzidisha unafiki na sheria nyingi sana

Hata wana wa Israeli yaliwakuta kwa kujaza sheria nyiingi matokeo yake hata kwao wenyewe zikawa nzito mno.
Haya ninayoyaona hapa yanathibitisha hilo
 
Hii ndio habari mpya iliyotufikia kwa sasa , Kwamba Sehemu " E " inahusu Tamko la kisheria la Mgombea Ubunge , na kwa vile Tadayo hakuisaini maana yake ni kwamba ameshindwa kuthibitisha kuwa anazo sifa za kugombea ubunge kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa 2020 , sehemu "E" haikuwekwa kwenye fomu kama mapambo , ilipaswa kujazwa .

View attachment 1548954

..na Joseph Tadayo ni mwanasheria lakini amefanya kosa ktk kujaza fomu.

..wengine tulishauri kwamba wasimamizi wawe facilitators wa wagombea kushiriki uchaguzi, na kamwe wasiwe kikwazo kwa wagombea.

..kama mgombea anazo sifa, na ameteuliwa na chama chake, hakuna sababu za msingi za kumkwamisha ktk kugombea.

..Tume inatakiwa iyapige stop mapingamizi, na badala yake ibakie na zile sifa za KIKATIBA tu ktk kupitisha wagombea.
 
"Haloo upo wapi ,njoo saini kimeo chako huku,usituletee shida bhana" alisikika msimamizi wa uchaguzi akimpigia simu mgombea Huyo wa ccm mwanga jana usiku saa 2
 
Lawama zielekezwe kwa Mhe. Hakimu aliyemgongea muhuri na yeye kuweka saini yake. Kwanza angemuomba mgombea kwanza kuweka sahihi yake. sijui hapo atajitetea vipi.
Huwa hawasomi na kukagua,wao wanatafuta mahali anapotakiwa kuandika saini yake kwisha.
 
Hii ndio habari mpya iliyotufikia kwa sasa , Kwamba Sehemu " E " inahusu Tamko la kisheria la Mgombea Ubunge , na kwa vile Tadayo hakuisaini maana yake ni kwamba ameshindwa kuthibitisha kuwa anazo sifa za kugombea ubunge kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa 2020 , sehemu "E" haikuwekwa kwenye fomu kama mapambo , ilipaswa kujazwa .

View attachment 1548954
Kwa jinsi hii hata za wale watakatifu waliopitishwa pasi kupingwa zikaguliwe tu tuzidi kuona viroja!!
 
Lawama zielekezwe kwa Mhe. Hakimu aliyemgongea muhuri na yeye kuweka saini yake. Kwanza angemuomba mgombea kwanza kuweka sahihi yake. sijui hapo atajitetea vipi.
Usikute ilipelekwa na kiongozi wa chama kwa maelekezo na si mhusika.
Nakumbukia "uchafuzi SM - Tuna wanasheria nchi nzima!!!"
Tunakoelekea sijui...
 
Hao wagombea 18 waliopitishwa baada ya wapinzani wao kuondolewa ndio ilikuwa hivi wasimamizi walikuwa wanakagua mapungufu ya fomu za wagombea wapinzani wa ccm tu
Ni vyema Sasa fomu za hata akina kabudi , nape, abood, ndugai, ndejembi, mavunde, na wengine waliojitapa tayari kupitishwa zikaguliwe zinaweza kuwa na makosa kibao
Like son like father
 
Tutaelewana tu, ngoja tuonyeshane makali.
Naaaam. Sheria walitunga CCM wenyewe acha sasa ziwarudi.

Those days wanaambiwa haya mambo mengine ni ‘madogo’ na yanarekebishika (mfano kumuita tena mtu apige saini kama alisahau..) ila wao walishupaza shingo

Kama kuna wagombea wa CHADEMA wamekatwa kwa “kusahau” kubandika picha, huyu nae aliyesahau kusaini atupwe nje. Hata yule aliyeandika majina manne akijiita Askofu nae atupwe nje kabisa. Tutaelewana tu.
 
Huyo amekosa sifa za kuwa Mgombea kwa sababu bila hiyo TAMKO unakuwa huna sifa hata moja, hiyo ni hasara kubwa sana kwa Chama chetu na hakuna namna nyingine kwani fomu ingetokaje kwake kwenda kwa mpinzani wake? Hii ni technical knock out-KO
 
Mbona kujaza fomu imekuwa ishu sana. Hv mtu akapeleka hiyo fomu hata kunakitu kasahau haiwezekani akaambiwa rekebisha kipengele flani afu uilete upya? Tume inapaswa kurekebisha haya Mambo.
Unadhani huko unakosikia wabunge wa CCM wamepita bila kupingwa kuna nini vimetokea?? Ni vitu vidogovidogo kama hivyo. Pia kitendo cha mtu kukamatwa na vyombo vya dola siku ya kurejesha form kwa tuhuma za uraia au rushwa na hivyo akashindwa kurejesha, unalionaje? Haya yasingeweza kusubiri arejeshe kwanza???
 
Hii ndio habari mpya iliyotufikia kwa sasa , Kwamba Sehemu " E " inahusu Tamko la kisheria la Mgombea Ubunge , na kwa vile Tadayo hakuisaini maana yake ni kwamba ameshindwa kuthibitisha kuwa anazo sifa za kugombea ubunge kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa 2020 , sehemu "E" haikuwekwa kwenye fomu kama mapambo , ilipaswa kujazwa .

View attachment 1548954
Huyu apigwe chini! Bila uhuni wala nongwa!
 
Huyo amekosa sifa za kuwa Mgombea kwa sababu bila hiyo TAMKO unakuwa huna sifa hata moja, hiyo ni hasara kubwa sana kwa Chama chetu na hakuna namna nyingine kwani fomu ingetokaje kwake kwenda kwa mpinzani wake? Hii ni technical knock out-KO

..jamani Joseph Tadayo amegombea nadhani mara 3 dhidi ya Prof.Jumanne Maghembe.

..sasa safari hii amepenya, then mnataka akatwe kwa makosa madogo-madogo kama hili?

..ndiyo maana nasisitiza wasimamizi na tume wawe WAWEZESHAJI wa wenye nia ya kugombea, kamwe wasiwe kikwazo kwa wenye nia za kugombea nafasi mbalimbali.

cc Kilatha, johnthebaptist , tindo
 
Back
Top Bottom