Kilimanjaro: Walimu wauza Rasilimali zao kupata pesa za uhamisho

Walimu zaidi ya 50 kutoka Katika shule za msingi zipatazo 46 katika Tarafa mbali mbali wilayani Rombo,mkoani Kilimanjaro wamelazimika kuuza Rasilimali zao kama vile mbuzi,kuku na baadhi ya vitu vya ndani na wengine kuingia kwenye mikopo ili kuweza kupata pesa Kwa ajili ya kujihamisha wao pamoja na familia zao baada ya kupata barua za uhamisho na kutakiwa kwenda kuripoti katika vituo vingine vya kazi.

Walimu hao wamedai ya kuwa walipata barua za uhamisho na kutakiwa kuripoti Katika vituo vyao vip ya vya kazi mnamo tarehe 8 mwezi wa pili (2)mwaka huu lakini baada ya kuripoti kazini waliahidiwa kulipwa stahiki za uhamisho mapema iwezakanavyo lakini Hadi sasa ni miezi Minne (4) imeisha Bila kupata chochote.

Baadhi ya shule hizo ni pamoja na shule ya msingi Urauri, Mashima, Kafumbu, kibaoni, Nanjara,na Samanga.

Baadhi ya Walimu hao ambao hawakupenda kutaja majina yao wamedai Kuwa malalamiko yao tayari walikwisha peleka Kwa Afisa Utumishi,Afisa elimu pamoja na mkurugenzi.

Lakini Majibu wanayopewa Kila wakati hayaridhishi Kwa kuambiwa Kuwa mfumo Unasumbua ndo maana pesa haijatoka.

Walimu hao wamedai Kufanya kazi katika mazingira Magumu kutokana na kuwa madeni mengi.
Wanehanishwa au wamejihamisha kwa kubadilishana vituo na walimu wenzao?
 
Sidhani kama ni wapenzi wa hiari wa ccm bali wanalazimika kuwa hivyo.
Waalimu wamefanywa masikini na serikali ya CCM kwa kulipwa masilahi kidogo ili waishi kwa kutegemea hisani ya serikali.

Kwa hali hiyo serikali inawatumia kama misukule huku ikiwapa bakshishi kidogo, walimu nao wanashangilia kama mazuzu kwa vile hawana jinsi.

Wakulaumiwa sana hapa ni hivyo vyama vyao kwa kushindwa kabisa kumtetea mwalimu.
Wataombewa dua mbaya kila siku kwa uonevu wanaowafanyia wafanyakazi
 
Walimu zaidi ya 50 kutoka Katika shule za msingi zipatazo 46 katika Tarafa mbali mbali wilayani Rombo,mkoani Kilimanjaro wamelazimika kuuza Rasilimali zao kama vile mbuzi,kuku na baadhi ya vitu vya ndani na wengine kuingia kwenye mikopo ili kuweza kupata pesa Kwa ajili ya kujihamisha wao pamoja na familia zao baada ya kupata barua za uhamisho na kutakiwa kwenda kuripoti katika vituo vingine vya kazi.

Walimu hao wamedai ya kuwa walipata barua za uhamisho na kutakiwa kuripoti Katika vituo vyao vip ya vya kazi mnamo tarehe 8 mwezi wa pili (2)mwaka huu lakini baada ya kuripoti kazini waliahidiwa kulipwa stahiki za uhamisho mapema iwezakanavyo lakini Hadi sasa ni miezi Minne (4) imeisha Bila kupata chochote.

Baadhi ya shule hizo ni pamoja na shule ya msingi Urauri, Mashima, Kafumbu, kibaoni, Nanjara,na Samanga.

Baadhi ya Walimu hao ambao hawakupenda kutaja majina yao wamedai Kuwa malalamiko yao tayari walikwisha peleka Kwa Afisa Utumishi,Afisa elimu pamoja na mkurugenzi.

Lakini Majibu wanayopewa Kila wakati hayaridhishi Kwa kuambiwa Kuwa mfumo Unasumbua ndo maana pesa haijatoka.

Walimu hao wamedai Kufanya kazi katika mazingira Magumu kutokana na kuwa madeni mengi.
Kwani hakuna CWT hapo
 
Afisa elimu msingi rombo hafai kabisa kwenye nafasi hiyo ni mwanamke mnyama sana, anazuia watu wasihamie rombo na wanaotaka kuhama hapitishi barua zao!
 
Hata wilaya ya moshi dc tatizo hilo lipo walimu wamehamishiwa shule mpya tokea mwezi wa april hadi keo mfumo mfumo na walimu wanajipigia kazi kama kawaida ila stahiki holaaa...serikali inawazaga nini sijui.?inasikitishq sana
 
Back
Top Bottom