Kilimanjaro: Waliohusishwa na utekaji wa watu na kujitambulisha kama Usalama wa Taifa watiwa mbaroni

Kilimanjaro: Waliohusishwa na utekaji wa watu na kujitambulisha kama Usalama wa Taifa watiwa mbaroni

Watu watatu waliokuwa wakimfuatilia mgombea ubunge jimbo la Vunjo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Ndg. James Mbatia wakiwa na gari aina ya Toyota Prado namba DFP 788 wamekamatwa na Jeshi la Polisi mjini Moshi jana saa 10 alasiri eneo la KDC baada ya Polisi kufukuzana na gari hilo na kufanikiwa kulidhibiti (block).

Mmoja wao alifanikiwa kukimbia baada ya kuona wamedhibitiwa lakini wawili walidhibitiwa na Jeshi la P

Watu hao waliokuwa wakijitambulisha maeneo mengi kuwa wao ni Usalama wa Taifa na wakati mwingine wakidai wao Askari wa Jeshi la Polisi hatimaye baada ya kukamatwa na kuhojiwa imedaiwa ni watu kutoka kitengo cha ‘Maadili na Usalama’ ndani ya CCM kutoka ofisi ndogo ya CCM Lumumba.

Baada ya kupekuliwa, watu hao walikutwa na nambari za magari tofauti tofauti na silaha mbalimbali zikiwamo koleo zinazodaiwa kutumika kuwatesa makada wa upinzani waliotekwa Vunjo na Moshi Vijijini na kuzua taharuki mkoani Kilimanjaro.

Wanaendelea kushikiliwa Central Police mjini Moshi.

View attachment 1599427
Hawa ndio walioweza kukamatwa

View attachment 1599428
Hizi ni nambari za magari zilizokutwa ndani ya gari lao

Mbatia akiongelea vitendo hivi 👇🏾

View attachment 1599436


Ilivyotokea: Mnamo majira ya saa 10 za jioni kulitoka kurupushani katika ya msafara wa James Mbatia pamoja na watu waliokuwa na gari hilo hali iliyozua taharuki kubwa. Nguvu ya ziada iliongezwa na Jeshi la Polisi kituo kidogo cha Himo na kuanza kulifukuza gari hilo ili kuli-block jambo ambalo pia halikufua dafu kwani almanusura gari hilo liligonge gari la OCS wa Kituo cha Polisi Himo.

Polisi walilazimika kuongeza nguvu zaidi ya magari kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Moshi - Kilimanjaro ndipo walipofanikiwa kulizuia gari hilo kwa kuziba barabara zote na kuwakamata watuhumiwa wawili kati ya watatu ambapo mmoja alifanikiwa kutoroka kwa kuruka Dirishani. Baada ya purukushani hizo zilizodumu kwa zaidi ya saa 2 ndipo gari hilo lilikutwa na Mapanga, Marungu, Sime, Mikuki, Jambia na plate number nne za magari tofauti.

Watuhumiwa wamejitetea kwamba wao ni usalama wa Taifa hata hivyo Idara hiyo imewakana haiwafahamu.

=====

Baadhi ya matukio wanayohusishwa nayo:

Septemba 9, 2020:

Watu wasiojulikana wakiwa na gari aina ya Toyota Prado lenye namba za DFP wanadaiwa kuwateka nyara makada wawili wa NCCR-Mageuzi jimbo la Vunjo kisha kuwatesa na mmoja kukatwa sikio lake la kulia.

Taarifa za uhakika zimewataja makada hao kuwa ni Yolanda Lyimo ambaye ni mgombea udiwani viti maalum na Deogratius Mosha ambaye ni kampeni Meneja wa mgombea udiwani kata ya Kilema kati, Gibras Riwa.

Vyanzo vya habari vinadai kuwa tukio hilo lilitokea juzi kati ya saa 12:00 na 1:00 usiku katika kijiji cha Mkyashi huko kata ya Kilema ambapo watu wasiojulikana, wakiwa na bunduki waliwateka makada hao.

Inadaiwa kuwa watu hao waliokuwa na gari aina ya Prado, walijitambulisha kwa makada hao waliokuwa na mazungumzo yao binfasi na watu wengine watatu, kwamba wao ni maofisa wa Jeshi la Polisi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, waliwachukua Yolanda na Deogratius na kuwaamuru wapakie kwenye gari kuwa wanakwenda kufanya nao mahojiano, lakini badala yake walilazwa kwenye gari hiyo.

Baadae katika eneo ambao hawakulitambua, watu hao walianza kuwatesa kwa kuwapiga ambapo Deogratius alikatwa sikio lake la kulia na baadae kutelekezwa kwenye pori lenye miba katika msitu Ghona.

Hata hivyo, waliweza kujikongoja umbali wa kati ya kilometa 3 hadi 4 hadi kijiji cha Ghona ambapo wananchi waliweza kuwapa msaada ikiwamo kupiga simu polisi Himo, ambao walifika na kuwachukua.

Yolanda kwa sasa ni mgombea udiwani viti maalum na katika mchakato wa uchaguzi mkuu 2020, alishiriki kura za maoni CCM kuwania Udiwani kata ya Kilema Kati lakini hakuteuliwa ndipo akajiunga na NCCR-Mageuzi.

Pia ni Diwani aliyemaliza muda wake katika kata hiyo hiyo lakini kupitia chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wakati Deogratius yeye ni kampeni Meneja wa mgombea udiwani kata ya Kilema Kati

>>>>>

Tarehe 6 Oktoba 2020:

Vitendo vya kiharamia vya kuteka makada wa vyama, kuwatesa na hata kuwaua vimeanza kutikisa nchi baada ya makada wawili wa CHADEMA Wilaya ya Hai, kutekwa na kufanyiwa mateso makubwa.

Miongoni mwa mateso hayo ni kuingiziwa mti sehemu ya haja kubwa, kuminywa korodani kwa koleo, kujaribu kuwang’oa meno kwa koleo, mmoja kukatwa sikio na wote kuteswa kwa kupigwa na shoti ya umeme.

Makada hao walitekwa kata ya Narumu juzi na watu waliokuwa na magari ya kiraia matatu wakidaiwa kuwa na bunduki mbili na bastola moja, na baada ya mateso hayo, waliwatupa maeneo tofauti wilayani Arumeru.

>>>>>

Matukio wanayohusishwa watu ni mengi, tusubiri kuona mwisho wao utakuwaje
polisi wakikamata hata mwizi wa kuku cha kwanza ni kuwatia pingu ila hawa wauaji na watesaji wamerelax tu. Kiufupi hapo hakuna jipya hawa wahuni wote dawa yao ni NGUVU YA UMMA TUWAGAWANE!!!😎😎😎😎
 
Duh basi Kawe wana hela kwani wamejipanga hasa mwaka huu
kuna sehemu leo Ukerewe na Chato watu wamejikusanya kwa kutumia usafiri wa miguu na mitumbwi bila mabango wala jezi, tena wametandika khanga zao na vitenge mwanakondoo apite
View attachment 1599959
Kutandikiwa kanga ni kawaida mkuu, hawajafagia barabara na kudeki ziwa?
 
Kama na huyo Sabaya anafanya hivyo ni rahisi kumubana kwa kutumia ushahidi wa nyuma, Nina ndugu zangu usalama wa Taifa huwa hawajitangazi kabisa tena nimewahi kuishi kwenye nyumba zao za ofisi lakini hata majirani tulikuwa tunawabishia Sasa hao usalama wa kufoji ndo wanajitapa ili kufanya unyanganyi.
Story zaidi
 
Dr Charles Kimei ameshaanza kuonesha sura yake halisi. Haridhiki na utajirisho aliouvuna na hata kuzawadiwa na CRDB? Ubunge ataupata au kuukosa kwa haki, sio kunyakua kwa nguvu. Unadhani hao vibaka wanagharamiwa na Nani?
Hali ngumu sana,🤗,mrema ni boss,mbatia boss,saitakuaje?..!!!😲😲
 
Hilo genge la kigaidi la CCM lilijisahau na kwenye kumfanyia wenzao Mbatia ndio maana mnaona liko hadharani
 
Kinachonishangaza sana ni kuwa CCM LUMUMBA wamekaa kimya. Huku ni kukiri kiaina.

Nccr au chadema waweke wakili kufuatilia hili.
 
PM anadiriki kuzurura kuomba kura nchi nzima pia kushiriki ibaada na dua ili hali yeye binafsi alibariki mbinu ovu kwa wapinzani wake kutekwa, kupigwa apite bila kupigwa. Nilikuwa namshemu sana PM ila dhuluma hizi!?
Ameshahukumiwa Huko.Mbinguni anasubiri kutumwa kwenye ziwa likawalo moto alioandaliwa ibilisi na malaika zake. Neno la Mungu liko wazi. Atendae dhambi ni wa shetani
 
Kwahiyo mkuu hapo ndio Yale maneno anayasemaga chair wao "win win situation"
Kwamba mbatia kasafishwa kuwa ni mpinzani wa kweli
Upande wa pili nao sasa serikali imeshalitambua na kudhibiti watu wasiojulikana wanaowavamia wapinzani
Tumeshaigundua hiyo. Washenzi sana hao.
 
Hii habari imefikaje kwenye public domain? Maana yake bila chembe ya shaka chama cha mapinduzi kina vikundi vya kigaidi, kutesa na kuua watu

Imekuwaje habari hii haijazuiwa kutoka?
Kuna jambo gani limepangwa?

Sina imani na polisi lakini hili linanifanya niwaze mara mbili

Huyu Mungu huyu, mnayofanya gizani sasa yanaonekana nuruni

Bado kitambo kidogo tu sasa tutaanza kuheshimiana
Ndio hapo sasa. Habari kama hii ya kiintelijensia? Wameshafeli
 
Back
Top Bottom