Kilimanjaro: Wanawake wakimbia makazi yao kukwepa wabakaji

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Baadhi ya Wanawake wa Kijiji cha Shirimatunda, Kata ya Mnadani, Wilaya ya Hai wamekazimika kukimbia makazi yao kutokana na kuibuka kwa wimbi la Wanaume wanaofanya vitendo vya ubakaji.

Matukio hayo yanadaiwa kutokea katika maeneo ya mtoni wakati Wanawake wakifuata maji, ambapo wanaofanya tukio hilo wanajulikana kwa majina ya ‘Teleza’

Wanawake wa Kijiji hicho wametoa malalamiko yao hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai wakati alipofanya ziara wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo. Baada ya kupata malalamiko hayo, Kagaigai amemuagiza RPC wa Kilimanjaro, Simon Maigwa kushughulikia tatizo hilo.

Mtendaji wa Kata ya Mnadani ajili ya ziara ya Sembuli Mkilaha amelikiri kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na kuyafikisha kwenye mamlaka husika ya wilaya hiyo.

Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema ataunda kamati kuhakikisha wanaofanya vitendo hivyo dhidi ya Wanawake wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 
Teleza bado wapo tu.
Ila huwa wanahusishwa na imani za kishirikina hawa jamaa.

Kaskazini kunani jana tena nimeona habari eti Arusha mawe yanarushwa na mrushaji haonekani.
Ukikaa vibaya utabondwa jiwe na hujui limetoka wapi
 
Huko ndo kwenye shule kila baada ya hatua mbili; huko ndo sehemu moja kati ga chache zilizoendelea zaidi tz yetu hii.
Kwa hakika Afrika bado saaaana!! Tuna safari ndefu mnoooo!
 
Baadhi ya Wanawake wa Kijiji cha Shirimatunda, Kata ya Mnadani, Wilaya ya Hai wamekazimika kukimbia makazi yao kutokana na kuibuka kwa wimbi la Wanaume wanaofanya vitendo vya ubakaji.

Matukio hayo yanadaiwa kutokea katika maeneo ya mtoni wakati Wanawake wakifuata maji, ambapo wanaofanya tukio hilo wanajulikana kwa majina ya ‘Teleza’

Wanawake wa Kijiji hicho wametoa malalamiko yao hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai wakati alipofanya ziara wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo. Baada ya kupata malalamiko hayo, Kagaigai amemuagiza RPC wa Kilimanjaro, Simon Maigwa kushughulikia tatizo hilo.

Mtendaji wa Kata ya Mnadani ajili ya ziara ya Sembuli Mkilaha amelikiri kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na kuyafikisha kwenye mamlaka husika ya wilaya hiyo.

Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema ataunda kamati kuhakikisha wanaofanya vitendo hivyo dhidi ya Wanawake wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Eti teleza. Kwahiyo wanatelezea tu humo. Jamani
 
Hatimaye neno utelezi limepata kitenzi chake Teleza.

Anyway pole kwa wahanga..jeshi la polisi na wananchi washirikiane kwa pamoja kutokomeza vitedo hivi.

#MaendeleoHayanaChama
Haujui kiswahili, utelezi si kitendo, teleza ni kitendo.
 
Back
Top Bottom