Kilimo cha maembe ya kisasa

Ndugu wazo ni zuri,ila hapo kwenye bei ya embe hapana,mara nyingi viwandani 1kg ya embe hua haizidi 500/=,mfano kwa sasa 1kg=350/= sayona,sio rahisi embe moja liwe na kilo moja,

NOTE.
Fanya tafiti ni aina gani ya embe ndizo zinahitajika zaidi viwandani,
Kuwa Makini na embe utazopanda kwani sio kila embe zinahitajika viwandani.
Kila la kheri.
 
Asante kwa taarifa muhimu na ushauri
 
Reactions: Lax
Mkuu toa msaada kama unafahamu embe zinazohitajika viwandani
 
Reactions: Lax
Unamkatisha tamaa kama kweli ni mwenyeji wa Tabora, Jirani na bwawa la Kazima kuna mstafu wa idara ya maji ana miti mingi ya miembe na kwa miaka ile ya 2019 embe zake zilikuwa zikiletwa soko la Tabora (kachoma) zilikuwa zinafanya vizuri sana.
 
Habari tena...naleta mrejesho tena...nimefanikiwa kupanda miche 450 ya miembe Nov 10,2024.(Dodo 200,Red Indian 100,Apple 50 na Kent 50).Kwa sasa kama yote imeshika vizuri na nataraji Mwezi huu nikaweke NPK 50gm kwa kila mti maana sikufanikiwa kupata samadi ya Ng'ombe.Mwezi wa 4 nitaipalilia na kufungua zile nylon za maungio...
 
Reactions: Lax
Reactions: Lax
Asante kunialika...ila nimechelewa naomba next time ukinialika nipigie na simu (0621095721).Niko serious na zao hili maana mwaka ujao napanda miche mingine kama 600 hivi
Sawa mkuu, pia unaweza jiunga na hiyo club na wewe ukawa mdau
 
Kongole mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…