Kilimo cha maembe ya kisasa

Kilimo cha maembe ya kisasa

Katika hekaheka za kujiandaa kustaafu miaka 7 baadae nimeamua nipande miche kama 500 yaani ekari 10 za maembe kisasa.

Shamba lipo Tabora kwa sasa naendelea kuchimba mashimo. Nitapanda bila mbolea ya samadi ila taweka NPK baada ya miezi 3 ikiwa imeshika.

Mpango wangu miche 450 ipone ili nipate wastani wa embe 500 kila mti mwaka wa 6 na hii itanipa embe 225,000 na kama tauza kwa Tzs 400 nipate 90m.Hapo nitaamua kustaafu kazi nikiwa na miaka 55.
Ndugu wazo ni zuri,ila hapo kwenye bei ya embe hapana,mara nyingi viwandani 1kg ya embe hua haizidi 500/=,mfano kwa sasa 1kg=350/= sayona,sio rahisi embe moja liwe na kilo moja,

NOTE.
Fanya tafiti ni aina gani ya embe ndizo zinahitajika zaidi viwandani,
Kuwa Makini na embe utazopanda kwani sio kila embe zinahitajika viwandani.
Kila la kheri.
 
Asante kwa taarifa muhimu na ushauri
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Ndugu wazo ni zuri,ila hapo kwenye bei ya embe hapana,mara nyingi viwandani 1kg ya embe hua haizidi 500/=,mfano kwa sasa 1kg=350/= sayona,sio rahisi embe moja liwe na kilo moja,

NOTE.
Fanya tafiti ni aina gani ya embe ndizo zinahitajika zaidi viwandani,
Kuwa Makini na embe utazopanda kwani sio kila embe zinahitajika viwandani.
Kila la kheri.
Mkuu toa msaada kama unafahamu embe zinazohitajika viwandani
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Unapoteza muda ndugu, ungetuuliza tuliozaliwa na kukulia Tabora kabla ya kuingia gharama zote hizi ikitarajia mapato hewa hewa (ya kwenye makaratasi).

Msimu wa maembe huko Tabora huwa yanagawiwa bure, yaani inafika muda Kenta zima linuzwa elfu 30. Ili unielewe vizuri uliza watu wa Iringa, msimu wa nyanya baei inakuwaje. Na kwanini kilimo cha nyanya hakiwatoi.

Pia waulize watu wa huko Mbeya na Njombe kwanini kilimo cha parachichi hakiwatoi?

Wakati wewe ukihangaika kupanda miembe, Kuna maeneo huko Tabora wamezaliwa na kukuta msitu wa miembe.
Unamkatisha tamaa kama kweli ni mwenyeji wa Tabora, Jirani na bwawa la Kazima kuna mstafu wa idara ya maji ana miti mingi ya miembe na kwa miaka ile ya 2019 embe zake zilikuwa zikiletwa soko la Tabora (kachoma) zilikuwa zinafanya vizuri sana.
 
Habari tena...naleta mrejesho tena...nimefanikiwa kupanda miche 450 ya miembe Nov 10,2024.(Dodo 200,Red Indian 100,Apple 50 na Kent 50).Kwa sasa kama yote imeshika vizuri na nataraji Mwezi huu nikaweke NPK 50gm kwa kila mti maana sikufanikiwa kupata samadi ya Ng'ombe.Mwezi wa 4 nitaipalilia na kufungua zile nylon za maungio...
 
  • Thanks
Reactions: Lax
  • Thanks
Reactions: Lax
Asante kunialika...ila nimechelewa naomba next time ukinialika nipigie na simu (0621095721).Niko serious na zao hili maana mwaka ujao napanda miche mingine kama 600 hivi
Sawa mkuu, pia unaweza jiunga na hiyo club na wewe ukawa mdau
 
Habari tena...naleta mrejesho tena...nimefanikiwa kupanda miche 450 ya miembe Nov 10,2024.(Dodo 200,Red Indian 100,Apple 50 na Kent 50).Kwa sasa kama yote imeshika vizuri na nataraji Mwezi huu nikaweke NPK 50gm kwa kila mti maana sikufanikiwa kupata samadi ya Ng'ombe.Mwezi wa 4 nitaipalilia na kufungua zile nylon za maungio...
Kongole mkuu
 
Back
Top Bottom