Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

Kiujumla mazao ya mbogamboga na matunda unapotaka kuzalisha unashauriwa kuzingatia yafuatayo
  • Upatikanaji wa uhakika wa maji kwani huhitaji maji ya kutosha na upungufu wowote huweza kusababisha hasara.
  • kulima sehemu ambayo panafikika wakati wowote ili kuweza kusafirisha mavuno kwenda sokoni
  • kufahamu soko lako litakuwa wapi na utawauzia wakina nani. Mazao mengi ya jamii hii huharibika haraka na hivyo hayawezi kutunzwa muda mrefu. Hivyo ni muhimu kabla ya kuotesha kutafuta soko kabisa. wengi ambao wamejaribu kupeleka mazao yao wenyewe sokoni waliambulia hasara kwan masoko mengi yameshikwa na madalali ambao ni walanguzi. Fikiria zao kama nanasi umefika nalo sokoni na fusso halafu madalali wanakuzungusha kulala siku moja tu yaweza kukusababishia hasara kubwa. Ushauri ni bora kumalizana na mnunuzi shambani asafirishe mwenyewe.
  • kupima udongo ili kujua hali yake
  • kuwa na elimu ya mwanzo ya utunzaji na magonjwa ambayo unayotegemea kukutana nayo hii itakupa muda wa kujiandaa. Mazao mengi huwa na kalenda ya kupulizia dawa katika muda maalum ili kuzuia ugonjwa kujitokeza. Kitaalamu tunasema magonjwa mengi yakishajitokeza unakuwa tayari umepata hasara kuanzia asilimi 10. Magonjwa kama ya kuvu (fungi) ni lazima yajitokeze tu kwenye tikiti na kuyazuia hasa kipindi cha kutoa maua ni muhimu. Suala kama la umwagiliaji lataka lifanyike vizuri vinginevyo laweza sababisha madhara ikiwemo kupasuka kwa tikiti. Hii hasa huletwa na kubadilishabadilisha ratiba ya uwagiliaji.
  • Mwisho lakini muhimu kuliko yote ni kuwa na andiko/mpango utakao ainisha gharama za uzalishaji ambapo kila hatua itaanishwa na gharama zake
 
Kwangu pale kambi kuu au kule tulikovuka kabisa?

Hata tulikovuka sio mbaya kaka, mradi pasiwe ghali tu Mkuu, si wajua tena miezi imekaa vibaya hii!!
 
Nimeshakupa mambo kupitia mail yako.

mimi napenda kujua taratibu au ratiba za kumwagilia shamba la tikiti maji hekari 2. Je unamwagilia kila baada ya muda gani na kiasi gani cha maji kinahitajika kwa shimo? Je water pump ya lita 3(euromax) itagharimu lita ngapi kwa hekari 2.?
 
nataka kulima kwahiyo napenda kufahamu machache tu. Mbegu aina gani ni nzuri? Ratiba ya umwagiliaji na kiasi cha maji kinachohitajika kwa shimo? Mbolea aina gani inatumika! Ratiba kunyunyuzia dawa? Kwa water pump ya lita 3 itanigharimu lita kwa hekari 2?
 
Kilimo hiki ni kizuri sana. Ila nadhani watu wengi wankuja kulizwa kwenye soko. Kabla mtu hujaingiza team kulima ni bora kufanya marketing survey and kujua utamuuzia nani na wapi.

Ukitegemea kupeleka sokoni madalali walishakamata soko na upeo wao wa kufikiri ni mdogo kama sisimizi
 


Nimeipenda hii brother Kisima niombe mawasiliano yako Mkuu ili nikihitaji msaada iwe rahisi. Big up
 
Last edited by a moderator:
  1. Mbegu za tikiti maji kwa ekari moja naweza kutumia kiasi gani?
  2. Kilo moja ya mbegu za tikiti maji ni Tshs ngapi?
  3. Soko la uhakika la zao la Tikiti Maji kwa Dar na Moro nitapataje? na wapi?
  4. Gharama za kutandaza mabomba (pamoja na motor) kwa ajili ya drip irrigation kwa ekari 6 ni Tsh ngapi?

N.B: Unaweza kujibu swali ambalo unaweza kujibu, ambalo hujui waachie wenzako watajibu.
 
Kama upo dar watafute uhuru farm.wanalimia kimbiji..ni wataalam wa kufa mtu..au nenda uhuru round abt utaona maduka ya komputa yameandikwa uhuru computers...uliza mohamed tatizo lako limeisha.
 
Nipm sasa hivi nikupe namba ya mtu Anatolia Hiyo na kufanikiwa ukiongea naye kwa simu atajibu maswali yako tote,siwez weka hapa namba yake bila ruksa Kama uko serious ni pm nikupe namba harafu uje kuleta majibu umu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…