BabM
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 1,166
- 954
Kiujumla mazao ya mbogamboga na matunda unapotaka kuzalisha unashauriwa kuzingatia yafuatayo
- Upatikanaji wa uhakika wa maji kwani huhitaji maji ya kutosha na upungufu wowote huweza kusababisha hasara.
- kulima sehemu ambayo panafikika wakati wowote ili kuweza kusafirisha mavuno kwenda sokoni
- kufahamu soko lako litakuwa wapi na utawauzia wakina nani. Mazao mengi ya jamii hii huharibika haraka na hivyo hayawezi kutunzwa muda mrefu. Hivyo ni muhimu kabla ya kuotesha kutafuta soko kabisa. wengi ambao wamejaribu kupeleka mazao yao wenyewe sokoni waliambulia hasara kwan masoko mengi yameshikwa na madalali ambao ni walanguzi. Fikiria zao kama nanasi umefika nalo sokoni na fusso halafu madalali wanakuzungusha kulala siku moja tu yaweza kukusababishia hasara kubwa. Ushauri ni bora kumalizana na mnunuzi shambani asafirishe mwenyewe.
- kupima udongo ili kujua hali yake
- kuwa na elimu ya mwanzo ya utunzaji na magonjwa ambayo unayotegemea kukutana nayo hii itakupa muda wa kujiandaa. Mazao mengi huwa na kalenda ya kupulizia dawa katika muda maalum ili kuzuia ugonjwa kujitokeza. Kitaalamu tunasema magonjwa mengi yakishajitokeza unakuwa tayari umepata hasara kuanzia asilimi 10. Magonjwa kama ya kuvu (fungi) ni lazima yajitokeze tu kwenye tikiti na kuyazuia hasa kipindi cha kutoa maua ni muhimu. Suala kama la umwagiliaji lataka lifanyike vizuri vinginevyo laweza sababisha madhara ikiwemo kupasuka kwa tikiti. Hii hasa huletwa na kubadilishabadilisha ratiba ya uwagiliaji.
- Mwisho lakini muhimu kuliko yote ni kuwa na andiko/mpango utakao ainisha gharama za uzalishaji ambapo kila hatua itaanishwa na gharama zake