Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

Naweza kukukodisha eka moja kwa Tsh 60,000/ unanilipa kabla, shamba lipo Pwani ya Mkuranga,maji yapo mengi sana,banda la kuishi kijana lipo. Unaweza pata eka hata 15 zilizo kando ya maji ya kudumu.

Mkuu malila naomba uni PM namba yako na mimi nahitaji kukodi eneo kwa ajili ya kulima matikiti.
 
March to may ndio masika kwa ukanda wa Pwani,nyanda za juu kusini masika huanza november mwishoni mpaka may. Kwa hiyo utaona kwamba,november mpaka february kwa ukanda wa pwani si masika. sasa tikiti maji lenye soko la kufa mtu ni hili la january,february, tikiti la kuanzia may mpaka july huwa ni majanga sababu wakulima wengi huwa wanamudu changamoto za maji mashambani.

Ahsante Mkuu nimepata kitu kutokana na maelezo yako. Je, Arusha pia huu msimu wa Novemba - Februari unafaa? Ni eneo la Nduruma lenye joto kiasi kuliko maeneo mengine ya Arusha.
 
Mkuu Livanga hapa dar mbona soko lipo kubwa la tikiti maji,

Zunguka mitaa ya hostel za wanafunzi (km mabibo hostel, UD main campus kuna cafteria kubwa 3) na pia karibu na vyuo kama IFM, CBE, NIT n.k kuna wauzaji wa matunda wengi sana unaweza ongea nao ukawa unasupply kwao kwa bei utakayo maana wengi wao huwa wanafata sokoni wenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Sisi tuliopo dar,tunawezaje kupata mashamba ya karibu ili iwe rahisi kufika shambani mara kwa mara,mwenye kujua..

Mbona mashamba yapo mengi sana,tena yenye maji ya kudumu, ukitaka ya kukodi au kununua yapo mkuu, ni wewe na hela yako basi.
 
Nipo Dar mkuu.

OK. Basi nakushauri kama uko kazini omba likizo ya wiki 2. Zunguka Kwa wauzaji wadogowadogo huku mitaani ujue bei wanazouzia then washawishi kununua kutoka kwako Kwa bei nafuu.

Mfano tikiti analouza Tshs. 4000 mfanyie 2500 Kwa vile unampelekea hadi alipo. Angalia mahesabu yako yalivyokaa hata Kwa 2000 muuzie maana nasikia ukipeleka kwenye masoko yale makubwa watanunua tikiti Kwa flat price ya Tshs. 1000 tu Kwa kila tikiti, maana unakutana na dalali kwanza kisha wanunuzi wengine.
 
Naweza kukukodisha eka moja
kwa Tsh 60,000/ unanilipa kabla, shamba lipo Pwani ya Mkuranga,maji yapo
mengi sana,banda la kuishi kijana lipo. Unaweza pata eka hata 15 zilizo
kando ya maji ya kudumu.

Mkuu nami naomba un PM namba yako ya simu tuwasiliane, nahitaji shamba la kukodi
 
mkuu mtaji sio mkubwa sana nimejaribu this year kulima ndio navuna sasa, nimetumia milion 2,320,000/= kwa heka mbili hapo nilikuwa mgeni ila next time ninauhakika wa kutumia mil. 1.8 hivi kwa ekari mbili,,,,so unaweza kujipanga hata eka moja tu mkuu.

unaweza kunichambulia zilitumikaje na yapi ambayo hayana umuhimu kwa sana maana hadi sasa nategemea kutumia ml 1 shamba la kukodi
 
Mr Edmund naomba uni PM namba yako nitaanza Kulima matikiti MAJI ##au nitumie namba yako kwa 0768366716
 
Matikiti ni matunda, japo tunasema ni mboga kutokana na njia zinazotumika kuyazalsha kwan siyo tofaut na mboga.

Matunda yanaanza kukomaa kuanzia siku 80-120 kufuatana na aina, kama sugarbaby inakomaa mapema. Na il kupata matunda makubwa na yenye ubora, tunashaur kwa mti mmoja usiwe na matunda zaidi ya matano ambayo interval ya kuvuna ni siku hadi 10 kwani uvunaj ni had miezi miwil kwa mti mmoja. Hector 1=8-12 tan za matunda.

Kwa maswali zaidi kuhusu kilimo cha mazao tuwasiliane.

Ur number plz au ni Pm kk ili tupeane madini juu ya tikiti
 
Habari ndugu, niko Dodoma na nina plan ya kulima tikiti maji, please assist me in some issues:
1. Shamba lanu liko maeneo ya Ntyuka, je ni mbe
gu gani zinafaa?
2. Chan
gamoto zinazoambatana na kilimo cha tikiti maji ni zipi?
3. If you have any other helpful details please provide me with them

Thanks in advance.
 
Mbona mashamba yapo mengi sana,tena yenye maji ya kudumu, ukitaka ya kukodi au kununua yapo mkuu, ni wewe na hela yako basi.
Mkuu nahitaji kule Shungumbweni, heka 2 tu alongside Mto, ukirudi kutoka kisiwani tutafutane basi!!
 
Mkuu nahitaji kule Shungumbweni, heka 2 tu alongside Mto, ukirudi kutoka kisiwani tutafutane basi!!

Ijumaa naingia mjini, jumapili nitaenda kule kaka nikawaone vijana.
 
Habari ndugu, niko Dodoma na nina plan ya kulima tikiti maji, please assist me in some issues:
1. Shamba lanu liko maeneo ya Ntyuka, je ni mbe
gu gani zinafaa?
2. Chan
gamoto zinazoambatana na kilimo cha tikiti maji ni zipi?
3. If you have any other helpful details please provide me with them

Thanks in advance.
 
Ushasikia mtu ametajirika kwa ukulima?

Hata kama hatutajiriki lkn ndio kimewaweka mjini zaidi ya asilimia 80 ya watz. wanakula wanalala na wanasomesha. utajiri ni majaliwa
 
Nimejaribu kufuatilia kuanzia mwanzo michango ya watu mbalimbali ili kuwona namna naweza kuchangia katika kuboresha.

Nikiri mapema kuwa mimi ni mtaalamu wa kilimo kwa ujumla na matunda na mbogamboga hasa na pia nimexcel kwenye maswala ya mbolea na udongo hivyo nitakuwa nachangia kwa kadiri muda utavokuwa unaniruhusu na kumoderate baadhi ya zana nitaugawa mchango wangu sehemu tatu kwanza ni ushauri wa ujumla, kisha utaalamu wa uoteshaji na magonjwa na mwisho mbolea na utunzaji.
 
Back
Top Bottom