Kilimo cha Tangawizi - Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Kilimo cha Tangawizi - Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Tangawizi inalipa. Hata hivyo kwa Mwaka huu bei imeshuka sana hadi wakulima wanauza kwa 700/- kwa kilo.Tufikirie mbali, kwa kufanya Agroprocessing ya Tangawizi. Kule Kg ni majonzi na vipimo kwa Wenye nayo kwa sasa.
 
Heshima kwenu wakuu.

Ninaambiwa na watu kwamba kilimo cha tangawizi kinalipa sana kwa sababu soko la uhakika lipo na ni zuri.

Nimeshaelekezwa sehemu ambayo hili zao linakubali uzuri.

Ombi langu ni kwa wale wenye uzoefu na kilimo hiki wanipe A,B,C...zote kuhusu kilimo cha zao hili.

Ningependa kujua kuhusu gharama ninazoweza kukumbana nazo mpaka zao hili lifikie hatua ya kuvunwa toka shambani.

Thanks in advance.
========== Majibu kutoka kwa wadau ===========

Nimependa sana maoni haya
 
Bei ya tangawizi imeshuka mkoani kigoma,kwa sasa kilo moja ni kati ya tzs: 500 na 800, kama utaifuata katika vijiji vya Kishanga,Kalela na Kanazi, Huu ndio wakati mzuri wa kununua mbegu kwa sababu bei itapanda siku chache zijazo kwa sababu kuna wafanyabiashara kutoka Rwanda na Kenya huwa wanaifuata vijijini.
Nitahitaji mbegu kias gani kupanda heka 2?
 
Back
Top Bottom