Kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kuomba radhi kutokana na mtu niliyemuachia maagizo ya kuweka bandiko hili hakutoa ufafanuzi mzuri.
Ufafanuzi huu ntautoa kwa kifupi hapa na ntaambatanisha na excel ambayo ina mchanganuo mzuri zaidi.
Mbegu hii imeandaliwa kisasa na inazalishwa nchini kenya, nimeitumia huu ni mwaka wa nne na sijawahi kukatishwa tamaa na mbegu hii.
Kwa kawaida hutumia lita 10 hadi 15 kwa eneo la ekari moja.
Suala la bei sokoni kwanza kabisa inatokana na ubora wa kitunguu na pia timing ya mavuno yako. Kwa mfano, mimi nalima Kidete na Bagamoyo. Kidete huwa napanda mwezi wa tatu katikati na nakuja kuvuna mwezi wa saba kwenye tarehe 10 na huwa nakutana na bei ya 110,000 hadi 95,000 na kwa bagamoyo nimepanda mwezi huu mwanzo na nategemea kuvuna mwezi wa tatu ambapo bei ya vitunguu huwa juu sana kwasababu shamban tu gunia hufikia hadi 120,000/=
Naomba nieleweke kwamba haya yote nnayoongea sio kwamba navutia biashara ya mbegu ila ni kitu halisi na mtu yoyote anaweza kufika ofisini na nikamuonyesha risiti za mauzo ya sokoni. Kwa fukara kama mimi anayetafuta kujiajiri hii ni nafasi nzuri na tutasaidiana kwa utaalamu bila malipo yoyote.
NB: Naomba muangalie excel niyoiambatanisha hapo chini nimejaribu kutoa mchanganuo wa gharama kamili ya kilimo kwa shamba la ekari moja na mchanganuo kama ukiamua wewe mwenyewe kuleta mzigo mjini na faida ya biashara nzima ndani ya miezi mitatu.
Kama kuna sehemu ntakua nimesahau kutoa maelezo basi tusameheane na ntashukuru ukinitafuta tukaongea zaidi kulikoni kutoa maneno machafu na ya kejeli mtandaoni.
Ahsanteni sana
namba yangu no 0655003510