Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

85000tsh imposible otherwise ulilima nakutoa mwezi wa5 ndyo hyo bei ilikuwepo.hafu pia bei hyo wanaokuta ni watu wanaoweka store kitunguu nakutoa mwezi 2 ndyo wanaokuta hyo bei.au niambie km unauza rejareja kwenye kibanda chako hapo dar sokoni unaweza kuikuta hyo bei.
 
Bei ya Onions sokoni Temeke kwa Current Week: Bei ya juu ni 85000Tsh /KGS Bei ya chini ni 80000Tsh / KGS

Bei ya Onions sokoni Lindi kwa Current Week: Bei ya juu ni 120000Tsh /100KG Bei ya chini ni 115000Tsh / 100KG
 
85000tsh imposible otherwise ulilima nakutoa mwezi wa5 ndyo hyo bei ilikuwepo.hafu pia bei hyo wanaokuta ni watu wanaoweka store kitunguu nakutoa mwezi 2 ndyo wanaokuta hyo bei.au niambie km unauza rejareja kwenye kibanda chako hapo dar sokoni unaweza kuikuta hyo bei.

Inaelekeaaa Ubishi ni Jadi yako kijanaa. Unachshangaaa nn na unabisha nn.

Unajua watu wanapouziaaa...
Au napayuka tu. Watu wameza hadi 120000.

Wewe nashangaaa 85000.
 
Sasa ndugu yangu niandike uongo hapa ili nimdanganye nani sasa, unabishana na mimi njoo ofisini kwangu nikuonyeshe risiti za kkoo.

Sijawahi kuuza rejareja na sina mategemeo hayo. Kwa maelezo yako hata bishara ya vitunguu yenyewe unaonesha unajifunza kwa kupitia maneno ya watu mdomoni.
85000tsh imposible otherwise ulilima nakutoa mwezi wa5 ndyo hyo bei ilikuwepo.hafu pia bei hyo wanaokuta ni watu wanaoweka store kitunguu nakutoa mwezi 2 ndyo wanaokuta hyo bei.au niambie km unauza rejareja kwenye kibanda chako hapo dar sokoni unaweza kuikuta hyo bei.
 
Biashara ya kilimo cha vitunguu ni kama biashara nyingine, huwezi ukasema utapiga hela tu bila kuwa na mbinu za kuepuka changamoto ndo mana ukitumia wazoefu hayo madhara hutoyapata.

Shida watu wanasikia tu mtaani kwamba kilimo cha vitunguu kinalipa then ghafla tu wanakimbilia mabondeni kwenda kulima bila kujua nini kipo nyuma yake ndo mana huishia kupata hasara na kuwakatisha tamaa wengine wenye nia ya kuanza kilimo. Kwahiyo nashauri watu kuconsult wazoefu wa biashara ya vitunguu kabla ya kuingia huko manake kuna wanaotoka kapa pia.

Narudia kusema tena, tokea nimeanza kilimo cha vitunguu sijawahi uza gunia langu chini ya tshs 85,000/= hata mwaka huu ambao umekua kilio kwa watu wengi.

Tupige kazi na kuachana na maneno ya vijiweni.
IMG_1365.JPG
IMG_1369.JPG
 
Sasa ndugu yangu niandike uongo hapa ili nimdanganye nani sasa, unabishana na mimi njoo ofisini kwangu nikuonyeshe risiti za kkoo. Sijawahi kuuza rejareja na sina mategemeo hayo. Kwa maelezo yako hata bishara ya vitunguu yenyewe unaonesha unajifunza kwa kupitia maneno ya watu mdomoni.

Baba inabidi nikutafute private
 
Mkubwa kufanya mapinduzi ya vipi vitunguu vyako unataka viwe inawezekana, ila kwenye suala la soko ni ngumu sana. Me ni mkulima wa vitunguu huu mwaka wa tano sasa na mali yangu huwa ziuzii shamba naleta mjini mwenyewe. Madalali wameharibu soko na wameteka kila mahala, huwez kutoka na vitunguu vyako hadi zanzibar au commoro hautauza na utashangaa ni kwann. Kuna mkongwe mmoja aliwah jibeba na mzigo wake hadi comorro kufika kule wakawa wanamuangalia kama nini sijui, na alipiga hasara mzigo wote. Individually huwez kuwatoka madalali na hii ni mpaka wizara husika iingilie kati, bila ivo tutaendelea kufanya biashara na madalali tu. Naongea kwa experience wakuu.

Habari za china kaka
 
Ha ha ha nzuri boss wangu. Nimerudi nakutafuta naona kimya, nikajua uko busy. Ikabd nikuache kidogo


Sent from my iPhone using JamiiForums

Niko busy kwenye mambo ya kitaifa..ntaku text unipe ile product
 
Niko busy kwenye mambo ya kitaifa..ntaku text unipe ile product

Hakuna shaka boss, niko dodoma kwa sasa ila next week ntakua dar kwa week moja. Tutafutane uchukue


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kama unakwenda kukodi shamba sawa, mashamba ya kununua bei iko juu vibaya, je kuna mtu unayemfahamu pale wa kukusaidia? Kama huna sema nikupe mtu akusaidie na yy ana shamba pale.

Naomba number ya huyo mtu wa ruaha mbuyuni
 
Binafsi nalima kitunguu maeneo ya Kware Ruaha Mbuyuni hapa ni potential kw maana ya irrigation na ardhi ni nzur kw kitunguu. Hili zao linahitaj ujikamilishe kifedha unapoanza kulima ni muhimu ukaitenga pesa yake pemben kbsa kw heka inayohudumiwa vzur kila kitu inagarim million 3 ukiweka na lak 5 ya miscellaneous inakua vzur incase kuna mlipuko wa magonjwa km n'gonyo ambao wana athar kubwa na hugarim dawa kila baada ya siku kadhaa. Kware heka moja inakodishwa kw laki na nusu na pamp ya kumwagilia ni elf 50 jumla lak 2 mbegu huuzwa kw lita yale makopo yanayo nywewa mbege vilabuni ambapo kw kila lita ni elf 25 na heka moja inahitaj lita 10 ukiongeza mbili sio mbaya Kulima kw trekta ni sh elf 50 kw heka na ngombe ni 30 ila kw trekta ni nzur zaid cz inachimbua udongo vzur na hupunguza majan meng kuota halaf kuna kupengelenga hii ni kutengeneza majaruba kw ajili ya vitalu vya mbegu na yale ya kupandia shamban kw yale jaruba za mbegu hufanyaga sh 300 kw jaruba kw lita 10 unaweza pata jaruba 35 na zikizid bas kidgo sna halaf kw zile za shamban uwa wana charge kw heka ambapo kw heka wana pelenga laki na 20 hapo inabidi wasawazishe ardhi mana trekta linatifua sna ambapo kw heka wanafanya chini kbsa elf 10 ila wanaanzia elf 20.. Then kuna kupanda mbegu (Kuombeka) hapa ni sh 400 mpka 500 kw jaruba heka moja huwa na jaruba maxmum 400 halaf unapiga dawa ya kuzuia magugu weed stop na ile ya kuua majan yaliyo ota galgan au oxfan hizi ni elf 22 kw lita kw weed stop na unahitaj lita 4 kw heka kuna zile za kuua na kuzuia wadudu km DuDuba 13 kw ml 500 na unahitaj lita 1 kw heka na profercon elf 17 kw lita na unahitaj lita 2 kw heka na ile ya kuzuia ukungu kwenye majan ya kitunguu Amezeb elf 8 kw gram 500 na unahitaj kilo 1 kw heka then kuna mbolea apply after 2 wks urea elf 60 sehem nyngne mpka 66 kw mfuko na heka huitaj mifuko 4 then baadae CAN hii ni kw kukuzia mfuko elf 50-55 weka tena 4 ila dawa zinaweza kua constant kutokana na uwepo wa magonjwa pia gharama constant ni ya kumwagilia ambapo eka moja huitaj diesel lita 10-15 kutegemea na umbali wa shamba toka mtoni pia gharama za kijana atayemwagilia ambapo hudai elf 10-15 kw heka na pia wapiga dawa hudai elf 15 kw heka close supervision ni muhim sna inacse bajet inabana unaweza mwaga urea once then after 3-4 weeks ukapiga booster inaitwa super grow hii ni nzur sna kw kukikuza kitunguu jus elf 22 unapata lita nzima na inatosha kw heka nzima ukishapanda maji ni mara moja kw wiki kumwagilia na wakat wa kuvuna wanacharg 100-200 kw jaruba halaf kuna kukata majan ya kitunguu sh 2000 kw gunia. Eka moja iliyohufymiwa vzur hutoa gunia 70-80 na kila gunia ni elf 80 uwa inapanda mpka lak na 10 kikiwa adim na pia huweza kusguka mara chache mpka elf 70-75 ila average ni 80 kw shamban Vitunguu vya Ruaha Mbuyuni vinalimwa kiustad tofaut na singida au dodoma ivyo bei yake iko juu na huweza kulipa mara 3 mpka 4 zaid kw faida ila uhudumie vzur shamba.. Karibuni

Uzi wako upo exhaustive sana mkuu.

Naomba mawasiliano yako kama hutajali.

Ubarikiwe sana.
 
Kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kuomba radhi kutokana na mtu niliyemuachia maagizo ya kuweka bandiko hili hakutoa ufafanuzi mzuri.

Ufafanuzi huu ntautoa kwa kifupi hapa na ntaambatanisha na excel ambayo ina mchanganuo mzuri zaidi.
Mbegu hii imeandaliwa kisasa na inazalishwa nchini kenya, nimeitumia huu ni mwaka wa nne na sijawahi kukatishwa tamaa na mbegu hii.

Kwa kawaida hutumia lita 10 hadi 15 kwa eneo la ekari moja.

Suala la bei sokoni kwanza kabisa inatokana na ubora wa kitunguu na pia timing ya mavuno yako. Kwa mfano, mimi nalima Kidete na Bagamoyo. Kidete huwa napanda mwezi wa tatu katikati na nakuja kuvuna mwezi wa saba kwenye tarehe 10 na huwa nakutana na bei ya 110,000 hadi 95,000 na kwa bagamoyo nimepanda mwezi huu mwanzo na nategemea kuvuna mwezi wa tatu ambapo bei ya vitunguu huwa juu sana kwasababu shamban tu gunia hufikia hadi 120,000/=

Naomba nieleweke kwamba haya yote nnayoongea sio kwamba navutia biashara ya mbegu ila ni kitu halisi na mtu yoyote anaweza kufika ofisini na nikamuonyesha risiti za mauzo ya sokoni. Kwa fukara kama mimi anayetafuta kujiajiri hii ni nafasi nzuri na tutasaidiana kwa utaalamu bila malipo yoyote.

NB: Naomba muangalie excel niyoiambatanisha hapo chini nimejaribu kutoa mchanganuo wa gharama kamili ya kilimo kwa shamba la ekari moja na mchanganuo kama ukiamua wewe mwenyewe kuleta mzigo mjini na faida ya biashara nzima ndani ya miezi mitatu.

Kama kuna sehemu ntakua nimesahau kutoa maelezo basi tusameheane na ntashukuru ukinitafuta tukaongea zaidi kulikoni kutoa maneno machafu na ya kejeli mtandaoni.

Ahsanteni sana
namba yangu no 0655003510
Bulldog
 
Last edited by a moderator:
Nawashukuru wadau wote kwa elimu na maelezo mazuri kuhusiana na biashara hii ya ukulima na masoko ya vitunguu, nimejifunza mengi, nami nipo kwenye mchakato wa kuingia kwenye hichi kilimo,naomba tuzidi kupeana maarifa zaidi, pamoja tunaweza.

Mungu awabariki sana!
 
Naam nami nahitaji elimu hii kwani ninataka kuwa mkulima ajira hamna jamani ,nisaidieni waungwana kwani sina cha kufanya kwa sasa na maisha magumu sana huku mtaani...
 
Wakuu, kwa anaejua bei ya kitunguu kwa sasa imefikia kiasi gani?
 
Back
Top Bottom