Wazo ni zuri sana. Mimi nalima vitunguu Singida Wilaya mpya ya Mkarama Kata ya Mwanga.
Baraka alichosema kimsingi anapenda watu waweze kupanua mawazo kuelekea kwenye kilimo kitu ambacho nakiunga mkono sana. Tatizo ambalo hajaweza kulijua na huende anasikia siyo MKULIMA ekari moja inapandwa kilo tatu za mbegu. Bei za mbegu ni tofauti sana kulingana na maeneo kwa mfano Red Bombay ambazo tunazalisha sisi wenyewe huku mashambani debe moja halizidi laki moja.
Mbegu aina ya Neptune inapatikana Barton Tanzania Ltd inauzwa 120,000/- kwa nusu kilo, Red Caraoke ya South Afrika inauzwa 80,000/- kilo moja.
Kuhusu bei ya soko huyu ndugu anazungumzia Hapa Dar, hajasema huyo mkulima kutoka Mang'ora, au Singida Vijijini kwa bei anayosema dalali wa sokoni hamzungumzii najua huwezi kuleta bidhaa sokoni ukauza mpaka uwaone madalali.
Nina uzoefu mkubwa mwaka jana nilileta gunia 130 kwa mtu aliyesema angenunua akaja akaona mzigo akaufungua na kushona upya akatoa gunia 124 kwa bei ya 73,000/- wakati nimevitoa shambani singida akalipa advance millioni sita na laki tano pesa nyingine mpaka leo hajalipa simu hapokei.
Mwezi wa tano vitunguu shambani wanunuzi walileta bei ya shilingi 40,000/- hadi 50,000/- kwa gunia la wavu wanapakia viroba vitatu wanasema ni gunia moja, nikaona ni bora nilete vitunguu soko la misuna singida mjini, bei yao ilikuwa shilingi 53,000/- kwa gunia moja. Ushuru ni shs 1000/- kwa gunia, dalali 2,000/- kwa gunia, wanaochmbua shs 1,000/- kwa gunia, mshonaji 1,000/- kwa gunia nilikuwa na gunia 67.
Rafiki bei ya vitunguu haijawa na msimamo inategemea baraka za madalali na wingi wa mzigo uliopo sokoni.
Nitakupigia Baraka simu ila ukweli ndio huo.