Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Biashara ya kilimo cha vitunguu ni kama biashara nyingine, huwezi ukasema utapiga hela tu bila kuwa na mbinu za kuepuka changamoto ndo mana ukitumia wazoefu hayo madhara hutoyapata. Shida watu wanasikia tu mtaani kwamba kilimo cha vitunguu kinalipa then ghafla tu wanakimbilia mabondeni kwenda kulima bila kujua nini kipo nyuma yake ndo mana huishia kupata hasara na kuwakatisha tamaa wengine wenye nia ya kuanza kilimo. Kwahiyo nashauri watu kuconsult wazoefu wa biashara ya vitunguu kabla ya kuingia huko manake kuna wanaotoka kapa pia.

Narudia kusema tena, tokea nimeanza kilimo cha vitunguu sijawahi uza gunia langu chini ya tshs 85,000/= hata mwaka huu ambao umekua kilio kwa watu wengi.

Tupige kazi na kuachana na maneno ya vijiweni.

nimependa ushauri wako Baraka sjui ntapata vp contact zako maana mimi nimelima kitunguu kama heka 3 nategemea mwezi ujao katikati nitavuna if posible nataka uniunganishe soko la uhakika nimeku PM namba yangu nawe unaweza nitumia namba yako.
 
Mkuu ninandikaujumbe huu nikiwa na lengo la kujifunza upandaji/kilimo cha vitunguu kupitia kwako tafadhali wasiliqna nami gap hapa +255657740797
 
Wazo ni zuri sana. Mimi nalima vitunguu Singida Wilaya mpya ya Mkarama Kata ya Mwanga.
Baraka alichosema kimsingi anapenda watu waweze kupanua mawazo kuelekea kwenye kilimo kitu ambacho nakiunga mkono sana. Tatizo ambalo hajaweza kulijua na huende anasikia siyo MKULIMA ekari moja inapandwa kilo tatu za mbegu. Bei za mbegu ni tofauti sana kulingana na maeneo kwa mfano Red Bombay ambazo tunazalisha sisi wenyewe huku mashambani debe moja halizidi laki moja.
Mbegu aina ya Neptune inapatikana Barton Tanzania Ltd inauzwa 120,000/- kwa nusu kilo, Red Caraoke ya South Afrika inauzwa 80,000/- kilo moja.
Kuhusu bei ya soko huyu ndugu anazungumzia Hapa Dar, hajasema huyo mkulima kutoka Mang'ora, au Singida Vijijini kwa bei anayosema dalali wa sokoni hamzungumzii najua huwezi kuleta bidhaa sokoni ukauza mpaka uwaone madalali.
Nina uzoefu mkubwa mwaka jana nilileta gunia 130 kwa mtu aliyesema angenunua akaja akaona mzigo akaufungua na kushona upya akatoa gunia 124 kwa bei ya 73,000/- wakati nimevitoa shambani singida akalipa advance millioni sita na laki tano pesa nyingine mpaka leo hajalipa simu hapokei.
Mwezi wa tano vitunguu shambani wanunuzi walileta bei ya shilingi 40,000/- hadi 50,000/- kwa gunia la wavu wanapakia viroba vitatu wanasema ni gunia moja, nikaona ni bora nilete vitunguu soko la misuna singida mjini, bei yao ilikuwa shilingi 53,000/- kwa gunia moja. Ushuru ni shs 1000/- kwa gunia, dalali 2,000/- kwa gunia, wanaochmbua shs 1,000/- kwa gunia, mshonaji 1,000/- kwa gunia nilikuwa na gunia 67.
Rafiki bei ya vitunguu haijawa na msimamo inategemea baraka za madalali na wingi wa mzigo uliopo sokoni.
Nitakupigia Baraka simu ila ukweli ndio huo.

Tafadhali ndugu,naomba tuwasiliane kwa kina juu ya mbegu bora,natarajia kufanya kilimo cha vitunguu msimu huu,ila swala la mbegu linanitatiza sana,Kuna watu wamenishauri kuwa mbegu ya singida ni nzuri sana lakini sijawa sure na hill,tafadhali naomba tuwasiliane,0714808196,0765781288,nipo morogoro.
 
Mtoa mada ulishawai kuwa mwalimu nini maana umejitoa sana kutoa mada na kujibu maswali.Big up mola akuzidishie.

Niliwai lima kitunguu Nyanzwa mwaka ulikuwa sio wenyewe nikala mweleka maji yalikuwa ya mgao.

Ila sijakata tamaa, kuna eneo chanika nitatest zali mpaka kieleweke maana ni karibu na soko tofauti na iringa
Nishatuma namba yangu pls niadd kwa whats up tuwe twapeana updates hasa za masoko
 
Wakuu msaada wenu wa uelewa kwenye kilimo cha vitunguu maana ndio nimeingia msimu wa kwanza kwa kuunga unga lakini sio mbaya sana najitahidi na nimeamua kufanya kilimo na kuachana na ajira kwani naona ntakuwa kwenye position nzuri zaidi.

Concern yangu kubwa nilitaka ushauri kwa mwenye uzoefu wa hiki kilimo kuanzia mandalizi ya shamba aina ya udongo unaofaa paka madawa,mimi nipo Ifakara morogoro..
 
Mbona wadau mliyokuwa mna changia sana mwezi wa saba mwishoni hadi mwezi wa nane kuhusu bei za vitunguu mmenyamaza ghafla, ingependeza kama mrejesho wa changamoto mlivyoitatua ingeletwa hapa kwa manufaa wa wengine, was it a win or a lose situation?

Ndio maisha jamani, msipotee mazima
 
Back
Top Bottom