Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Acha izo mahesabu yako ya mbolea,maji na dawa yanafka karibu 1500000 then wasema gharama za had kuvuna ni karibu million moja aisee embu fanya research zaid kuliko kudanganya watu
 
Ni 60000 Jamaa kazngua

Sorry ni spelling error kwenye hiyo 60,000 kumbuka situmii excel hapa hivyo ni rahisi kupata spelling error kama hiyo.

Angalia kwenye nyekundu hapo juu nawe umefanya kosa. Hebu tusijikite kwenye ubishani maana lengo letu ni kuelimishana na kupeana njia ya ukweli. Badala ya kubisha kwa hasira, hebu toa wewe mchanganuo wako kama mimi ili wangalau utoe picha ya ukweli kwa upande wako.

Mimi hiki kitu nimefanya kwa vitendo wala sio nahadithiwa.
 
Tupo pamoja wewe walimia wapi
 

Huu ujasiriamali wa kilimo na mifugo ni kitu tumefanya na bado tunafanya kama wito. Ki ujumla mimi nina ahueni lakini kwa walio wengi naona wakiingia na kuishia kukwama. Ni kwanini inatokea hivyo?

Wakati unaingia kwenye hizi shughuli sehemu kubwa utakuwa unaambiwa mafanikio tu, hakuna anayekuambia mapungufu yake, lakini ukiingia kwenye ngoma ndio utajua mziki wake. Nakuunga mkono kwa kusema unahitaji uvumilivu sana.

Kwa kweli huku kwenye kilimo na ufugaji kuna maslahi duni sana kutokana na sera za nchi kwenye upande wa kilimo. Ukiona zao zinalipa vizuri ni kutokana na uhaba wake sokoni, lakini mara nyingi bei yake ina faida kidogo sana kulinganisha na gharama ya zao husika.

Na walio wengi wanataja bei ya juu wakati wa uhaba sokoni lakini sio kila mara zote utakutana na uhaba, kwani wengi wanalima wakati wa msimu, hivyo ni wazi utaingiza mzigo sokoni soko likiwa limefurika.

Haya mambo tunayafanya kwa vitendo, hao vijana wa TAYOA wao wamesema mafanikio tu, lakini hakuna mahali wameonyesha changamoto. Ama ukipenda jaribu kuangalia wanaonzisha mada za kilimo uone kama wanaweza kurudi ndani ya miaka miwili wakatoa feedback ya wapi wamefikia.

Hii ni kwasababu changamoto zinakuwa nyingi kuliko matarajio ya awali hivyo hawawi kwenye nafasi nzuri ya kutoa mrejesho.
 
Tupo pamoja wewe walimia wapi

Nimelima Arusha, na pia nimelima msitu wa mbogo moshi. Hizo gharama nilizoainisha nimekutana nazo na nimelima mara 3 ndani ya miaka 6. Mara zote gharama za uendeshaji zimekuwa na tofauti kidogo. Wakati naingia nilitajiwa mafanikio tu, tena bei niliyotajiwa ni ile inayotokea wakati wa uhaba. Ila chagamoto nilizokutana nazo ni nyingi inabidi nipate page kama 2 hivi kuzielezea ukweli kuhusu kilimo hiki kwa upande wa huku. Mimi nimelima kwa kukodi shamba, kila kitu kinahitaji pesa hivyo kujikuta gharama inakuwa kubwa sana.

Haya mambo ili tufanikiwe inabidi tuambiane ukweli na kwa sehemu kubwa inabidi serekali yetu isadie ama inabidi sisi wakulima tuwe na umoja wa kusimamia bei, vinginevyo madalali wataendelea kutajirika kwa mgongo wetu.

Sisi wakulima tunauza gunia kwa macho, wakati wao wanaenda kuuza kwa kilo, tena wanachukua kitunguu bora tu kilichokolea rangi, unaweza kukuta umepata labda gunia 70 kwa heka, lakini wakichambua wakapata gunia 40 zenye ubora wanaotaka wao na wananua bei wanayopanga wao. Hivyo wasivyovitaka wanaweza kununua kama vile takataka.

Kwa kweli inauma, inakwamisha na inafedhehesha. Sitaki kukumbuka siku niko na mke wangu shambani tukitajiwa bei iliyotuacha na hasara huku ada na kila kitu kinatusubiri.
 
Habari njema lakini ni muhimu pia kubainisha changamoto kuu za ujasiria mali huo na kutoa mapendekezo ya hatua na mikakati muhimu ya kurekebisha mambo na kukuza tija. Watu wangependa kujua kama kilimo kinalipa hivyo inakuwaje wakulima wabakie kuwa tabaka la chini sana kimaisha hapa nchini?

Ilivyoandikwa hapa imekaa zaidi kama promo tena ya kisiasa. Hii kauli ya kuhusisha mradi na kauli ya Magufuli kutaka vijana wafanye kazi badala ya kucheza pool si muafaka hapa. Harakati za vijana katika uzalishaji ni za enzi na enzi. Hazihitaji kauli za kisiasa. Vijana wengi wanajituma lakini kuna changamoto nyingi zinazowarudisha nyuma.

Onyesha mafanikio wengi watajiunga. Wavivu walikuwepo, wapo na watakuwepo. Lakini mahitaji ya kuishi hayaruhusu wawe wengi.
 
Wao wako dodoma ndiko wanakolima inawezekana hata soko kwao ni zuri, wewe uko wapi mkuu!?
 
Nalima Arusha na Kilimanjaro, tena ni ukanda wenye kutoa kitunguu bora tu.
Ok poa mkuu, yawezekana dodoma kuna soko zuri ukizingatia ni nusu jangwa hivyo ushindani ni mdogo.
 
Ok poa mkuu, yawezekana dodoma kuna soko zuri ukizingatia ni nusu jangwa hivyo ushindani ni mdogo.

Sina tatizo na hilo, wao wamezungumzia tu bei ya kuuza, je gharama za uzalishaji ziko wapi? Changamoto pia hawajaainisha. Kama ni hivyo huo umasikini wa watu wengi wa dodoma unasababishwa na nini?

Lazima ujiulize kuhusu ukweli wa hawa vijana, sipingi walichokisema lakini wameleta ukweli nusu. Wakieleza hali halisi kwa ufasaha na sisi ni wajasiriamali tunaweza kwenda kujaribu huko.
 
Wewe bei kwa gunia unauza shilingi? Nainaonekana unauzia shamba.
 
uko sawa mkuu watu wanaelezewa faida tu bila changamoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…