na mm nipo interested na hii kitu nipo moshi..........kama uneza taka partnership npo tayarNaomba kujuzwa gharama za kilimo cha vitunguu kwa heka moja wadau, kwa Iringa na Kilimanjaro
Nawasilisha
Thanks mkuu uko vizur ,big upMkuu tindo tatizo lako dogo tu. Ilikuwa mara ya kwanza kulima ulipaswa uanze kidogo ili ujifunze kwa gharama kidogo. Biashara yoyote unapoianza mara ya kkwanza mieleka ni kawaida, kama unapojifunza kuendesha baiskeli. Mtu asitarajie anapoanza jambo kwa mara ya kwanza apige bingo haiko hivyo. Pia ukae ukijua kuwa kunapokuwa na mafuriko ya zao sokoni wanunuzi wote na si madalali peke yao hunyanyasa sana wakulima. Hali hiyo ipo katika kilimo cha nyanya pia. Mkoa wa Morogoro ukilima nyanya za kiangazi mwezi wa nane hadi wa kumi na moja huwa kuna mafuriko ya nyanya. anaevuna miezi hiyo na kkama ni mara yake ya kwanza ataapa kwamba nyanya si biashara. Kuna msemo huku NYANYA NINYANYUE NYANYA NINYANYASE. Soko zuri la vitunguu ni mwwezi March hadi June. Ukiweza kuwa na kitunguu majira hayo huna maumivu. wateja wanakutafuta na unaweza kuuza kwa utaratibu unaotaka wewe. wakati huo wewe mwenye mali ndio mjanja. suala la madalali linakuwa halina umuhimu na wala si lazima upeleke sokoni na hata ukipeleka sokoni mzigo wako utagombaniwa.
Tumia utaallam uweze kuhifadhi kitunguu uweze kulifikia soko la Mwezi March, au lima vitunguu uvune February au uvune kuanzia mwezi May hadi July. Ukilima kitunguu cha msimu ambacho kila mtu analima maumivu yake ndiyo hayo. Kwenye suala la soko kunapokuwa na mafuriko hakuna serikali itakayokusaidia hapo utakuwa umeumia tu. wewe mkulima ndiyo unatakiwa uchemshe bongo kuona utalifikia vipi soko la mwezi March hadi July. Hii miezi hakuna dalali atakae kunyanyasa. Na pia sio lazima upeleke mzigo sokoni kunawanunuzi wazuri tu hufuata mazao mashambani. watu wengi wanafanikiwa sana kwa kuuzia mashambani. kama huna uzoefu afadhari ukauzia shamba ukapata bei utakayoridhika nayo kuliko kwenda mjini ukakutana na madalali wajanja ukarudi kijijini na story tu huna pesa mfukoni.
Kwa hiyo Mkuu kila biashara inachangamoto zake. Tumia muda mwingi kujifunza kwa wazoefu badala ya kulalamika hivyo. Ulikosea kuanza kwa kulima pakubwa ukapata hasara ukarudia makosa yaleyale kwa kulima pakubwa zaidi huku hujarekebisha kilichokutia hasara ulipo anza. Ushauri wangu msimu wa kwanza jifunze mbinu za kilimo cha vitunguu uzijue changamoto zake. Msimu unaofuata boresha uzalishaji kwa kutatua changamoto, pata ushauri kwa wazoefu. Panua eneo kadri unavyopata uzoefu. Hata kama unauwezo mkubwakifedha usianze kuwekeza eneo kubwa kama huna uzoefu. Usivutiwe na takwimu tamu unazosikia nyingi hufikiwa na wazoefu na nyingi ni exagerated. Ukizalisha eneo dogo inakupa picha halisi itakayokufanya uamue iwapo kilimo hicho kinalipa au la. Na hapo ndiyo utaamua kupanua eneo la shamba kwa kutokana na picha halisi uliyoiona na changamoto zake.
Mkuu sheria namba moja ya kilimo ni tafuta soko ndio ulime hiyo mosi ,jingine tumia mbegu bora ndio utaona faida hizo mbegu za kupimiwa kwa ndoo hamna kitu ndg na ni kwa mazao yote ,tumia hybrid utaleta mrejesho mfano neptune nusu kilo mbegu ni 185,000/= eka moaja inahitaj kg1.5-2 ila eka moja ukiitunza hovyo gunia 80 ukiitunza vyema gunia 120,hapo hata ukiuza kwa bei ya elfu 80 gunia unafaida hizi mbegu za kawaida zikipata stress tu kwanza zinaacha kubeba kitunguu zinatoa maua ,kingine soma alama za nyakati ili uwin soko mkuuuMkuu Kubota nimependa mchanganuo wako, mimi niliwahi kulima vitunguu misimu miwili, msimu wa kwanza nilipata hasara ya shilingi laki tatu kwa kilimo cha heka moja. Msimu wa pili ndio ilikuwa funga kazi maana nilipata hasara ya 2 million kutoka kilimo cha heka mbili!! Changamoto nilozokutana nazo huku Arusha, bei ya kukodisha shamba ni kubwa, tulikuwa tunakodisha shamba sh 300,000 kwa heka. Bei ya pembejeo nayo iko juu sana kulinganisha na soko. Kuuza mazao wakati mzigo umejaa sokoni, yaani mali kuzidi mahitaji (demand na supply). Mwanzoni niliambiwa naweza kupata gunia 70-100 kwa heka, lakini sikuwahi kupata idadi hiyo ya magunia japo niliweka mahitaji yote kama inavyotakikana na kitunguu kilitoka vizuri sana kwa misimu yote. Tatizo kubwa nililiona wakati wa mauzo, hapa ndio mahali nilijua kilimo ni mwanaharamu na wakulima wataendelea kuwa maskini mpaka mwisho wa maisha yao kwa mtindo huu. Kitunguu hakipimwi kwa kilo huku bali kwa mtindo wa rumbesa. Unakuta gunia moja linabeba mpaka kilo 150. na bei yake haivuki 60,000 kwa gunia. Na mazingira yalivyo huuzi bila dalali, yaani pale ndio nilijua kwanini watu wengi wanalazimisha kubakia kwenye ofisi za kuajiriwa kuliko kujichanganya na kilimo. Na viongozi wetu hawana msaada wowote kwa huu uhuni tunaofanyiwa wakulima hasa wakati wa mauzo. Tatizo hili ni sugu na litaendelea kumfanya mkulima wa nchi hii kuwa maskini na kudharaulika daima (nadhani mmewahi kusikia msemo wa kejeli kama maisha yamekushinda kalime) Yaani kilimo kimegeuzwa kama sehemu ya kumkomoa mtu, eti utasikia ili kumkomoa mtu inabidi arudhishwe akalime, na ukijaribu kuangalia kama kweli mimi katika misimu yangu miwili ya kilimo cha kitunguu nimepata hasara unategemea nini?
Nini kifanyike, kama tunataka kweli kilimo iwe ni sehemu ya ajira inayolingana na jasho unalovuja ni lazima serekali iingilie kati na kusiwepo tena na manunuzi ya mazao ya mkulima kwa njia ya rumbesa bali kipimo iwe ni kwa kilo. Pembejeo zishushwe bei hata kama ni kwa ruzuku toka serekalini japo sidhani kama hili linawezekana kwani watunga sera za kilimo wao sio wakulima bali wafanya biashara. Iwapo sera haziboreshwa na kusimamiwa kwa umakini ni dhahiri wakulima hasa wadogo wadogo wataendelea kuwa maskini na mimi sintowashauri watu waache kazi za ajira huko maofisini hata kama wananyanyasika kwani huku kwenye kilimo ni kutafuta kufa siku si zako.
CC: Bavaria
Mkuu nina taka kuingia kwenye kilimo target yangu kubwa ni horticulture,sana ni kilimo cha mboga mboga ikiwemo vitunguu nyanya karoti na hoho wazo langu kuu ni kuanza na kitunguu mwakani nifanye deployment ya horticulture kwa kitunguu kwa eka moja.. nimesikia swala la mvua kunyesha na kuozesha vitunguu nataka nipate msaada wa kitaalamu pia na makadirio ya gharama za horticulture kwa hyo eka mojaTatizo mtu hajui abc za kilimo ila anataka nae alime ,jaman kulima sio kukwatua ardhi ni profession tumeikalia darasan tukaisoma ,hivi kama wewe ni mwanasheria,muhasibu,dereva,doctor any profession ni rahisi mtu yeyote kumuelekeza akafanya kazi yako !!!??? Jibu ndio utafahamu why kilimo ukiingia kichwa kichwa unaumia ,tumieni wataalam wa kilimo mlionao / wanaowazunguka kama mnataka kufanikiwa ndugu zanguni
Bado vikao vinaendelea?kasopa
Asante ndugu yangu.
Kama uko DSM niambie ili siku nikifika dar nikutafute, leo niko nje ya dar. Unaweza kushiriki vikao vyetu bila taabu. Hakuna kiingilio na hatumfichi mtu kitu tunachofanya. Tunajadili namna ya kushiriki uchumi wa nchi yetu na sio kuwa watazamaji.
Mkoa gani upo kiongoziSina utalamu sana na ardhi ya huko lakini ni mazao mazuri, japo kitunguu maji ningekushauri uje mkoani tupige kazi utafurahi....hila kwa ardhi za kisarawe sina hakina.
hiyo mboga hapo mkuu naipenda sana, huku kwetu adimu sana.Sina utalamu sana na ardhi ya huko lakini ni mazao mazuri, japo kitunguu maji ningekushauri uje mkoani tupige kazi utafurahi....hila kwa ardhi za kisarawe sina hakina.
kufunga irrigation system kama hiyo inagharimu tsh ngapi mkuu?Sina utalamu sana na ardhi ya huko lakini ni mazao mazuri, japo kitunguu maji ningekushauri uje mkoani tupige kazi utafurahi....hila kwa ardhi za kisarawe sina hakina.
Kwa jinsi ninavyofahamu mm, viutunguu vinastaw sehemu nyingi sana cha msingi ni maji....Wadau nataka kupanda vitunguu maji na pilipili hoho maeneo ya kisarawe.
Naomba wadau mnisaidie ushauri pamoja na soko .
Asante.
Sina utalamu sana na ardhi ya huko lakini ni mazao mazuri, japo kitunguu maji ningekushauri uje mkoani tupige kazi utafurahi....hila kwa ardhi za kisarawe sina hakina.