Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

poleeeeee mpendwa, nilikua naomba kuuliza miezi mizuri ya kulima vitunguu ni ipi?
 
naomba kukuuliza mpendwa kwa uko morogoro miezi ipi ni mizuri kulima vitunguu pia wanakodisha heka moja sh ngap?
 
mpendwa naomba kuuliza kwa morogoro miezi ipi ni mizur kwa kulima vitunguu pia wanakodisha heka moja kwa sh ngapi?
 
Kwanza hongera kwa kutaka kulima. Kwa Ushahuri Wangu, nenda Karatu - Mang'ola ili ukajifunze. Kulima usilime pale, nenda ukalime Singida. Mang'ola is very expensive. Kwa sababu ya madawa na mbolea. Wadudu wameshakuwa sugu. Haya ni maoni yangu
Asante sana kiongoz lkn singda ni sehem gan itafaa zaid
 
Kukisaidia zaidi ongea na wakulima wakupe vivid data hizi za mitandaoni mostly huwa si kweli kwenye mavuno ,kupata gunia nyingi inategemea ukubwa wa shamba na aina ya mbegu
 
Kukisaidia zaidi ongea na wakulima wakupe vivid data hizi za mitandaoni mostly huwa si kweli kwenye mavuno ,kupata gunia nyingi inategemea ukubwa wa shamba na aina ya mbegu
Adante mkuu itabid npite kwa wakulima wazoefu ili nipate uhalisia baada ya kupata theory za huku mitandaoni
 
Hongera mkuu kwa kuthubutu kwanza naomba nikuambie kuwa kitunguu boraa kinatokana na mbegu mostly F1, udongo pamoja na kuzingatia utaaalam katika kilimo.

Pia ili upate faida angalia msimu umekaaje kisha wewe lima kinyume na msimu hapo ndo utapata faida saana mkuu.

Fanya saveyi mkuu kwa wanaolima kitalaamu
 
Asante sana mkuu mapenz matam[emoji23]
Najipanga mwanzon mwa mwezi decemba niende mang'ola nikajifunze mengi zaid lkn kwa kuanzia niwaskilize kwanza wadau wangu mnipe hints
 
hybrid kama neptune usijaribu kama unategemea kuuza ndani ya nchi.

Ndani ya nchi lima mbegu za kawaida tu kama red bombay au red creole au mang'ola red au singida local.
 
MKUU
hybrid kama neptune usijaribu kama unategemea kuuza ndani ya nchi.

Ndani ya nchi lima mbegu za kawaida tu kama red bombay au red creole au mang'ola red au singida local.
UNAPOSEMA JAMBO JARIBU KUTOA NA UFAFANUZI MKUU. MIMI NIMEANZA MWAKA JANA KULIMA HII NEPTUNE NA NILIPATA BAGS 120 NA VISADO 3 NA SEHEM. NA NILUZA VIZURI TU. TATZO NILILOLIONA KATIKA HII MBEGU NI KUWA LICHA YA KUWA NI F1 LAKINI INASHAMBULIWA SAANA NA MAGONJWA SAANA SAANA KUANZIA KITALUNI LAKINI INA ZAA SAANA KULIKO HATA RED CREOLE. NILIANZA KULIMA RED BOMBAY MWAKA 2010 NA NILICHOGUNDUA NI KUWA BOMBAY F1 INA ZAA SAAANA PENGINE ZAID YA NEPTUNE LAKINI KITUNGUU CHAKE SIO CHA KUKAA SAANA KINAWAH KUHARIBIKA NA PIA NDO INAPENDWA SAANA HATA SOKONI INAFANYA VIZURI.

LAKINI UKIWA KAMA MKULIMA WA KISASA MWENYE MBINU MISIMU NA VIPIND NILIVYOVITAJA HAPO NI VIZURI SAANA MAAANA UNAKUTA HAKUNA KITUNGUU KABISA SOKONI NSO HAKUNA ANAEBAGUA KABISAAA
 
cute confetti

Kwa mororgoro Kitunguu kinalimwa maeneo ya Ulaya kilosa, Mvumi (km kama 20 kutoka Dumila), Dakawa, na huku mpakani mwa Iringa na Morogoro hapo Ruaha Mbuyuni

Jambo moja la kufahamu kitunguu kinapenda joto, na udongo uwe kichanga au tifutifu ili kiweze kutanuka, so hata kama uko dar na kuna maeno kama huko mkuranga au kibiti, au mto ruvu kwenye udongo huu ukiwa na maji unaweza lima kitunguu. UDONGO USIWE MFINYANZI WA KUTUAMISHA MAJI TAFADHALI.

Kwa hayo maeneo niliyokutajia nadhani (Sina hakika sana) Ruaha mbuyuni ndio itakuwa inaongoza kwa ughali wa kukodi shamba, mpaka mwaka jana November walikuwa wanakodisha eka moja kwa tsh 300,000 kwa msimu, na mwenye shamba anakupa na pump ila gharama za matengenezo na mafuta ni kwako

Jambo lingine la kuzingatia sana, plan unavyo plan mambo yako, FAHAMU KUWA kitunguu kinachukua wiki 6-8 kitaluni na siku 90 hadi 120 shambani MPAKA KUFIKIA KUKOMAA. Kitunguu HAKITAKI MAJI KABISA KIKIWA KIMEKOMAA, hivyo piga hesabu zako na UFAHAMU VYEMA KWA HILO ENEO LAKO UNALOTAKA KULIMA, ULIZIA JE MVUA ZINAANZA LINI??? , MVUA IKIKUTA KITUNGUU SHAMBANI NA KIKIWA KIMEKOMAAA HESABU HASARA KITAOZA CHOOTE.

Wadudu wasumbufu sana wa kitunguu ni Ng"onyo/Funza (Jina maarufu kwa wakulima)=Cut worm/Sota, huyu hukata miche saizi ya kiuno/juu ya uso wa ardhi huyu ndio husumbua sanaaa wakulima. Dawa yake mujarabu nia Match, au Dume, au Dimethoate

ASANTE

mpendwa naomba kuuliza kwa morogoro miezi ipi ni mizur kwa kulima vitunguu pia wanakodisha heka moja kwa sh ngapi?
 
tulu

Kwa Mororgoro Kitunguu kinalimwa maeneo ya Ulaya kilosa, Mvumi (km kama 20 kutoka Dumila), Dakawa, na huku mpakani mwa Iringa na Morogoro hapo Ruaha Mbuyuni

Jambo moja la kufahamu kitunguu kinapenda joto, na udongo uwe kichanga au tifutifu ili kiweze kutanuka, so hata kama uko dar na kuna maeno kama huko mkuranga au kibiti, au mto ruvu kwenye udongo huu ukiwa na maji unaweza lima kitunguu. UDONGO USIWE MFINYANZI WA KUTUAMISHA MAJI TAFADHALI.

Kwa hayo maeneo niliyokutajia nadhani (Sina hakika sana) Ruaha mbuyuni ndio itakuwa inaongoza kwa ughali wa kukodi shamba, mpaka mwaka jana November walikuwa wanakodisha eka moja kwa tsh 300,000 kwa msimu, na mwenye shamba anakupa na pump ila gharama za matengenezo na mafuta ni kwako

Jambo lingine la kuzingatia sana, plan unavyo plan mambo yako, FAHAMU KUWA kitunguu kinachukua wiki 6-8 kitaluni na siku 90 hadi 120 shambani MPAKA KUFIKIA KUKOMAA. Kitunguu HAKITAKI MAJI KABISA KIKIWA KIMEKOMAA, hivyo piga hesabu zako na UFAHAMU VYEMA KWA HILO ENEO LAKO UNALOTAKA KULIMA, ULIZIA JE MVUA ZINAANZA LINI??? , MVUA IKIKUTA KITUNGUU SHAMBANI NA KIKIWA KIMEKOMAAA HESABU HASARA KITAOZA CHOOTE.

Wadudu wasumbufu sana wa kitunguu ni Ng"onyo/Funza (Jina maarufu kwa wakulima)=Cut worm/Sota, huyu hukata miche saizi ya kiuno/juu ya uso wa ardhi huyu ndio husumbua sanaaa wakulima. Dawa yake mujarabu nia Match, au Dume, au Dimethoate

ASANTE

Naomba kuuliza wadau vitunguu Mororogoro vinalimwa wilaya gani na sehemu naomba brief yake wadau
 
Thanx mkuu maana nilikuwa blind
 
Too good to be true
 
Baada ya kufuatilia mijadala na ushauri wa watu mbali mbali humu jf Mimi niliamua Kujitosa katika kilimo cha vitunguu especially swaumu ambayo inaonekana siyo maarufu Sana ukilinganisha na vitunguu maji.

Kwa kuanzia nlianza na nusu eka kwa sababu bado nilikuwa na soma ila namshukuru mungu nilifanikiwa kupata tani 1,5, ila kiuhalisia huwa kwa nusu eka unapata tani 2.5.

Hivyo basi nikaamua kusubir bei ipande mpaka 4800-5000/= kwa kilo moja so nna uwezo wa kupata sh 7,200,000/= hadi 7,500,00/= kwenye mwezi wa January hadi march ntauza mzigo wangu

Kilimo kinalipa sana. Karibuni.....
 
ulitumia shulingi ngapi? shamba lilikuwa lako au la kukodi? unasema ulikuwa unasoma nani alikuwa anahudumia na je mgao ukoje?
 
ulitumia shulingi ngapi? shamba lilikuwa lako au la kukodi? unasema ulikuwa unasoma nani alikuwa anahudumia na je mgao ukoje?
Shamba nilikodi kwa miaka miwili iligharimu sh 1.000.000/=kwa miaka yote miwili kuhusu kuhudumia shamba nlimpata kijana ambaye alikuwa anasimamia shughuli zote za shamba kwahyo iligharimu Kama sh 500,000/= kwahiyo gharama yote ilikuwa 1,5m
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…