tulu
Kwa Mororgoro Kitunguu kinalimwa maeneo ya Ulaya kilosa, Mvumi (km kama 20 kutoka Dumila), Dakawa, na huku mpakani mwa Iringa na Morogoro hapo Ruaha Mbuyuni
Jambo moja la kufahamu kitunguu kinapenda joto, na udongo uwe kichanga au tifutifu ili kiweze kutanuka, so hata kama uko dar na kuna maeno kama huko mkuranga au kibiti, au mto ruvu kwenye udongo huu ukiwa na maji unaweza lima kitunguu.
UDONGO USIWE MFINYANZI WA KUTUAMISHA MAJI TAFADHALI.
Kwa hayo maeneo niliyokutajia nadhani (Sina hakika sana) Ruaha mbuyuni ndio itakuwa inaongoza kwa ughali wa kukodi shamba, mpaka mwaka jana November walikuwa wanakodisha eka moja kwa tsh 300,000 kwa msimu, na mwenye shamba anakupa na pump ila gharama za matengenezo na mafuta ni kwako
Jambo lingine la kuzingatia sana, plan unavyo plan mambo yako, FAHAMU KUWA kitunguu kinachukua wiki 6-8 kitaluni na siku 90 hadi 120 shambani MPAKA KUFIKIA KUKOMAA. Kitunguu HAKITAKI MAJI KABISA KIKIWA KIMEKOMAA, hivyo piga hesabu zako na UFAHAMU VYEMA KWA HILO ENEO LAKO UNALOTAKA KULIMA, ULIZIA JE MVUA ZINAANZA LINI??? , MVUA IKIKUTA KITUNGUU SHAMBANI NA KIKIWA KIMEKOMAAA HESABU HASARA KITAOZA CHOOTE.
Wadudu wasumbufu sana wa kitunguu ni Ng"onyo/Funza (Jina maarufu kwa wakulima)=Cut worm/Sota, huyu hukata miche saizi ya kiuno/juu ya uso wa ardhi huyu ndio husumbua sanaaa wakulima. Dawa yake mujarabu nia Match, au Dume, au Dimethoate
ASANTE