Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Wadau mim ni mkuwa wa vitunguu ila sijawahi kulima kipindi cha masika nataka nijaribu kipindi hiki nalimia mkoani dodoma naomba mwenye experience wa kulima kipindi hiki anipe ushauri nini changamoto risk ikoje na namna ya anavyokabiliana nayo
 
Huvijui Vitunguu Wewe. Acha Mbwembe Ya Kujifanya Unauzoefu hili sio jukwaa la jokes. Kajipange kisha urudi hapa kuuliza mambo yatakayokusaidia kubadili maisha yako.
 
Nashukuru wadau,nimefatilia uzi huu..nimejifunza mengi sn, Naingia katika kilimo kwa mapendo yangu na sio ushawishi, nahitaji mafunzo mengi wadau.
 
Hatimaye bei ya vitunguu imepanda mara dufu Dar es Salaam. Gunia sasa ni Tshs. 110,000 hadi 130,000. Mliofanikiwa kutunza kama mimi tupige pesa sasa.

Nilitegemea kuona statement kama hii muda wowote kipindi hiki. Hivyo mmeprove kuwa kipindi hiki ndio hot kwa mauzo ya zao hili.

Sasa nilitaka kuuliza, je kuna mtu yeyote ameshawahi kutumia ushauri wa wataalamu wa BALTON? au YARA?

Maana nimeambiwa ukiwatumia hao, hakika utapata maximum production.

Any experience ya kuwatumia watu hao?
 
Mimi pia nimeingia katka kilimo hiki cha vituguu na kwasasa nimemwanga mbengu na wiki ijayo ntaanza kupanda, nimeandaa heka tano hivi ambazo naanza nazo... Kama itanilipa ntapanua zaidi ingawa garama yake ni kubwa sn, nko nakima Moshi... Asanten wadau kwa kututia moyo aisee

Mkuu walima moshi pande gani mkuu
 
Baada ya kununua Power tiller,
Nunua Water pump na mipira mirefu ya kutosha.
Nenda kariakoo kwa wahindi.
 
Vitungui ni balaaa. Me nimelima sikutoa hata robo eka ktk eka 6
 
Natoa huduma ya Kukufungia Greenhouse ya bei nafuu kabisa. 8m by 18m with complete Drip irrigation system & 1000lt Tank plus Free Extension Service for 3month kwa TSHS.3,200,000/- ONLY. just call 0772668500
 
Uje mbeya
Kukod shamba 50000
Mbegu gram 400-500
Gram 100-25000
Kulima 50000
Vitalu kwa ajur ya kupanda 50000
Kupanda 100000
Dawa ya palizi 40000
Paluz 3
Mbolea 150000
Madawa tote 150000
Kuvuna 100000
Hapo unaweza kuvuna gunia had 90 hakuna migogoro ya maji yapo kubao unwagiria SAA yeyote ukitaka coll me 0759185832
 
Realtor,'

Kuna sehemu fulani inaitwa ruaha mbuyuni, hapo bwana kilimo hakitegemei mvua, kitunguu kinakubali sana hapo mpendwa, vilevile uzuri wa hapo ni kwamba unawezakulima vitunguu marambili kwa mwaka, ukitoa kitunguu unaweza kulima mahindi mara mbili na maharage mwaka huo huo mmoja. Yaani ardhi ya hapo inakubali karibu kila kitu na serikali imeshapaendeleza.

Ukiweza kupapata hapo utafaidika sana lkn bei sio zile za elfu 50 kwa hekari,bei hapo ni kubwa na ni vigumu kidogo kupata eneo maana tayari mabebari tumeshayakamata,,(kidding).

ni-PM kama unataka maelezo ya zaidi naweza kukusaidia.
Nimekuwa interested na maelezo yako bepari..kidding!!naomba namba yako tuongee
 
Last edited by a moderator:
kiukweli waliokuwa wanatushawishi kulima niwaongo, ni vigumu kupata hizo gunia 100 wastan ni gunia 40. pia nimeamin wengi wao nahisi niwafanyakaz wa maeneo hayo kwa hiyo wanakuwa wanakupiga kwenye mbegu, mimi mwaka jana nimejaribu ila nilikuwa tofauti na wenzangu mimi nilinunua lita moja tu za mbegu.

Kiukweli ni mbegu nyingi sana kwa ufupi wasiozijua ni vimbegu vyenyewe ni saiz ya mbegu ya nyanya na baada ya kuzihudumia nilifanikiwa kupanda zote na chache zilibaki, pia sikutaka kubana sana kama wengi wetu wanavyoshauri humu eti size ya kiberiti.

kuhusu dawa mara nyingi nilipulizia dawa ya kuzuia wadudu tu tena mara moja kwa wiki kopo nilikuwa nanunua buku tano mpaka navuna nilitumia kopo kumi ambayo total ilikuwa 50000.
mbolea kwetu huku zipo za kununua mchanganyiko ila mimi nilinunua mfuko mmoja mmoja kwa kila mbolea na bei zake kwa mbeya ni
urea 48000
can48000
npk nilikuwa nanunua ya unga inauzwa 5000 na kila baada ya siku 14
sa 45000
uchumi haukuwa mzuri sikununua dap
kuandaa kitalu mpaka kupandikiza jumla ya matumizi ilikuwa35000 na mimk mwenyewe nilikuwa nashiriki.
nilivuna jumla gunia25 kwa eka moja.

NILICHOJIFUNZA
watu wanadanywa kuhusiana mbegu hivo wanajikuta wananunua mbegu nyingi na kumwaga shamban. hata wakati wakupandikiza vitunguu vinabanwa sana hivyo mbegu nyingi inakufa au mkulima anajikuta anapata vitunguu vidogovidogo vingi sana badala ya vile vya wastan. pia mbolea inatakiwa iwekwe kila baada ya siku ishirini na moja na ingependeza upandikize kwa mstari hata wakat wa kumwaga mbolea ufuatishe mstari badala ya kumwaga ovy sabab ukimwaga onyo wakati wakumwagilia mbolea inaweza sombwa na kujikuta ni sehem moja ndo imenawili tena kwa muono wangu ni vyema kupitisha mstari wa kishimo pembeni ya mstari wa vitunguu na uksha mwaga ufukie.
kwa ushauri wangu ni vyema kama ndo unaanza ushiriki mwenye kwa usaidiz wa wafanyakazi kuna uongo mwingi sana unaenezwa ambao ndo unawaliza wengi humu.

mtu anakwambia unahukika wa kuvuna gunia 100. wadau gunia linalozungumzwa hapa sio kilo mia ni debe nane ambalo si chini ya kg 130 sasa hata ukiingia kenyanseed.com hizo mbegu za red bombay na redcreole wamekadilia kg 10000 per hectare ambazo ni acre 2.5 pia kitunguu kwa jinsi nilivoona ukijitoa mwenyewe kwa usimamizi mzuri hupaswi kufikisha gharama ya milion.

pia tusikariri maeneo mfano lumuma wenyeji washakuwa matapeli wanapokuona mgeni wenyewe wanachofikiria ni kukukamua tu. pamoja na kuwa bei haikuwa nzuri lakini nashukuru gharama yangu ilirudi na faida pia. twenden shamban lakini kabla ya yote tutafute information bila kukurupuka. love you all. sikuwahi kulima ila mwaka huu mungu bariki ntalima kila kitu mpaka nyanya
 
Well said and Mungu akubariki , maana umetenda wema na kutoa ufafanuzi mzuri na wenye uhakika
 
Back
Top Bottom