Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Baada ya kufuatilia mijadala na ushauri wa watu mbali mbali humu jf Mimi niliamua Kujitosa katika kilimo cha vitunguu especially swaumu ambayo inaonekana siyo maarufu Sana ukilinganisha na vitunguu maji.Kwa kuanzia nlianza na nusu eka kwa sababu bado nilikuwa na soma ila namshukuru mungu nilifanikiwa kupata tani 1,5, ila kiuhalisia huwa kwa nusu eka unapata tani 2.5.Hivyo basi nikaamua kusubir bei ipande mpaka 4800-5000/= kwa kilo moja so nna uwezo wa kupata sh 7,200,000/= hadi 7,500,00/= kwenye mwezi wa January hadi march ntauza mzigo wangu
Kilimo kinalipa sana. Karibuni.....
Mkuu tueleze changamoto haswa ulizokutana nazo mpaka kuvuna
 
Shamba nilikodi kwa miaka miwili iligharimu sh 1.000.000/=kwa miaka yote miwili kuhusu kuhudumia shamba nlimpata kijana ambaye alikuwa anasimamia shughuli zote za shamba kwahyo iligharimu Kama sh 500,000/= kwahiyo gharama yote ilikuwa 1,5m
Hongera mkuu,

Swali langu naona kama uleelezea Gharama za kukodi 1M na msimamizi laki 5. Vipi kuhusu Gharama za Mbegu, Madawa nk...
Na je kilimo hicho ni mkoa gani?
 
Mbegu nilinunua kg 500 ukinunua wakati wa mavuno utapata kwa 1200@kg so inakuwa laki 6 na dawa nilitumia laki 2 na palizi ilikuwa laki 1,5 pamoja na umwagiliaji, msimamizi nlikuwa simlipi direct yeye nlikuwa namsaidia kumnununilia dawa ktk shamba lake ambalo liko karibu na la kwangu, so cost ikawa laki 1.5 ukiongezea na laki 3.5 hapo juu unapata laki 5.

Kuhusu mkoa ni Manyara maeneo ya Bashay wilaya ya Mbulu
 
Changamoto kubwa ilikuwa kutu katika majani na bursting mana dawa zake zilikuwa ghali Sana na huwa hazisaidii Sana Kama kuna wataalamu humu watanisaidia ni dawa zipi nzur kwa kutu(rust)
Cc @kilimoutajiri.maarifa
 
Hongera mkuu,

Swali langu naona kama uleelezea Gharama za kukodi 1M na msimamizi laki 5. Vipi kuhusu Gharama za Mbegu, Madawa nk...
Na je kilimo hicho ni mkoa gani?
Asante mkuu, sorry unaweza kujua kwanini gharama za kukodi shamba zikawa juu hivyo? ni nusu ekari ulikodi kwa milioni moja ama ni eneo kubwa zaidi ya hilo na wewe ukaamua kulima nusu ekari tu?
 
Asante mkuu, sorry unaweza kujua kwanini gharama za kukodi shamba zikawa juu hivyo? ni nusu ekari ulikodi kwa milioni moja ama ni eneo kubwa zaidi ya hilo na wewe ukaamua kulima nusu ekari tu?
Mkuu huku kupata shamba ni changamoto kwa sababu watu wameshajua faida ya kilimo hiki ndo mana wanakodisha kwa bei kubwa kidogo...
 
Mkuu kwa upande wa mbolea uliweka mbolea gani? Kiasi gani hadi kuvuna nusu heka? Bei ya mbegu kilo 1200 ilikuwa ni mwezi gani?

Je ulinunua ikiwa bei rahisi (wakati wa mavuno) au ghali? Ulipanda aina gani ya vitunguu kati vile vikubwa vyeupe au vile vidogo vya kawaida?
 
ngoja nitulie nijifunze. huko bashay ni baridi, joto au wastani? ni miezi gani wanavuna.
 
Upepo wa Pesa
ASANTE MKUU

Kwa mujibu wa ndugu
[URL='https://www.jamiiforums.com/members/lucky01.399662/']Lucky01

alipambana na magonjwa ya rust (Kutu ya majani/Fangasi ), kwenye bursting hapo sijampata vizuri kama anamaanisha vitunguu kupasuka (pacha) hiyo si fangasi bali ni upungufu wa lishe ya Calcium (ALipaswa ahakikishe pale kilipoanza kufunga mbolea za Calcium kama CAN/Yara Nitrabor hazikosi) na huku juu akiendelea kusparay booster hasa zenye Sulphur (S) KWA WINGI ili kuongeza ile Aroma (Harufu)

SULUHU.
Kwa matatizo ya kutu ni vyema kufanya yafutayo ili kujikinga na hizo shida

1.Epuka kumwagia maji jioni, yakatuama na yaka lala shambani, baadhi ya wakulima hufanya hivi. Hii huleta umande mwingi wakati wa usiku, na umande/unyevu ni mazingira rafiki ya fangasi kumea, hivyo mwagia mapema kama ni asubuhi mwagia kuanzia hata sa 12 hadi sa 5 hivi inatosha, kama ni jioni anza mapema ili kufika sa 12 jioni uwe umemaliza maji yasituame

2. Kwa upande wa dawa za kujikinga na ukungu, ni dawa zooote zenye viambata vifuatavyo (Propneb-Mfano ipo inayoitwa Milraz), Copper (Mfano Bluue Copper/Nordox/Fungurani), Mancozeb (Mfano Farmazebo), Cholothalonil (Mfano-Damka/Banko/Odeonetc) , Hexaconazole (Mfano Xantho); Kipimo ni mls /gram 30-60 kwa maji lita 15, kama kuna ukungu mwingi piga kila baada ya siku 7

3. Za kutibu ukungu. Ni Amista extra (Kiambata-Azoxtrobin +Hexaconazole), Multi power 78 PLus WP (Kiambata Myocin), Agrifos 400 (Kiambata PAS-Phosporic Acid Salt-Di-Mo Potassium Phosphate). Nativo, etc

========

Cc @kilimoutajiri.maarifa
 
Baada ya kufuatilia mijadala na ushauri wa watu mbali mbali humu jf Mimi niliamua Kujitosa katika kilimo cha vitunguu especially swaumu ambayo inaonekana siyo maarufu Sana ukilinganisha na vitunguu maji.Kwa kuanzia nlianza na nusu eka kwa sababu bado nilikuwa na soma ila namshukuru mungu nilifanikiwa kupata tani 1,5, ila kiuhalisia huwa kwa nusu eka unapata tani 2.5.Hivyo basi nikaamua kusubir bei ipande mpaka 4800-5000/= kwa kilo moja so nna uwezo wa kupata sh 7,200,000/= hadi 7,500,00/= kwenye mwezi wa January hadi march ntauza mzigo wangu
Kilimo kinalipa sana. Karibuni.....
Good luck
 
Nmekuelewa na umentamanisha kweli mkuu maelezo yako mepesi na yanaeleweka asante
 
Back
Top Bottom