Kilimo kinalipa kama ukikifanya kama kazi

Kilimo kinalipa kama ukikifanya kama kazi

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,047
Reaction score
1,832
Natoa ushuhuda wangu wa kilimo cha mahindi nilichofanya msimu wa 2022

Niliandaa shamba ekari 3 kwa tsh 180,000.

Nilinunua mbegu aina ya Dk mifuko 7 ya kilo 2 kwa garama ya tsh 91,000.

Gharama za kupandà ni tsh 60,000.

Palizi 180,000.

Jumla ya garama zote ni tsh 511,000.

Mavuno niliyopata ni gunia 22.

Bei ya gunia moja kwa sasa ni elfu 95.

Siwezi kuuza sasa hivi kwa sasa nitayahifadhi mpaka mwaķani mwezi wa pili.

NB:
Mbegu zimeìngia chache sababu shamba lina mazao mengine kama michungwa, minazi na miģomba
Vijana tuacheni kulalamika kilimo kinalipa ukiwa makini
 
Kweli.. kabisa, mimi niliogopa kulima mahindi nikaamua kupanda viaz na mihogo kulinda shamba, dalali kanipigia simu anataka viazi lishe kwa 800/kg...

Nimeamua kuwa serious na kuacha uvivu pia kuweka degree pembeni...
 
Natoa ushuhuda wangu wa kilimo cha mahindi nilichofanya msimu wa 2022

Niliandaa shamba ekari 3 kwa tsh 180,000.

Nilinunua mbegu aina ya Dk mifuko 7 ya kilo 2 kwa garama ya tsh 91,000.

Gharama za kupandà ni tsh 60,000.

Palizi 180,000.

Jumla ya garama zote ni tsh 511,000.

Mavuno niliyopata ni gunia 22.

Bei ya gunia moja kwa sasa ni elfu 95.

Siwezi kuuza sasa hivi kwa sasa nitayahifadhi mpaka mwaķani mwezi wa pili.

NB: Mbegu zimeìngia chache sababu shamba lina mazao mengine kama michungwa, minazi na miģomba
Vijana tuacheni kulalamika kilimo kinalipa ukiwa makini
Heka zote hizo Gunia22!hasara itakuinua bei hiyo February2023,Omba usikutane na mahindi ya Zambia.
 
Yaani ikifika mwakani mwezi wa tatu au wa nne naamini nitapata mtajì wa kulimia na wa biashara, naamini gunia moja la mahindi si chini ya 150000
Tazama hapa kwa makini;
Gunia 20 ×150,000 = 3m.
3M tukisie imekaa shamba kwa miezi 10,,,Ukiigawa kwa miezi 10 utapata Laki tatu kwa mwezi,,,,,Laki tatu igawe kwa siku 30 utapata elfu kumi kwa siku,,,,duh kazi nzuri.
Hujagusia mbolea au ardhi inajitosheleza?
 
Yaani ikifika mwakani mwezi wa tatu au wa nne naamini nitapata mtajì wa kulimia na wa biashara, naamini gunia moja la mahindi si chini ya 150000
Labda vuli isinyeshe, mvua za vuli zikinyesha, mwezi pili watu wanavuna na bei inaporomoka ghafla.
 
Tazama hapa kwa makini;
Gunia 20 ×150,000 = 3m.
3M tukisie imekaa shamba kwa miezi 10,,,Ukiigawa kwa miezi 10 utapata Laki tatu kwa mwezi,,,,,Laki tatu igawe kwa siku 30 utapata elfu kumi kwa siku,,,,duh kazi nzuri.
Hujagusia mbolea au ardhi inajitosheleza?
Sijatumia mbolea inajitosheleza kwenye ardhi
 
Back
Top Bottom